Dodoma: Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yafunguliwa kwa mazoezi ya kukimbia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,884
12,133
Run.png

Run5.png
Wadau wa Tasnia ya Habari wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri wameshiriki kukimbia katika mbio ‘Media Fun Run’ mwendo wa Kilometa 10 kwa lengo la kuweka mwili safi.

Mabio hizo ni ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (World Press Freedom Day) kwa Mwaka 2024 yanayofanyika Mei 1-3 Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre yakiwa na Kauli Mbiu ya “Uandishi wa Habari katika kukabiliana na mgogoro wa mazingira”.

Run1.png

Akizungumza kaba ya kuanza kwa mbio hizo leo, Mei 1, 2024, DC Jabir Shekimweri amesema “Mazoezi ni sehemu ya kuboresha Afya, pia mbio hizi zitumike kuhamasisha maboresho utunzaji wa mazingira.


Run2.png

Run3.png

Run4.png

“Mazoezi kama haya yanasaidia hata kwenye maisha binafsi, kwakuwa siku hizi kuna matangazo mengi ya Waganga na tiba mbalimbali lakini mazoezi kama haya yanaweza kuwa msaada mkubwa ya kukwepa kwenda kwa watu kama hao.

“Pamoja na hivyo, Wanahabari mtumie tasnia yenu kufikisha ujumbe na elimu kwa Wananchi ili mabadiliko ya mazingira yawe bora yapatikane.
Run 7.png

Run 6.png

“Kuna kipindi fulani ukifika Dodoma mwezi Juni hadi Oktoba kulikuwa na vumbi nyepesi ambayo iliathiri macho kiasi cha kuanza kueleza kuwa Dodoma tuna changamoto ya macho, siku hizi hizo mambo hazipo.”

Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya amesema Kauli Mbiu hii itumike vizuri kuweka mazingira safi na mikusanyiko kama hii iwe kichocheo cha kupeana elimu na kufikisha ujumbe kwenye jamii kuhusu mazingira.

Snapinsta.app_440762824_1462352931385933_2407132357893834250_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom