Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 54,323
- 122,955
Wanabodi
Angalizo la Uchawa!
Baada ya kutokea fani mpya ya uchawa, kuna watu wenye akili fupi humu, ukisifu tuu jambo lolote zuri la Rais, unanyooshewa kidole cha uchawa!.
Tofauti ya pongezi za kweli na pongezi za kichawa, ni pongezi za kweli unapongeza kwenye mazuri, na pia unakosoa.
Pongezi za kichawa ni kusifu tuu bila kukosoa!. Mimi kwenye linalostahili sifa nitasifu, na la ukosoaji nina kosoa!
Leo asubuhi nimeangalia TBC live kipindi cha Jambo Tanzania, Waziri wa Muungano Mhandishi Hammad Yusiph Masauni, amehojiwa live akizungumzia kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano, leo asubuhi kutafanyika kongamano kubwa la Muungano litakalo rushwa live mubashara na TBC kuanzia Saa 3 asubuhi.
Jambo moja kubwa na zuri ambalo Waziri Masauni amelisema ni jinsi Rais Samia alivyo fanya funga kazi kero za Muungano!, Kati ya Kero 25 za Muungano, yeye mwenyewe ametatua kero 15!, marais wengine wote watano waliomtangulia, kwa pamoja walitatua kero 7 tuu, sasa kero za huu Muungano wetu adhimu zimebaki kero 3 tuu!.
Kwenye hili la kero Muungano, kiukweli kabisa, Rais Samia anastahili apewe maua yake!, kwasababu hakuanza leo, "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Hivyo nawaomba wana JF, katika umoja wetu, tumpeni Rais Samia Maua Yake !.
Ili kuzidi kuuimarisha huu Muungano wetu adhimu na adimu, maoni yangu ni twende kwenye serikali moja. Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
Tukutane hapo saa 3 kwenye kongamano ambapo miongoni mwa watoa mada ni Dr. Harrison Mwakyembe na Hammad Rashid Mohamed
Moderator ni Anthony Mgeni waTBC, usikose!.
Paskali
Rejea za Mtoa Mada Kuhusu Muungano

- Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
- Pongezi za Miaka 60 ya Muungano: Twende Kwenye Muungano Kamili wa Ukweli wa Nchi Moja, Serikali Moja na Rais Mmoja? Kero Zote za Muungano Zitayeyuka!
- Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"
- Swali: Hivi Muungano Tanzania Upo Kweli?! au ni Dhana Tuu?!. (Ufuatiliaji Muungano Sehemu ya I)
- Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?
- Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano? Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?
- Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?
- Live on TBC1: Kongamano la Vyuo Vikuu kuhusu Muungano
- Muungano: "Hoja ya Nguvu" V/S "Nguvu ya Hoja"!.
- Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio utauvunja Muungano
- Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja
- Je, kunahitajika ‘affirmative action’ ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?
- Bunge Maalum Lapigwa Changa la Macho!? Lapewa"Act of Union" na Kudanganywa ni "Articles of Union"!.
- Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?
- Tanzania Nchi 1 ya JMT, Zanzibar Kujiita Nchi, Sio Uhaini?. Zanzibar Iadabishwe Kuondoa Ubatili wa Katiba Yake ili Tuitambue au Tumchelee Mwana Kulia?