Makonda: Watalii hawaji Arusha kulala wanakuja kula starehe, ni lazima Arusha iwe salama saa 24. Hao wadudu nitaongea nao

Lema anabubujikwaa na machozi yasiyokatika na sasa ameanza kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu. Anawatukania w nzao hadi mama zao bila kosa lolote lile
Hivi ukitokea ukapata bahati ya mtende ukawa rais wa nchi hii, utawafanyia nini wapinzani wako? Ninavyohisi waweza kuwa zaidi ya Magufuri.
 
Watalii hawawezi kuja kwa MUUAJI! Marekani imeshasema ni muuaji , sasa ni kuitangazia Dunia kuwa yule Muuaji kapelekwa Arusha, MSIJE. HAWATAKUJA
Marekani ndiyo msemaji wako? Tujitahidi kujenga hoja.....kwahiyo we kama mwanaume utaolewa na mwanaume kisa USA? Au mwanamke ukaolewe na mwanamke kisa tu unapata mwongozo toka kwa marekani? Siyo kila jambo lazima tutumie references za nje na wao ni wapuuzi na wanamadhambi yao kibao
 
Kwanza nianze kwa kumshukuru Rais Samia kwa kumpeleka Makonda Arusha!

Baada ya kufika jijini Arusha Mh Paul Makonda ameanza rasmi kazi leo na ameongea na baadhi ya wana chi na madiwani akisisitiza kuwa ni lazima jiji la Arusha liwe namba moja zaidi kwa utalii na watalii wanatakiwa kuwa salama zaidi masaa 24 kwani watalii hawaji Arusha kulala bali wanakuja kutalii na wanatakiwa kula raha masaa 24 uku wakiwa salama kabisa!

Amesema kuwa ni lazima kila mwana Arusha awe salama na hata asiye mwana Arusha ni lazima wote wawe Salama!

Amesema pia kuhusu wahuni wa mtaani wanaojiita wadudu atakaa nao na kuongea nao na wataelewana na Arusha itakuwa salama salimini!

Anasema Arusha ni lazima liwe jiji la utalii namba moja nchini na linalovutia….
Kama hapo Arusha mjini kuna maduka ya wahindi, wawe makini sana na hicho kijamaa kinachoitwa Paula Makondo, mnakumbuka ile tabia yake ya kutumia vitisho kama fala Sabaya kutaka apewe favours ambazo hazistahili.
 
ni wakunyoshwa..mtu ukipasikia arusha na ukifika ni vitu viwili tofauti maneo ya starehe hakuna usalama kabisa vibaka na msongamano wa watu kama mbuzi zizini
Nilipita kwa mara ya kwanza mwaka jana,nikajiuliza hii ndiyo Geneva kweli? Binafsi sikupaelewa
 
Dar aliweza kuvamaliza hivi?
Ulisikia tena watu wanaporwa na wezi kwenye boda boda? Ulisikia tena watu wanauawa wakitoka kutoa hela benki? Uliwahi kuwasikia panya road katika kipindi chake? Ulikuwa unaona tena mateja wanasinzia vituoni huku wamesimama? Uliina trna watu wakijisifu kwa kuuza madawa? Au mashoga wakijinadi hadharani..?
 
Kwani wadudu Wana shida gani? vijana wameamua kujipa majina hayo na Wala hawana habari za upigaji ngeta,bangi na ulevi.
 
Wanao bugudhi, wanao hatarisha na wanaotatiza usalama wa watalii, wafanya biashara na wanainchi wa Arusha lazima wakabiliwe ipasavyo na kudhibitiwa bara-bara, ili kulinda hadhi na heshima ya Arusha kitaifa na kimataifa 🐒
 
Hivi ni shuruti kutumia maneno haya wakati wa kumsifu na kumpamba mtu?

Akili kubwa
Mwenye maono
 
Watalii hawawezi kuja kwa MUUAJI! Marekani imeshasema ni muuaji , sasa ni kuitangazia Dunia kuwa yule Muuaji kapelekwa Arusha, MSIJE. HAWATAKUJA
Kumbe Marekani anachukia mauwaji kiasi cha hadi kufanya hivyo?
 
hao wadudu ni wakutokomeza mara moja ashuke nao jumlajumla hadi kandokando mwa jiji maeneo ya tengeru
Na atapita nao kweli !
Wale huwa ni chui wa karatasi tu !
Ukiamua wakutishe watakutisha lakini ukiamua kuwachana unawachana kirahisi kabisa !
Hawawezi kushindana na mamlaka ikiamua kuwashughulikia !
Usalama ni priority ya kwanza kila binadamu anaihitaji na ni haki yake !
Hata hao wanaojiita wadudu wakikosa usalama watajisikia vibaya sana !
One good turn deserves the other !
Kama hutaki mabaya nawe usiwafanyie mabaya wengine ! 🙏🙏
 
Ulisikia tena watu wanaporwa na wezi kwenye boda boda? Ulisikia tena watu wanauawa wakitoka kutoa hela benki? Uliwahi kuwasikia panya road katika kipindi chake? Ulikuwa unaona tena mateja wanasinzia vituoni huku wamesimama? Uliina trna watu wakijisifu kwa kuuza madawa? Au mashoga wakijinadi hadharani..?
Panya road aliwaacha (hawa hawakuisha kipindi chake) watu kuporwa kwa pikipiki bado lipo halijaisha 100%. Mashoga aliwaacha mpaka wengine leo wana ji post social medias,
Na atapita nao kweli !
Wale huwa ni chui wa karatasi tu !
Ukiamua wakutishe watakutisha lakini ukiamua kuwachana unawachana kirahisi kabisa !
Hawawezi kushindana na mamlaka ikiamua kuwashughulikia !
Usalama ni priority ya kwanza kila binadamu anaihitaji na ni haki yake !
Hata hao wanaojiita wadudu wakikosa usalama watajisikia vibaya sana !
One good turn deserves the other !
Kama hutaki mabaya nawe usiwafanyie mabaya wengine ! 🙏🙏
Makonda ata wa suprise sana, hivyo mnavyotaka a deal nao, ndivyo sivyo. Atatumia akili moja safi, wala haitajiki nguvu
 
Wanao bugudhi, wanao hatarisha na wanaotatiza usalama wa watalii, wafanya biashara na wanainchi wa Arusha lazima wakabiliwe ipasavyo na kudhibitiwa bara-bara, ili kulinda hadhi na heshima ya Arusha kitaifa na kimataifa 🐒
Hakika
 
Back
Top Bottom