TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Pia wametoa waziri Mkuu, haipiti miezi miwili bila kufanya ziara ya zaidi ya sikuu saba, na mpaka sasa yuko Lindi kwa siku zisizopungua nne. Korosho zimepanda bei, bodi ya korosho imevunjwa na kuunda nyingine. Nadhani unaona faida walau mkoa/wilaya kutoa kiongozi mkuu wa nchi.
Sisi viongizi wetu waliofanikiwa kushika nafasi nzuri kama hizo si tunawatukana na kuwapiga mawe
Tunashinda kwenye mitandao kuwakatisha tamaa
 
MWONEKANO WA SOKO KUU LEO TAR 20-10-2016

9494d7fd18d12767577abb0b5419f504.jpg
244a99627c3316f4a992c3df77b3c671.jpg
9757aa29d9629ac6ff1a5dc0d1e61235.jpg
66844d903dcbeb535c56137bebc2ac0a.jpg
abc268fed4cc8d1547bf12a0d2f0df5c.jpg
593240c13e51120cd673b7657d693904.jpg
 
Ndio maana nikasema nasikitishwa na Ukimya wa viongozi wetu katika miradi hii. kimya chao kinatujengea hisia kuwa haidha haipo au hawaoni umuhimu wa kutushirikisha. Wanatakiwa kufahamu kuwa hapa hatulalamiki kiitikadi bali tuko hapa kuhakikisha gurudumu linasonga mwisho wa siku wote tuushangilie ushindi. Kupaza sauti kwetu kutasaidia kuwaamsha na kukumbuka wajibu wao, ila endapo wataona kukaa kimya ndo suluhisho basi watambue 2020 sio mbali tutawahoji ahadi zao wamezitendea haki au ilikuwa ni "nipe kura nipate kula"

Kusema kweli hawa jamaa siwaelewi mie. Ukiachia wao ambao manispaa iko mikononi mwao bado walituhakikishia kupitia bumudeco kwamba hii mipango itakuwa ya kwanza kabisa, sasa unashindwa kujiuliza, kama wao ndo wapitisha maamuzi, kama vikao wanakaa, kama maeneo yalishapatikana, kama michoro na ramani vyote vilishakuwepo hivi leo ni kitu gani sasa hawa wenzetu wamekwama tena, wamekwama wapi?

Na sasa mbona hawaji kutwambia? Mikutano ya jimbo hapo kwa mayunga mbona haifanywi ili wananchi wakaambiwa a, b, c? Tatizo nini. Na hapa bado hujaweka yale yoote yaliyoazimiwa na bumudeco, hivi hawa jamaa wakiulizwa yaliyoachwa mikononi mwao kama msnispaa kuna hata 40% ya kilichoamliwa kweli?

These guys have to wake up and stand with vigour, they need to work hard enough kwa kweli. They also need to pass some reliable information over issues.
 
Nashukuru kwa ufuatiliaji wa kila mmoja wetu na hamu ya kujua kinachoendelea. Mchakato wa kufanya formalities zote zinazotakiwa kisheria na kiutaratibu zinaendelea. Na kwa bahati mbaya taratibu za serikali yetu ni ndefu mno na zenye kujaa vikorikoro vingi. Tuko makini tutavuka na tutapeana taarifa ipasavyo

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
MAELEZO RAHISI YA JINSI MRADI WA TUSHIRIKISHANE UNAVYOTEKELEZWA

1eb5fbb67a6a9e27f0b938837ca05c04.jpg


1. vipaumbele vyetu vinne ni baadhi ya ahadi za mbunge. Utekelezaji wake unaanzia BMC na taarifa za mradi zinaanzia BMC. Mbunge ni daraja la kuleta habari zilizo rasmi kuhusiana na maendeleo ya utekelezaji wa mradi kutoka BMC.

2. Mbunge anasimamia utekelezaji na ndiye anatoa taarifa rasmi kwa umma kupitia jukwaa maalum la Jf

3. Jf inahimiza na kufatilia taarifa na vipaumbele ilivyokubaliana na wananchi na mbunge kutekeleza ktk kipind cha mradi.

4. BMC na Mbunge wanawajibika kwa wananchi moja kwa moja

5. JF ni daraja la kupasha habari na kufikisha taarifa za maendeleo ya utekelezaji wa mradi kwa jamii kama zinavyowasilishwa na mamlaka husika

8b8c0feed918b115b7a3bee293dde0b2.jpg


Hivyo basi, mimi kama Afisa Habari wa Jf ninawajibika kutoa taarifa ya kila hatua ya mradi (za vipaumbele vyetu vinne) kama ninavyozipokea kutoka kwa mamalaka husika. Kuchelewa au kutokutoa taarifa ya mradi kuna uhusiano wa moja kwa moja na mamlaka inayohusika kunipa taarifa hizo.

Maelekezo, maswali na hoja juu ya utekelezaji wa vipaumbele vyetu vinne vinakwenda moja kwa moja kwa ofisi ya Mbunge (mbunge na katibu wake) ambayo inapaswa kujibu hapa.

Hata hivyo, kupitia jukwaa hili tunapata fursa ya kujadili, kushauriana, kuhoji na kusaidia kufanya maendeleo ya jimbo letu bila kusahau vipaumbele vyetu

Vipaumbele vyetu vinne vya mradi wa [HASHTAG]#Tushirikishane[/HASHTAG] ni;

1. Ujenzi wa Soko Kuu, Soko la Kashai na Stand Kuu ya Mabasi

2. Urasimishaji Makazi

3. Mikopo kwa Vijana na kina Mama

4. Bima ya Afya

*BMC - Bukoba Municipal Council
*JF - Jamiiforums

Bwana atuwezeshe
 
Nashukuru kwa ufuatiliaji wa kila mmoja wetu na hamu ya kujua kinachoendelea. Mchakato wa kufanya formalities zote zinazotakiwa kisheria na kiutaratibu zinaendelea. Na kwa bahati mbaya taratibu za serikali yetu ni ndefu mno na zenye kujaa vikorikoro vingi. Tuko makini tutavuka na tutapeana taarifa ipasavyo

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app

Mh. mbunge, pole na majukumu yako kwa ujumla. Nianze kwa kukushukuru walau kuja jukwaani kwa mara nyingine tena, na mara hii kusema kweli tuna mambo mchanganyiko lakini kuu kupita yote ni miradi mikubwa miwili, stand na soko kuu.

Kwa kuanza, tunakupongeza kwa kumpata huyu dada yetu Happy katika tushirikishane yetu, hakika huyu dada atakusaidia sana kufikia malengo yako kwa haraka endapo utampa ushirikiano ili naye akusaidie kupitia vipawa vyake alivyojaaliwa na muumba. Tumefurahi kuona ujenzi wa barabara ya mafumbo ukiwa unamuonekano mzuri kabisa, tumefurahi pia kuona ujenzi wa barabara ya n/housing ukiwa umeshika kasi na inshallah nao utakamilika vyema kabisa, kwa haya tunakupongeza sana na chini yako na mayor wako tunaamini manispaa inaweza kufanya mengine mengi zaidi na zaidi.

Kusema kweli ni furaha yetu sote, na kama tu unaweza walau kwenda kwa mwendo huu basi naamini wananchi watakuwa radhi tena na tena uendelee kuwepo, hatuna nongwa kwani kiu yetu kubwa ni kumpata mtu wa kuipendezesha upya Bukoba yetu ( kaitu kaila).

Jambo la pili ni jambo kuu, miradi. Tunakuomba kwa maombi yote ya kiasiri na kimungu utwambie, leo hii ofisi yako iko hatua gani. Ni vyema umesema ni "formalities" na mambo ya kiserikali yana mlolongo, sasa tueleza (nichwe bamoi). Leo mko hatua ipi haswa, najua mpaka miradi hii isimame kunaweza kuwa na hatua hata 10, sasa nyinyi leo mko hatua ya ngapi na inaendelea ama inaonesha kukwama? Huko serikalini ni nini tatizo?

Nasema hivi kwani naelewa, rais mwenyewe alishasema atakayetaka kumkwamisha kuhusu mipango ya maendeleo atambomoa, sasa hizo kona ni nani anaziweka tena kufifisha maendeleo ya wananchi? Huku mtaani pia, inasikika huu mradi umezuiwa kimakusudi na serikali kisa hapo ni kwa wapinzani, wewe hili umeliona, unalijua na linakuingia?

Mara ya mwisho taharifa iliyokuja hapa ilisema tayari UTT wameshakubali kutoa pesa, na kiasi kingine kutoka BMC. Na kwamba ilibaki ofisi ya BMC kushauliana na UTT kujenga soko la mda katika eneo lililo tayari, sasa haya yote baada ya kuwa yamefikiwa miezi 2 iliyopita leo tena mmefikia wapi? Mnafikiri hapo mlipo mtatokaje wakati mwingine pasipo kuhusisha wananchi ili kuchanga upya mawazo?

Hii miradi ni kipimo kwako mh. kwani kama manispaa iko chini yako na ramani na maeneo vyote vilishakuwepo ni wewe sasa kutuita wananchi kila mara ili tusaidiane, tushirikishane ili kuondoa baadhi ya mikwamo, sote tunahangaika kwa ajiri ya Bukoba mpya (a banana city).
 
Umekaribishwa mkuu ...good/bad, who invites you?

Mkuu watu wengine ni ma sadists by default - wewe unafikiri kwa nini Watanzania tuko nyuma kimaendeleo, akili mbovu kama za huyo jamaa zinachangia sana - sasa mtu kama huyo mpe Ukurugenzi wa kusimamia manispaa ya mji wa Bukoba au Mkoa unafikiri kutatokea nini? Ndiyo hiyo unakuta barabara zote mjini Bukoba lami ilikwanguliwa ikabaki vumbi - lakini kila mwaka Serikali inatoa fedha za maendeleo ya Mkoa lakini hakuna kinacho endelea lengo ni kutaka kukomoa Wenyeji wa Kagera- dhana hii imejengeka sana kwa baadhi ya Watanzania, wana chuki binafsi na Mkoa huo - jaribu kufatili majibu jibu yao yamejaa chuki tu - hata Natural disaster kama tetemeko la aridhi bado kuna baadhi ya Watanzania wana ubavu wa kubeza beza tu wanaishia kuwapatia wana vijiji andazi, biskuti na maji ya kunywa kama msaada - uwanadamu hawana kabisa - mwezi umekatika bado tunaendeleza ngojera tunashindwa NGO kama WorldVision ambayo imeonyesha mfano wa kuigwa, maafa ya Kagera yasichukuliwe kisiasa, yeyote anaye jisikia kutoa msaada atoe tu bila ya kutumbukiza itikadi za kisiasa kwa kujali zaidi kupigiwa kura kuliko kujali uwanadamu!!

Tetemeko la aridhi ni shule tosha kwa wana Kagera tunavyo chukuliwa na baadhi ya Watanzania wenzetu na baadhi ya wale walio pewa dhamana kuendeleza Taifa letu - mambo yanavyo kwenda ni wazi Mkoa huo utaendelea kubaki nyuma kadri miaka inavyo kwenda, tuwe wakweli hapa hakuna political will ya Serikali kuendeleza Mkoa wa Kagera kiviwanda vidogo na vya kati - hakuna kabisa!

Wala awajifunzi chochote kutoka Uchina ambayo inaendeleza kiviwanda na warehousing miji iliyopo mipakani ili nchi jirani zipate mahitaji yao ya muhimu mipakani kuliko kufunga safari kuja Dar au kwenda Dubia, sisi mawazo hayo hatuna kabisa tunakazania kujaza viwanda Mkuranga, Kibaha, Bagamoyo na Morogoro - policy kuhusu sehemu hipi ya kujenga kiwanda na kwa sababu zipi wazo hilo hatuna tunafanya vitu in ad hoc bila ya kufikiria implications zake in a long run, na kibaya zaidi baadhi ya viongozi wetu awashauriki, ukimpa ushauri/maoni yenye mshiko anakuwa na wasi wasi kwamba labda unamuona hafai wakati hiyo si kweli!! Wako defensive kweli kweli wanaji feel uneasy unapo gusia mambo yenye mshiko/yenye nia ya kujenga - sitanii biological/physiological defensive mechanism zao nimezi shuhudia kwa macho yangu.

Wana Mkoa wa Kagera hatuna jinsi, lilo baki ni kujitafutia mikakati ya kijiletea maedeleo kiviwanda vidogo na vya kati, commercial farming na ufugaji n'gome, samaki na Nyuki - tu run joint ventures na (wawekezaji) i.e wafanya biashara/ma Industrialists kutoka Nje ya Africa vile vile Uganda, Rwanda, Burundi na Congo, bila ya kufanya hivyo Mkoa wa Kagera masuala ya viwanda tutakuwa tunayasikia kwenye Radio na TV.
 
Soko kuu Bukoba limechoka sana, nafikiri ni wakati sasa tushirikiane pamoja kufanikisha mradi wa soko kuu! Linahitajika zaidi kuliko miradi mingine na linaweza kurudisha pesa zilizowekezwa mapema zaidi
 
Hahaaaa.......nacheka

Ila Lindi tusiwachukulie poa, wana korosho.....na umeona jitihada za serikali katika zao hilo, wana zao la nazi (hili si zao la mchezo mchezo), wana matunda kama embe. Na wana sekta nyingne likely to develop km uvuvi. Pia ni karibu na Daslama.......

Lakini pia wana sehemu kubwa za kitalii kama Husuni Kubwa, Songo Mnara, Kilwa Kivinje na Kilwa Kipatimo ambako vita ya Maji Maji ilianzia. Na Wizari ya Maliasili na Utalii inawekeza Kilwa kama kipaumbele chake (Southern Circuit)

Sisi Kagera tunahitaji jitihada kubwa sana kupata pa kusimamia kiuchumi

Ila bwana Lindi wanapenda sana ngoma na kuolewa aseeee
Miaka 14 ana watoto mpk 3 wamebarikiwa sana mwanaume anaoa wake mpk 6 halafu hatunzi hata mmoja kila mbuzi anakula kwa kamba yake ichwe ebyo titubibasa owaishe!
 
Jarida letu la Kagera mwezi huu kutoka frajo media tunaomba tuwekewe hapa jamvini
 
BAJETI YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA KWA MWAKA 2016/2017

3d4168a78dcc9b425c86481474da154a.jpg
b727dd74cb5b12d5c698f4ed647c7ca7.jpg
ee2129885af11efa68a5a03aa5a96f63.jpg
541a02c447fc198d5af131d0095d9c5f.jpg
6aee6a3c47370dcb59b4c42ea09b80ce.jpg
03001184c33964453254606f01b09de3.jpg
934b6b696d6e07c0ba796205e71c6446.jpg


Wataaamu, mnakaribishwa kujadili bajeti yetu na kushauri kwaajili ya maboresho kwa mwaka unaofuata

Karibu!
 
CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA TAARIFA NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO KAMA INAVYOONEKANA KATIKA VIDEO ZIFUATAZO;








Video hizo hapo juu zimeangazia hali ya taarifa kwa kundi la wafanyabiashara wa sokoni, mama lishe, na bodaboda. Makundi haya yameonyesha ni kiasi gani ushiriki wa wananchi katika miradi ya maendeleo hauridhishi, lakini pia kumeonekana kuwa na umbu kubwa wa utoaji na upatikanaji wa taarifa kati ya manispaa na wananchi.

Katika warsha ya Tushirikishane moja ya ushauri uliotolea kwa manispaa (mbunge, meya, naibu meya na madiwani waliokuwepo kwenye warsha hiyo) ni kutafta namna ya kufikisha taarifa na ushirikishaji wa wananchi katika mipango na miradi yote ya maendeleo.

Tushirikishane ilipendekeza;

- Ukusanywaji wa namba za simu za wakazi wa manispaa kutoka kwenye mitandao ya simu na kuanzisha namba maalum ambayo itakua ikitumiwa kufikisha jumbe jumbe fupi kupitia simu za mkononi za wananchi

- Kufanya mikutano ya mara kwa mara kuelezea mipango na hatua zinazofikiwa katika utekelezaji wa miradi

- Kufahamisha wananchi ofisi muhimu zilipo na kazi zake mfano ofisi ya mbunge, maendeleo ya jamii, msaada wa kisheria n.k

- Kutafta namna rahisi kwa wananchi kufikisha hoja na malalamiko yao na kuhakikisha yanafanyiwa kazi

- Kutumia mitandao ya kijamii katika kutoa taarifa

- Kuboresha njia za awali zilizokua zikitumika kufikisha taarifa. Mfano kama inavyotumia njia ya gari kukumbusha wananchi kulipa kodi vivyo hivyo njia hiyo itumike kutoa taarifa nyingine muhimu kwa wananchi

Hivyo basi, kwakua tatizo la utoaji na upatikanaji wa taarifa bado ni kubwa, ninawakumbusha wahusika kuzingatia ushauri hapo juu kama tulivyokua tumekubaliana awali.

Bukoba Kazi, Amani na Maendeleo!!
 
KYAKAILABWA

4523bc105a7d622ce2190a0d916c3c27.jpg
5b09e06b00aa2560bdaeed02202e2d61.jpg
c19e2bfe1b1a81a4be3685c997b2ca80.jpg
6b15d1e79a4efc166a7e880917a5ae65.jpg


Hili ndilo eneo ambako stand mpya ya mabasi itajengwa. Tayari uwekezaji mbalimbali umeanza maeneo jirani. Jengo la ghorofa 3 linaloonekana pembeni kulia ni kiwanda cha kutengeneza maandazi. Mliowahi maeneo Kyakailabwa tafadhali mje muwekeze kusaidia kupanua mji wetu
 
NYANGA

6b75ed6d01df108d301df1b8b87aa16c.jpg
7d4f1840b8f91f4cad01a9dede6b6310.jpg
05fca41d83bb0fb1fc66dc83ae052386.jpg
aaa83144cdd337c9f63a1bb263a6c998.jpg


Usafi wa barabara ya Kyakailabwa - Nyakato ukiendelea kama inavyoonekana katika picha. Barabara hii inapita kata ya Nyanga. Kata ya Nyanga inapatikana manispaa lakini inatabia zote za vijiji. Sehemu kubwa ya kata ya Nyanga haijafikiwa na umeme na maji, barabara zake ni za vumbi na kilimo ndio uti wa mgongo wa watu wa eneo hilo

Katika bajeti ya BMC 2016/2017 naona miradi inayohusu nyanga moja kwa moja ni matengenezo ya kawaida ya barabara ya Buhembe - Nyanga 2.1km na Nyanga - Kanisani 1.8km. Lakini pia katika vipaumbele vya Tushirikishane, Kashai na Bakoba zimezingatiwa na kufikiwa haraka hasa katika Urasimishaji Makazi na Mikopo kwa Vijana na Wanawake. Kashai na Bakoba zina kundi kubwa la watu wa uchumi wa kati ukilinganisha na Nyanga

Tunahitaji kuiangalia Nyanga kwa jicho la tatu (3)
 
Mheshimiwa RAS
Kwa heshima na taadhima kwa niaba ya wananchi wako tunakuomba uutumie muda wako adhimu uwatembelee hawa Mabwana wakubwa wa Bukoba Water and Sanitation(BUWASA), na kuwauliza kwa nini hatupati maji?
TANESCO wasipotoa huduma hututangazia tuwe tayari! BUWASA ni wepesi kutuma bills kubwa kubwa kwetu bila kutoa huduma.
Mheshimiwa nikuambie kitu!
Tangu BUWASA wanifungie maji mwaka 1992 maji hayajawahi kukatika kwangu!
Tangu walipowaleta hawa Wahindi "eti" kuboresha huduma leo ni kilio kila nyumba.
Mheshimiwa nafahamu una majukumu mengi lakini BUWASA wamekuwa na kazi nyingi kukuzidi.
Naomba nirudie tena; Sisi tumekuwa watumishi wa BUWASA badala ya wao.
Kwa ufupi sasa mimi sipati maji na kama yatapatikaa saa kumi na moja alfajiri hadi saa mbili asubuhi. Nisielewe hawa malaika watateremshwa lini ili na wao waishi kama mashetani. Ni wepesi wa kuleta bills kubwa kuliko matumizi lakini bila kutoa wao kutoa huduma.
Wako boi wa BUWASA
Ramadhani Kingi
 
UTEKELEZAJI WA KIPAUMBELE CHA MIKOPO KWA VIJANA NA WANAWAKE

Kata Nyanga

e93103185f43c400247357fbb7164631.jpg
26fe74ffc1a667afcaf8c4684df9f5ef.jpg
169ef1578a6e46d851042daff1292acf.jpg
ab096a6648bc805197eedd6fd9d1004e.jpg


Harakati mojawapo ya kukabiliana na umasikini ni utoaji wa mikopo kwa vijana na wanawake. Hiki ni kipaumbele namba tatu (3) katika mradi wa Tushirikishane. Pesa inayotolewa kama mkopo ni asilimia kumi (10%) ya makusanyo ya ndani ya halmashauri yetu ya Bukoba ya kila mwezi.

Utoaji wa mikopo hiyo unafanyika katika vikundi vilivyosajiliwa rasmi kwa kupitia SACCOS zilizoidhinishwa na manispaa.

Katika kata Nyanga, tayari vikundi 30 vya watu watano (vijana na wanawake) vimekwishaundwa na kusajiliwa. Pia wamepata elimu ya ujasiriamali
 
HISTORIA

Balimi Girls Secondary School

34860824dbfd7376e3a78c6ef09a1363.jpg
aca3c1f45e964004a5eeda9a467b38b0.jpg
ba1ae8924f44ec9dcf81e1b4e7f71e77.jpg
a1fa13d1623608febaac399af8bc8d62.jpg
4cceab6cfe9599516091a0205c8faeda.jpg
9e390789a348c105c840de3b8b8a291c.jpg
008f877121e327dc69a6678d197ce21b.jpg
62bc8d2557b235f33f06151624ba7716.jpg
12f682c3e2183dda5bb18407c7a501c7.jpg
5956cfcc91db972699193fd984d2fb88.jpg
6cf32b024d8ec15bf6a99eaafd20a840.jpg
857ee7534a2cd1661b7e54bc519f7a16.jpg
9507beb016fa45ff68b36eae3e136e16.jpg


Shule hii ilikua ikiendeshwa na chama cha ushirika BCU. Iko eneo la Kyakailabwa
 
Back
Top Bottom