Mganga Mkuu wa wilaya ya Singida awekwa mahabusu baada ya wananchi kuugua kipindupindu

Kipindupindu kimeonekana baada ya mheshimiwa kwenda huko? Huyo mkuu wa mkoa ni mzigo, anawatoa wengine kafara ili yeye abaki ofisini.
 
Mtumishi yupi wa kuwekwa ndani kutokana na kuongezeka kwa vibaka, wakabaji, majambazi n.k kwenye wilaya husika?
 
Yeye anahusikaje na kuenea kwa kipindu pindu mtaani?
Hawa wateule wa rais wanajichanganya sana
Tatzo hapa lilikuwa n kutokutoa taarifa mapema kwan inasemekan kulikuwa na wagonjwa wengi tayar na mmoja alishafariki kwahyo alkuwa anafanya isssue ya kupambana na kipindupindu kichinichini
 
Msimu wa sikukuu za Chistmass na mwaka mpya umekuwa mbaya kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Singida baada ya kuwekwa ndani na kushikiliwa na Jeshi la Police baada ya wananchi wa halmashauri hiyo kuugua ugonjwa wa kipundupindu.

Akitoa taarifa ya hali ya kipundupindu kwa Mh. Mkuu wa Mkoa; Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida alisema Daktari huyo wa wilaya hajawajibika ipasavyo katika kupambana na kipindupindu hivyo ugonjwa huo kuenea kwa kasi, baada ya kauli hiyo ndipo Mkuu wa Mkoa akatoa amri halali ya kumuweka ndani Mganga Mkuu wa Wilaya ili iwe funzo kwa watendaji wabovu.

My take; Kasi hii ikiendelea hivi hata kwa magonjwa kama ya UKIMWI kwa madakatri wa wilaya na mikoa kuwekwa ndani pindi maambukizi ya UKIMWI yanapoongezeka inaweza kusaidia kupunguza kasi ya maambukizi.
Hii michezo ya kuwekana ndani ni ya kipuuzi.
Kupambana na kipindupindu sio jukumu maalum la mganga mkuu.
Kuna mwngi yako nje ya uwezo wake...kama usafi wa mazingira, maji safi na salama, ulinzi wa vyanzo ya maji na mifumo ya kutupa taka, uwepo wa wataalam na vifaa tiba vya kutosha etc..kazi za wakurugenzi, wakuu wa wilaya etc
Na hata kama amezembea majukumu yake kama daktari adhabu stahiki sio kumweka ndani...haya ni matumizi mabaya ya madaraka...
Basi sasa wakuu wa wilaya na mikoa waanze kuwekana ndani wao kwa wao, na mawaziri pia tujue moja.. hii tabia
Inakera na kutia kichefuchefu.
 
Msimu wa sikukuu za Chistmass na mwaka mpya umekuwa mbaya kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Singida baada ya kuwekwa ndani na kushikiliwa na Jeshi la Police baada ya wananchi wa halmashauri hiyo kuugua ugonjwa wa kipundupindu.

Akitoa taarifa ya hali ya kipundupindu kwa Mh. Mkuu wa Mkoa; Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida alisema Daktari huyo wa wilaya hajawajibika ipasavyo katika kupambana na kipindupindu hivyo ugonjwa huo kuenea kwa kasi, baada ya kauli hiyo ndipo Mkuu wa Mkoa akatoa amri halali ya kumuweka ndani Mganga Mkuu wa Wilaya ili iwe funzo kwa watendaji wabovu.

My take; Kasi hii ikiendelea hivi hata kwa magonjwa kama ya UKIMWI kwa madakatri wa wilaya na mikoa kuwekwa ndani pindi maambukizi ya UKIMWI yanapoongezeka inaweza kusaidia kupunguza kasi ya maambukizi.
Kosa juu ya kosa. Rais karuhusu watu wafanye biashara ovyo. Kila sehemu watu wanauza vyakula. Ukiwafukuza/kuwachukulia hatua wanasema unapingana na rais. So confusing! Poleni watendaji, inabidi mjitambue mfanye kazi kwa mujibu wa sheria hata kama ukifukuzwa kazi wewe fanya ila siyo kwa kuogopa matokeo yake unalazwa ndani.
 
Mbona mvua hainyeshi na mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa hajachukuliwa hatua yoyote? Huu ni upendeleo kabisa.
 
Back
Top Bottom