Makonda: Watalii hawaji Arusha kulala wanakuja kula starehe, ni lazima Arusha iwe salama saa 24. Hao wadudu nitaongea nao

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,214
42,086
Kwanza nianze kwa kumshukuru Rais Samia kwa kumpeleka Makonda Arusha!

Baada ya kufika jijini Arusha Mh Paul Makonda ameanza rasmi kazi leo na ameongea na baadhi ya wana chi na madiwani akisisitiza kuwa ni lazima jiji la Arusha liwe namba moja zaidi kwa utalii na watalii wanatakiwa kuwa salama zaidi masaa 24 kwani watalii hawaji Arusha kulala bali wanakuja kutalii na wanatakiwa kula raha masaa 24 uku wakiwa salama kabisa!

Amesema kuwa ni lazima kila mwana Arusha awe salama na hata asiye mwana Arusha ni lazima wote wawe Salama!

Amesema pia kuhusu wahuni wa mtaani wanaojiita wadudu atakaa nao na kuongea nao kwani ni watu wazuri lazima wataelewana na Arusha itakuwa salama salimini!

Anasema Arusha ni lazima liwe jiji la utalii namba moja nchini na linalovutia.

PIA, SOMA:

Uteuzi wa Ukuu wa Mkoa Arusha
Matukio baada ya Uteuzi
 
Kwanza nianze kwa kumshukuru Rais Samia kwa kumpeleka Makonda Arusha!

Baada ya kufika jijini Arusha Mh Paul Makonda ameanza rasmi kazi leo na ameongea na baadhi ya wana chi na madiwani akisisitiza kuwa...
Watalii hawawezi kuja kwa MUUAJI! Marekani imeshasema ni muuaji , sasa ni kuitangazia Dunia kuwa yule Muuaji kapelekwa Arusha, MSIJE. HAWATAKUJA
 
Jiji la Arusha linakwenda kuwa jiji maarufu kama ilivyo kwa jiji la Washington DC au Newyork Marekani au DUBAI au Paris ufaransa. Makonda ni kiongozi mbunifu sana.

Ukisikiliza hotuba yake ya leo unagundua kuwa huyu Mwamba ni akili kubwa, kiongozi mwenye Maono na mwenye kiu ya Maendeleo.
 
Watalii hawawezi kuja kwa MUUAJI! Marekani imeshasema ni muuaji , sasa ni kuitangazia Dunia kuwa yule Muuaji kapelekwa Arusha, MSIJE. HAWATAKUJA
😂😂😂😀😀😀😭😭😭
 
Binafsi nilijua move ya Mhe.Rais kumpeleka Makonda Arusha, ukiachilia mbali sababu za kisiasa, ni kuimarisha usalama jijini Arusha kwa ajili ya watalii, kusimamia vyema ujenzi wa uwanja wa mpira, na pia kuhakikisha kuna usalama wa kutosha jijini Arusha ahead of AFCON ambayo sisi ni wenyeji. Kudos Mhe.Rais SSH!

Niliwahi kujiuliza. Usalama wa wageni watakaokuja kwenye AFCON utakuwaje kwa usela mavi (uhalifu) ulioota mizizi namna ile pale Arusha? Kuna siku nimeona wapuuzi fulani wamebebana kwenye pikipiki halafu mmoja (aliyekaa nyuma) ameshika panga huku akilinoa kwa kuliburuza kwenye lami. Na watu wanaona ni jambo la kawaida tu eti! Shwaini kabisa.

Kwangu, ni viongozi wachache wanaoweza kudeal na situation kama hiyo, na mmoja wao ni Paul Makonda.
 
Back
Top Bottom