TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Binafsi napongeza uongozi wa jf maana nimekuwa kati ya wana warsha walio shiriki katika uzinduzi wa program hii kigamboni ingawa nimegundua mengi ambayo kimsingi jimbo ili nadhani dr ndungulire atajitaidi kufanya alivyo aidi. Si haba nikachangia kwa upande wa kagera maana ni kwetu ila jambo msingi hapa ni kuwa kila mwanakagera ashiriki kikamilifu na sio kumwachia mbunge.ningeoenda nione ahadi za mbunge hyu walau nishiriki kumkumbusha pale atakaposahau
Ahadi zipo mkuu sema kama unavyotamani, sie nasi tunafanya kumkumbusha lakini kitu kimoja dhahiri, ni kwamba ama anakikimbia kivuli chake ama si mtumiaji mzuri wa mitandao
 
Binafsi napongeza uongozi wa jf maana nimekuwa kati ya wana warsha walio shiriki katika uzinduzi wa program hii kigamboni ingawa nimegundua mengi ambayo kimsingi jimbo ili nadhani dr ndungulire atajitaidi kufanya alivyo aidi. Si haba nikachangia kwa upande wa kagera maana ni kwetu ila jambo msingi hapa ni kuwa kila mwanakagera ashiriki kikamilifu na sio kumwachia mbunge.ningeoenda nione ahadi za mbunge hyu walau nishiriki kumkumbusha pale atakaposahau
Ahadi zipo mkuu sema kama unavyotamani, sie nasi tunafanya kumkumbusha lakini kitu kimoja dhahiri, ni kwamba ama anakikimbia kivuli chake ama si mtumiaji mzuri wa mitandao
 
Ahadi zipo mkuu sema kama unavyotamani, sie nasi tunafanya kumkumbusha lakini kitu kimoja dhahiri, ni kwamba ama anakikimbia kivuli chake ama si mtumiaji mzuri wa mitandao
Asante siku zake zinahesabika.
 
TUSHIRIKISHANE

da164d45284730d98edcb4e757cad3a6.jpg
 
Asante siku zake zinahesabika.
Ndugu sifi leo, vipaumbele vyetu ni;

1. Ujenzi wa soko kuu, soko la Kashai na standi ya mabasi

2. Urasimishaji makazi 10000

3. Mikopo kwa vikundi vya Vijana 100 na wanawake 150

4. Bima za afya 5000

Shukran kwa kufatilia
 
Ndugu sifi leo, vipaumbele vyetu ni;

1. Ujenzi wa soko kuu, soko la Kashai na standi ya mabasi

2. Urasimishaji makazi 10000

3. Mikopo kwa vikundi vya Vijana 100 na wanawake 150

4. Bima za afya 5000

Shukran kwa kufatilia
nimekuelwe sana nashukuru, hivi mfano Mbunge alivyo haidi mfano mikopo alieleza ni jinsi gani ataweza kutyoa mikopo? matahalani alizungumzia wapi atapata fedha za kutoa mikopo kwa vijana na wakina mama? na je ni akina vijana gani wajasiriamali au wa vijiweni?

Urasimishaji amejipanga kurasimisha vipi makazi, mathalani urasimishaji wa makazi atafanyaje?

Bima vipi atawezesha wananchi kukata bima? Tumekuwa na ahadi nyingi za watawala wengi ila huwa hatuelezwi ni kwa jinsi gani watatimiza ahadi wazitoazo.
 
MIKOPO KWA VIJANA

Tatizo la ajira ni zaidi ya linavyofikiriwa! Unaweza kuona mitaji ya vijana wengi wa hapa manispaa ni kiasi gani kwa kuangalia biashara za mfano wa hawa wanaoonekana pichani.

Ukiongea nao zaidi utagundua tatizo si mitaji tu na pia halianzii hapa Bukoba Manispaa.

1b3dc8c4f25511ee2727ba63957b9758.jpg
572302ab5ff2adeec6156fe06f727f47.jpg
379b96ced1baac1e81fbee55b38fe865.jpg
2c22194c8162c7052dc1d4f7120ebff9.jpg
e18d594fbdcaee3b8ac868f2cdf106f2.jpg
d21b9563626dc6d19e32a0af6af63bfb.jpg
45a23df0fce4c8540865b5887f85dbc9.jpg

5c8a15c760449d83d7200cb3d6f20545.jpg
5a590a972f4b2178220248dcfb707fff.jpg
 
nimekuelwe sana nashukuru, hivi mfano Mbunge alivyo haidi mfano mikopo alieleza ni jinsi gani ataweza kutyoa mikopo? matahalani alizungumzia wapi atapata fedha za kutoa mikopo kwa vijana na wakina mama? na je ni akina vijana gani wajasiriamali au wa vijiweni?

Urasimishaji amejipanga kurasimisha vipi makazi, mathalani urasimishaji wa makazi atafanyaje?

Bima vipi atawezesha wananchi kukata bima? Tumekuwa na ahadi nyingi za watawala wengi ila huwa hatuelezwi ni kwa jinsi gani watatimiza ahadi wazitoazo.
Maswali mazuri, ukipitia uzi huu kuanzia mwanzo utaelewa. Kama hutoelewa unaweza kuomba ufafanuzi zaidi na mbunge atakuja kujibu maswali na hoja zenu zote akipata muda. Lakini pia katibu wake anaweza kusaidia.
 
Maswali mazuri, ukipitia uzi huu kuanzia mwanzo utaelewa. Kama hutoelewa unaweza kuomba ufafanuzi zaidi na nafikiri ipo siku atakuja kujibu maswali na hoja zenu zote
Happiness nakuelewa sana na hakika unastaili kuwa afsa habari, nikuombe kitu kimoja rwakatare ni miongoni mwa member wa jf abu mkopi tunachokijadili ili aweze kujibu haya maswali yetu, kimsingi utoaji wa mikopo kwa vijana si jambo baya, ila ni jambo baya pale unapoitoa kama mikopo kwa vjiana kama ulio wapiga picha na mwishowe watu hawa wanatimuliwa na serikali kwa kuwapereka sehemu hisyo na wateja,au kutowapereka sehemu yyte hapo ndipo pesa za wabunge zinazopopotea. tatzo ninalo liona hapo ni kuwa ahadi nyingi ni unreastic to be fullfilied, pengine anatakiwa kuja hapa na kuonesha jinsi gani ataweza kutimiza ahadi hizo ili tuweze kusaidiana mawazo jinsi ya kutimiza ahad hizo
 
MRADI TARAJIWA WA SOKO VS SOKO LILILOPO KWA SASA

512a10d16b1bf85bb18dc59edb503433.jpg
adc75bfeb7eb60ac696f442bc0232b8e.jpg
65f6d2ab3ef1f0b616bcf1963f30e51e.jpg
48dc19bd417d4af3cc865f2fcc6914f0.jpg
9f4834cda248ea3c7624b78c42c0b0c5.jpg
34b125539ab837045f50f352799876c6.jpg
f37585906599ed2f888261ebeee195a7.jpg


HALI ILIVYO KWA SASA

7ef99609e8a60faf1b41b30f1b4ba902.jpg
ebb0ae37e68e43d355e82308231f2425.jpg
2b0b9cfbbdcc0623b36114152f35b909.jpg
d218e80a26d840a7426895c66d005bdd.jpg
baefe9adf92757013ea08704cda7bae2.jpg
458eba55c1b0b6ce89b671588ca50d01.jpg
100ef084628b952e66afb4cb738bdab0.jpg
ac8878a67ca05f60df9e2cc451afa45a.jpg
6b7fc829ef7c27b02f87d7a0389556ae.jpg
d41399974cd9125708ca00d3214e2dc1.jpg
a9eac8d13a03a589aa3302e2ce040bd1.jpg


Soko ni kipaumbele namba moja katika Tushirikishane. Wanabukoba wanahitaji kuona soko jipya kuliko kitu kingine chochote. Soko kuu linaathari kwa uchumi wa mkoa mzima si Bukoba tu!
 
Happiness nakuelewa sana na hakika unastaili kuwa afsa habari, nikuombe kitu kimoja rwakatare ni miongoni mwa member wa jf abu mkopi tunachokijadili ili aweze kujibu haya maswali yetu, kimsingi utoaji wa mikopo kwa vijana si jambo baya, ila ni jambo baya pale unapoitoa kama mikopo kwa vjiana kama ulio wapiga picha na mwishowe watu hawa wanatimuliwa na serikali kwa kuwapereka sehemu hisyo na wateja,au kutowapereka sehemu yyte hapo ndipo pesa za wabunge zinazopopotea. tatzo ninalo liona hapo ni kuwa ahadi nyingi ni unreastic to be fullfilied, pengine anatakiwa kuja hapa na kuonesha jinsi gani ataweza kutimiza ahadi hizo ili tuweze kusaidiana mawazo jinsi ya kutimiza ahad hizo
Nitafanya hivyo ili aweze kuja, shukran ndugu sifi

Jina zuri sana
 
TAARIFA YA MRADI YA AUGUST - OCTOBER, 2016


UTANGULIZI

Tushirikishane ni mradi unaowahusisha viongozi wa kuchaguliwa (mbunge na madiwani) serikali (halmashauri) na wananchi katika kufanikisha maendeleo. Wadau wakuu wa mradi huu ni Halmashauri ambayo ndiyo kitovu cha mipango ya maendeleo na utekelezaji wake, Mbunge ambaye ni msimamizi wa serikali (halmashauri), Jamiiforums ambao ni wasimamizi wa mradi na Wananchi.

Tushirikishane ilianza rasmi mwezi August katika jimbo la Bukoba mjini kwa kukutanisha wadau husika. Kundi la wananchi liliwakilishwa na makundi yote wakiwemo viongozi wa dini, wanawake, vijana, wazee, wafanyakazi na wafanya biashara mbalimbali wakiwemo bodaboda, n.k na kupitisha vipaumbele vinne ambavyo vimetokana na ahadi za mbunge alizotoa wakati wa kampeini. Vipaumbele hivyo ni;

1. Ujenzi wa Stand Kuu ya Mabasi, ujenzi wa Soko la Kuu na Soko la Kashai

2. Urasimishaji Makazi

3. Mikopo kwa Wanawake na Vijana, na

4. Bima ya Afya

Utekelezaji wa mradi unaanzia Halmashauri ambayo inasimamia miradi yote na inayotokana na vipaumbele vyetu vinne (4). Pia inatoa taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vipaumbele vyote. Mbunge katika mradi ni daraja kati ya manispaa na wananchi katika kuweka msukumo wa utekelezaji na kutoa taarifa kwa wananchi. Mbunge pia anatoa taarifa kwa JF juu ya kila hatua zinazofikiwa katika vipaumbele vya mradi. Halmashauri na mbunge wanawajibika moja kwa moja kwa wananchi. Jamiiforums ni mfatiliaji wa shughuli zote za mradi (utekelezaji wa vipaumbele) inatoa taarifa kwa wananchi juu ya mradi kupitia hapa, mitandao ya kijamii, magazeti, radio na mikutano midogo midogo katika kata zilizoko manispaa.

Hatua zilizokua zimefikiwa katika vipaumbele vyetu mwezi August zilikua ni za kuridhisha isipokuwa mwezi September shughuli za tetemo la ardhi zilikua nyingi zaidi kwa takriban mwezi mzima na hivyo kuchelewasha utekelezaji kwa kiasi flan. Kutokana na hili vipo vipaumbele ambavyo vimerudisha nyuma sana kutokana na athari ya tetemeko kama 'Urasimishaji Makazi'. Kutokana na hilo ripoti hii itaanzia August mpaka October ili kuweka mtiririko mzuri. Na baada ya hapa ripoti itakua ikiandaliwa ya kila mwezi.



TAARIFA

1.Ujenzi wa Soko Kuu

Lengo la Tushirikishane katika kipaumbele hiki ni angalau ifikapo April 2017, ujenzi uwe umeanza angalau kwa hatua ya msingi. Hatua zilizokwisha kukamilika mpka sasa ni zifuatazo;

- Tayari vikao vya OGM (mhandisi mshauri) na CTM vimekwishafanyika kuhusu nyaraka mbali mbali kama feasibility study, architectural drawings, engeneering drawings, geotechnical survey, bills of quantities, na tender document

- Kampuni hiyo ya OGM imekwishawssilisha taarifa yake ya utendaji kuhusu utayarishaji wa nyaraka za mradi kwa kamati ya ilinzi na usalama

- Michoro ya jengo, usanifu na upembuzi yakinifu umekamilika ukionyesha basement, ground floor ghorofa tatu na tower

- Ukokotoaji wa gharama za ujenzi uko tayari umekamilika ambapo itagharimu shilingi 13 bilion

- Upimaji wa hali ya udongo tayari umekamilika

- Uchunguzi wa athari ya mradi kimazingira umekamilika

- Nyaraka za zabuni zimeandaliwa

- Mazungumzo kati ya OGM na TIB na halmashauri juu ya kupata pesa yamekwishakufanyika. TIB wameahidi kutoa 70% ya pesa yote na halmashauri kutoa 30% katika mapato yake au kwa ubia

- Baraza la madiwan limekwishakutoa kibali cha kukopa

- Akaunti maalum imekwishafunguliwa

- Aidha business plan haijakamilika kwasababu OGM waliomba kulipwa ghrama yao ya 50,000,000/- ili kukamilisha kazi hiyo lakin manispaa haikuweza kuipata kutokana na kushuka kwa mapato. Badala yake manispaa imeiandikia barua TIB kuomba kulipa kampuni ya OGM deni lake lote la zaidi ya mil 400 kama sehemu ya pesa ya mradi wa ujenzi wa soko kuu

- Maombi ya eneo la KCU lililoko kati ya ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa na Mkombozi Commercial Bank yalifanyika kwaajili ya kuhamishia wafanyabiashara wa soko kuu kwa muda ili kupisha ujenzi. KCU wamekubali kutoa eneo

- Hatua inauofuata ni kukaa uongozi wa halmashauri pamoja na uongozi wa soko na wafanyabiasha kuweka mikakati ya kusonga mbele, kutangaza na kupata mzabuni, kuhamisha wafanyabiashara, kutaguta pesa hiyo 30%, n.k


2. Ujenzi wa Stand ya Mabasi

Vilevile katika ujenzi wa standi tuntegegema ifikapo April 2017, ujenzi uwe umeanza angalau kwa hatua ya msingi. Zifuatazo ni hatua zilizofikiwa;

- Fidia ya jumla ya 12, 967, 735/- imekwishalipwa kwa watu watatu ambao walikua hawajalipwa

- Eneo la hekta 6.53 limetengwa na kupimwa

- Mchoro umekwishaandaliwa

- Uchunguzi wa athari ya kimazingira umekwishafanyika

- Shirika la Mzinga Holding Cooperatio Ltd tawi la Morogoro limeingia makubaliano na manispaa lifanye kazi ya kuandaa feasibilitu study, ramani ya michoro na majengo, business plan, na kusaidia kutafuta mbia au mfadhili wa mradi

- Kazi zinazofuata ni kuandaa andiko la mradi na kutafuta fedha kwa wabia wau wafadhili ( Bank ya Dunia wameonyesha nia)


3.Mradi wa Ujenzi Soko Kashai

Ujenzi wa soko la Kashai tunatarajia uwe umeanza ifikapo April 2017. Zifuatazo ni hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wake;

- Michoro na usanifu tayari

- Andiko la mradi limekamilika

- Uchinguzi wa athari ya mrafi kimazingira umekamilika

- Nyaraka za zabuni zimekamilika

- Fedha za ujenzi bado zinaombwa kutoka bank ya dunia

4.Urasimishaji Makazi

Katika kipaumbele hiki tunatarajia kuwa zimesajiliwa nyumba zipatazo 10000 igikapo April 2017. Hizi ni hatua zilizofikiwa katika kipaumbele hiki;

- Zoezi la kuunganisha mitaa katika vikundi limekwishakamilika Kashai na Bakoba.

Kashai imewekwa katika vikundi vitatu;
i. Kashenya
Kilimahewa
National Housing

ii. Mafumbo
Matopeni
Lwome

iii. Kashai
Kisindi
Katatolwansi

Bakoba mitaa ni miwili;

i. Nyakanyasi
Mtoni

ii. Forodhani
Buyekela

- Gharama za kupima ni 200000 kwa kila nyimba ambazo zinawekwa katika akaunti za vikundi

- Tayari akaunti maalumu zimekwisha kufunguliwa kwa kata hizo mbili

- Wananchi wanaendelea kuelimishwa

Aidha, zoezi hili limeathiriwa sana na tetemeko la ardhi.

5.Mikopo kwa wanawake na Vijana.

Tunatarajia ifikapo April 2017, vikundi 250 viwe vimepata mkopo wa pesa ya 10% ya mapato ya manispaa inayotengwa kila mwezi na kupelekwa SACCOS kwaajili ya wanawake na vijana kukopa. Hizi ni hatua zilizofikiwa;

- Halmashauri inatenga 10% ya mapato yake ya kila mwezi na kupeleka SACCOS kwaajili ya mikopo ya wanawake na vijana

- Uhamasishaji wa wanawake na vijana kujiunga katika vikundi unaendelea katika ngazi ya kata

- Elimu ya ujasiriamali inatolewa

- SACCOS mbili zitakazotoa mikopo kwa wanawake na kwa vijana zimekwisha ainishwa

- Maombi ya mkopo yanaendelea kuwasilishwa katika SACCOS husika


6.Bima ya Afya

Zoezi hili halijaanza ila tunategemea ifikapo April 2017, ziwe zimetolewa bima si chini ya 5000 na makampuni mbali mbali


HITIMISHO

Hiyo ndiyo taarifa fupi ya maendeleo ya mradi na hatua zilizofikiwa katika vipaumbele vyetu vyote kwa mwezi August mpk October.
 
WEBSITE YA BUKOBA MUNICIPAL COUNCIL


52dc82350217fd69439474008f23c29f.jpg
0b96c333e40966a194926bab76b1bcfe.jpg
e59914886dab64df70298887425d51b6.jpg
04a5dce35abe52602f5b04d3e80db373.jpg
a541282633fad2d28ddfa6daeee92279.jpg
30c8dc20eeca3b8c1d7884c1c9004ea7.jpg


Website updated 2012, taarifa zote zilizopo na matangazo yaliyoandikwa 'NEW' ni ya 2012. Taarifa ya idadi ya watu ni ya sensa ya 2002 . Website haijui hata kama uwanja wa ndege ulishapanuliwa na kwasasa una lami, manispaa haijui hata kama kuna ndege zinatokea dar na kuja moja kwa moja Bukoba.

Yeyote anayetamani kuwekeza Bukoba akifungua website yetu haangalii hata mara mbili anakua keshaghairi. Sijui tunatangaza vipi fursa zilizopo, sijui tunatoa taarifa kwa wananchi wetu kwa njia gani
Idara ya IT







TUONE WENZETU WA IRINGA, MOROGORO NA KINONDONI WANAFANYAJE

46f116d0f33ec65574cb4c8fa7754a66.jpg
0e493ac0023787a01b10d2773fdcce86.jpg
21d655d03feb649e21d5e785b5a87f9b.jpg





NA TUONE BASI ENTEBBE WAMEFANYAJE

972c59a7d6931df69afadd0526dfb269.jpg
df1f656e1dfa05e6984d34de8888158f.jpg
90ffc27114bd5cfe63d5e29006ce9009.jpg
3a34a930dc34fb9f03cd0a0f180f6268.jpg
b4494f175c211d2f5b473a2c8ae69e05.jpg
01185982fe96f0f8b1616b563ada5290.jpg
dc80da7bedd16db119b726687b143266.jpg
73114f40cd1c06af427e66fa1f67aa78.jpg
98475c5696e89f318762e8746e8c862a.jpg
3f5b001c5f3208f3e39e530e9a235a7e.jpg
4f1103818450994472364559e43d49a7.jpg


Kuna vitu huonekana kuwa vidogo sana lakini vina maana kubwa kiuchumi, tusivipuuze. Tutengeneze website yetu ya Bukoba Manispaa kibiashara ili kuvutia uwekezaji na kutoa taarifa kirahisi kwa wananchi. Wananchi wanaotumia mtandao ni wengi sana

Bukoba Kazi, Amani na Maendeleo
 
Asante kw NEWS hiz hakika ini nzuri sanaaaaaaaaaa, zimenivuta na kunisahangaza sana skujua kama mkoa wangu ni mzuri hivi jamani, ila all in all, your right Public relation wa jf nimependa, asante kwa kupenda jina langu ila tumsifu sana na kumpongeza sana mzee, Leo aliyeniita sifi.
 
4231e422a93c363ed5519c5c6701b3af.jpg
9645c35a20a501738b9e601ba93c6658.jpg
f77d2578695004e95b4fe83660612108.jpg
fa216a10eca8dee1d6237053ffcb1ead.jpg


Huu pia ni mradi unaoendelea pia manispaa. Ni ujenzi wa jengo la kitega uchumi litakalojengwa ilipo stand ya sasa. Jengo litakua na ghorofa tisa (9) kwenda juu, pia litakua na basement na ground floor. Mradi huu hauko katika vipaumbele vya Tushirikishane.

Hatua zilizofikiwa katika mradi huu ni zifuatazo;

- Michoro, usanifu na upembuzi ya kinifu umekamilika

- Andiko la mradi limekamilika

- Ukokotoaji gharama za mradi umekamilika

- Shirika la NSSF liko tayar kwa mazungumzo ya ubia muda wa ujenzi utakapofika


Tunasubiria Inshaallah
 
MAAGIZO KWA MH. LWAKATARE


Anaandika Ramadhan Kingi

Likumbushe Bunge kuhusu mchango wa Kagera katika kutafuta Uhuru wa Tanganyika. Wakumbushe kabisa jinsi wanavyoupuuza mkoa wa Kagera! Wakumbushe hata JPM alikozaliwa na kusomea. Lwakatare don't flinch an inch from the whole truth. Let us know kwamba Kagera must have its rightful place katika Political life! Nyerere asingelikwenda UNO kama si Kagera! Wamtafute mtoto wa Al Marhum Kandoro awape kitabu cha baba yake na humo wamtafute Mar. ALI Migeyo na mchango ws Kagera katika Mkutano wa TANU 1958. Waonyeshe kwamba tumekasirika sana. Watu wa kwanza kuwekwa jela kwa sababu ya kudai UHURU ws nchi hii waambie! Wala si Nyerere bali mar.
Ally Migeyo alifungwa! Mar. Mzee Jaafary Rwabyo alifungwa
Mar. Ayoub Rubai alifungwa. Hawakufungwa kwa wizi ama Lugumi bali katika kuutafuta Uhuru wa Nchi hii. Waulize wakutajie na wengine waliofungwa kwa kujinasibisha na TANU!
Naiweka humo na CHATU. Kwanza na hiyo Chatu inapaswa kuilipa fidia KAG3RA kwa kulelewa kwa miaka yote. Leo Chatu ni mtoto wa kambo!!! Kamsahau babu yake!!!
TELL THEM LWAKATARE tell them usiogope! You will have nothing to be ashamed of!! OTAKUPOKYA!
WAAMBIE KAGERA HAISTAHILI KUPUUZWA HASA WAKATI HUU WA TETEMEKO. Mwisho wakumbushwe kwamba hata JWTZ isingelishinda vita baina yetu na Uganda kama si umoja na uzalendo wa watu wa KAGERA. Kagera hatupendi siasa za kimzahamzaha!!!!

Mzee wa kwanza Mtanzania kumtandika kofi Mwingereza (district officer) tena ofisini mwake hapa Bukoba baada ya ukereketwa wa uhuru wa Tanganyika ni mar. Abdallah Kaluandira kwake hapo Busimbe Bukoba! Wapo wengine nitawataja ambao hawakukubaliana kabisa na matakwa ya Wakoloni. Mnaweza mkajiuliza hata wengine kwa nini ni Kamachumu tu kilijengwa kituo cha Polisi!!! Msubiri tufe halafu mje mjifarague vizuri! Lwakatare waambie!

Anaongezea LUCAS MNUBI

Ramadhani Kingi, niulize, hivi hadi leo mwezi wa pili hiyo misaada ya maafa ya tetemeko imepelekwa wap? Sio Kagera! Aah huh....Lakini, pia, ninaona una manung'uniko ya kihistoria kwa kutaja majina ya mashujaa wa kudai, Uhuru kutoka "Akagera" ambao unalalamika kusahauliwa, kulikoni, muungwana? Je, hicho kituo cha polisi cha mkoloni bado kinatumika kwa watuhumiwa wa kosa yapi? Mzee Ally Migeyo, John Rupiya na kikundi cha wahindi kutoka Singida na Dar majina yao yametwa miongoni watu waliochanga hela za tiketi ya kumpeleka mtu mmoja UNO, Tanu, wakamteua Nyerere kwa kauli "moja" kuzungumzia Uhuru. Ambapo kikundi cha wakulima Meru(Tanganyika) na Meru(Kenya) wakachangishana vihela vya tiketi ya ndege ili Japhet Krilo, Mmeru kutoka T'nyika kwenda UNO kudai ardhi ya Wameru iliyokuwa imekaliwa na masetla! Historia ipo, ila nadhani kwa sababu za makusudi, hila, roho mbaya, chuki binafsi, na elimu kama miundombuni, kuwa mikononi wa chache, bila shaka mengi zaidi au hata machache mazuri hayajawekwa wazi....juu ya nani alitamka kauli ya kwanza kudai Uhuru!
Mengine kama nini mchango wa Mkoa wa Kagera dhidi ya mikoa mingine katika kufanikisha ushindi katika kampeni ya kijeshi wakati wa vita ya 1978/79, ambayo inafahamika rasmi kama Vita ya Kagera (Kagera War) sijui ila kinachojulikana duniani, ni kwamba Kagera iliathirika zaidi (collateral damage) kwa sababu vita ilipiganiwa kwenye ardhi yake! Rudisha moyo nyuma rafiki yangu.

APOLLO LWEIKIZA anaunga mkono hoja


Mzee Joel Rweikiza Alita nyumba yake akamkabizi Mwl. Baba wa Taifa. Hapo Hamgembe akawapa TANU bure. Akumbukwi!!!!! Lol


TUNAOKOTEZA HISTORIA YA KAGERA KUTOKA KWAA WAZEE WETU
 
TATIZO LA UPATIKANAJI WA MAJI NA WIZI KATIKA ANKARA ZA MAJI

Ramadhan Kingi

Nianze upya tena safari ya kuwakumbusha BUWASA kwamba kuanzishwa kwao ni kwa sababu Serikali ilitaka kuanzisha mahusiano ya haraka kwa wale wanaohudumiwa.
Serikali ikiuona umuhimu huo kwa kuanzisha mashirika kama EWURA, SUMATRA, TRL na mengine ili kurahisisha huduma kwa wananchi.
Kinyume chake mashirika mengine yamekuwa hayafanyi kazi ya huduma kama lengo la Serikali! Tunafahamu kabla ya kuanzishwa Serikali kupitia Wizara ilikuwa ikitoa huduma kama hizo!

Ajabu ni kwamba mashirika hayo yamekuwa yakisubiri Wananchi watoe mashtaka dhidi yao mbele ya viongozi! Mfano mkubwa kwa Kagera ni hili shirika la BUWASA. Hawa BUWASA ni wepesi kuleta ankara za maji zikiwa na bei ya ajabu ajabu kila mwisho wa mwezi lakini bika kuhakiki kama wametoa huduma. Kabla ya kuleta mradi wa Wahindi hapa Bukoba watu tulipata maji kwa bei ya uhakika na bila kuikosa huduma.

Leo ni ajabu baada ya mradi mpya wa Wahindi tumekuwa hatupati huduma kama mwanzo! Niseme tu mafundi hawa wamesaidia kuharibu mfumo mzima wa maji hapa mjini!
BUWASA kwa mazoea tu hawatoi taarifa kwa nini hatupati maji hata baada ya kuleta marekebisho yao mapya! Walichojaliwa sana ni kushirikiana na EWURA kupandisha gharama za maji katika mfumo waliouharibu.
Tunamwomba Mhes. RAS afuatilie kwa nini wamepandisha gharana za maji ilhali wakijua kwamba maji yenyewe hayapo!

Tangu wamechimbachimba na kuweka hizo paipu za maji sasa hatupati maji kama iluvyokuwa mwanzo!
Imekuwa ni baraka kwao ikifika mwisho wa mwezi kuleta ankara za kupikwapikwa na tishio la kukatia watu maji!
Kama wao hutishia kuyajata maji sisi tunaoyahitaji maji hayo na hatuyapati tuchukue hatua ipi? Kabla ya mfumo maji nyumbani kwangu tangu mwaka 1992 maji hayajakatika!
Leo kwa mfumo mpya tena eti wa kisasa wa digitali maji hayapatikani kabisa. Wakileta ankara zao unabaki ukijiuliza hivi nyumba yenye watu wawili na mtoto kuweza kutumia units saba kwa mwezi. Nasikia kila uniti ni sawa na ujazo wa mapipa kumi. Nyumba hiyo itatumia ujazo wa mapipa sabini. Utafikiri kaya hiyo wana mradi wa kuosha magari!

Swali je tusipopata maji twende wapi ikumbukwe kwamba tuna mkataba! Kwa hali hiyo tusipende kufikishana Mahakamani. au?

BUWASA iko chini ya himaya ya Katibu Tawala wa Mkoa Tusubiri tu waje Viongozi wa Kitaifa tutoe malalamiko yetu.
Tangu mwezi wa nane tumekuwa tukipata Huduma hii kwa kuomba. Lakini ajabu ukipata Ankara zao utafikiri umewekeshwa fedha! Unit nane ama tisa kama maji yalikuwepo muda wote
Tunaomba mawakili watusaidie tuwafikishe mahakamani kwa Huduma hafifu

Edith Ntagalinda

Umenena mzee Wangu Ramadhani Kingi mi mwenyewe kwangu watu wawili tu lkn mahesabu ya units zilizotumika toka wameingia hawa wahindi sijawahi kuzitumia toka nimeanza kutumia huduma ya Buwasa,alafu gharama Za unit zinachange kila mwezi!je tuelewe lipi? Basi tujuzwe wapi tupeleke malalamiko yetu?maana kesi ya mbuzi kumpelekea fisi nayo matatizo

Jovin John

Kwakweki mi nimechoshwa NA BUWASA mwezi Jana nililipa sh.26500 elf mwezi huu nimelipa sh.32450 je Unafuu upon wapi? Kiukweli maji hatuyapati kabisa bac kamandivyo ata bills tusipewe make mi sioni ninachokilipia mbona tunateseka utadhani hatukuzaliwa?acheniizo.

Ananis Rushojo

Wanafanya kazi kwa mazoea bili sijui wanatuletea za hewani maji hakuna bili kubwa haya ni majipu ya kansa
 
Back
Top Bottom