Nenda uhamiaji wako kurasininipe process zote nataka jifatilie walai
vigezo/masharti?Nenda uhamiaji wako kurasini
Utapata maelezo yote na fomu za kujaza mrembo.
Kamata it mpka Zambia mengine utayajua mbele kwa mbele maana ni cheap sana kupanda gar za itKuna njia 2 ya Lusaka na ya Harare
Kutoka Dar mpk harare kwa bus ni 150,000 Harare mpk Joburg Rand 200
Kutoka Dar mpk Tunduma 45,000 kutoka tunduma mpk Lusaka sikumbuki na kutoka Lusaka mpk SA Rand 700.
watashangaa sana hizo gari za mitumba haziko kulekwanini mkuu??
Kaka jitahidi muwe wawili au watatu kusaidiana hiyo safari ni safari nzuri lakini inafikia kipindi utatamani utembee kwa miguu
Maandalizi ya safari utaanza na Service yako ya gari vizuri, kisha utalipeleka gari traffic pale makao makuu kwa wakaguzi wa gari (Vehicle Inspector) ukishapata hiyo Report yao, utaenda nayo INTERPOL (pale Wizara ya Mambo ya Ndani) wao watakupa Clearance report kuwa hiyo gari ni yako na haina tatizo lolote hivyo kokote utakofika walihesabie kuwa hilo gari sio la wizi, HIYO REPORT YA INTERPOL NI MUHIMU SANA SAA NYINGINE UNAWEZA KUPATA USUMBUFU UKIWA HAUNA HIYO
Safari za mbali hazihitaji speed zaidi ya 100km/hr , ukiwa na speed kubwa zaidi ya hiyo utahitaji concentration kubwa na utachoka mapema,
Kwanza Ipange safari yako kwamba siku ya kwanza utalala Tunduma, ili asubuhi uanze na paper work, kwa upande wa Tanzania watataka kuona karatasi zote pamoja na hiyo interpol report, KADI YAKO ORIGINAL YA GARI ITABAKI PALE BORDER UPANDE WA TANZANIA (Custom),
Zambia wanakuwa na kausumbufu kadogo, hakikisha gari lako umelibandika vi reflector vidogo. Mbele vyeupe na Nyuma vyekundu, Zambia utalipia insurance kulingana utakaa siku ngapi hapo (Transit status), kisha utalipia Carbon Tax, na vitu vingine vidogvidogo, ukianza procedure hizo za paper work say saa moja na nusu au saa mbili basi ikifika saa tano utakuwa umemaliza na unaweza kuanza safari yako
Umbali wa kutoka Tunduma/ Nakonde mpaka Lusaka unaweza kukuchukua masaa 18 mpaka 20, kuna sehemu za kujaza mafuta kwenye miji mikubwa ya njiani kama Serenje, KapiliMposhi nk, uwe makini na speed kwa upande wa Zambia hasa kutoka Tunduma/Nakonde mpaka Kapilimposhi njia sio nzuri sana,
Kutoka Lusaka njia nzuri ni ya kupitia Botswana, hivyo utaelekea njia ya Livingstone mpaka Kazungula hapo kuna kivuko cha kuingia Botswana, ukishaingia Botswana utaitafuta Gaborone kwa kupitia miji ya Maun, Serowe, Francistown, Palapye, Mahalapye, Mochudi kisha Gabs,
Kutoka Gaborone mpaka Border ya South africa ni Umbali wa kutoka Mwenge mpaka Posta Mpya, na hiyo Border inakuingiza moja kwa moja Gauteng Provence ambayo ndio ina Jos na Pretoria, kutoka Gabs mpaka Jos ni six hrs
PLZ: Kwa safari ndefu kama hizo usisahau Spare tyres hata mbili, spanner zote muhimu zinazofungua gari yako Fix na combine, wheel spanner ile ya msalaba pamoja na jack, set ya Screw drivers, set ya fuse zinazotumika kwenye gari yako, hydraulic na engine oil, ikiwezekana set ya bulb pia uwe nayo
Kidumu cha maji na dumu la liter 20 la Petrol,
Kwenda na kurudi anahitaji kama 700 litresGari ya cc 2.5 appx utatembea 8-9 km kwa kutumia lita 1 ya Petroli, sasa piga hesabu kutoka Dar mpaka Pretoria ni kilomita ngapi kwa njia utakazo pita? Hapo utapata atleast an idea ya kujua utatumia Petrol lita ngapi kwenda na kurudi.
460k up to 600kKwa pipa Tsh ngapi
SA Magari choka mbaya yapo kibao mbona?watashangaa sana hizo gari za mitumba haziko kule
Gari za mtumba zipo hata wao wenyewe wananunua zilizopata ajali pale pale wanarekebisha kidogo maisha yanaenda...SA hawawezi kushangaa gari walishatoka huko kitambowatashangaa sana hizo gari za mitumba haziko kule
Kwanini asiweke bluetooth kwenye matairi? Huoni itakuwa vyema zaidiWeka upepo wa Nitrogen kwenye matairi ili gari iwe nzito ....
Africa's Cowboy Capitalists (Full Length)
Journey by road from Johannesburg in South Africa through Zambia, Tanzania, Uganda and South Sudan
sehemu gani korofi katika njia hiyo ki miundombinu na kiusalama
(3) mipakani regulations kama unatoka na mzigo wa biashara toka pretoria kwenda dar inakuwaje?
(4) vitu gani vya muhimu ambavyo ni lazima niwe navyo standby
(5) na safari inakadiria kuchukua siku ngapi (max)
(6) mwisho kabisa ni changamoto gani nitarajie kukutana nayo kwenye njia hiyo
(7) lakini pia ni mazuri gani nitarajie kukutana nayo kwenye safari hiyo
Source: VICE
Ila kwenye hii safari ya hawa mabwana Tanzania tumuwazingua sana inabidi tubadilishe mifumo yetu