Dar to Pretoria na gari private: Ushauri na changamoto zake plus gharama

Mkuu zingatia tairi za hiyo gari usitumie ilizokuja na gari pitia Lusaka hapo Nakonde kuna road toll,bima,council hizo. kukata nadhani hazizidi 100 usd unapita Living Stone kazungura kuelekea Botswana kuingia Botswana unalipia usd 50 kwa kuingia na utakaporudi hautalipia tena utaruhusiwa kupita hizo karatasi kupata ni saa moja tuu pita boarder iliyo karibu na Gaborone kuingia haina magari mengi hata utakapotoka. South Africa kuingia haulipii kitu kupata document pale umbali kutoka Tunduma mpaka pretoria ni 2700 km..
Asisahau kubandika reflects sticker kwenye bumper mbele na nyuma. Maana watamsumbua polisi sana.
 
hv hio biashara gani inakufanya uendeshe mbali hvyo? kwenda moshi tu na cc2500 laki tatu hizo.
 
Kaka jitahidi muwe wawili au watatu kusaidiana hiyo safari ni safari nzuri lakini inafikia kipindi utatamani utembee kwa miguu

Maandalizi ya safari utaanza na Service yako ya gari vizuri, kisha utalipeleka gari traffic pale makao makuu kwa wakaguzi wa gari (Vehicle Inspector) ukishapata hiyo Report yao, utaenda nayo INTERPOL (pale Wizara ya Mambo ya Ndani) wao watakupa Clearance report kuwa hiyo gari ni yako na haina tatizo lolote hivyo kokote utakofika walihesabie kuwa hilo gari sio la wizi, HIYO REPORT YA INTERPOL NI MUHIMU SANA SAA NYINGINE UNAWEZA KUPATA USUMBUFU UKIWA HAUNA HIYO

Safari za mbali hazihitaji speed zaidi ya 100km/hr , ukiwa na speed kubwa zaidi ya hiyo utahitaji concentration kubwa na utachoka mapema,
Kwanza Ipange safari yako kwamba siku ya kwanza utalala Tunduma, ili asubuhi uanze na paper work, kwa upande wa Tanzania watataka kuona karatasi zote pamoja na hiyo interpol report, KADI YAKO ORIGINAL YA GARI ITABAKI PALE BORDER UPANDE WA TANZANIA (Custom),

Zambia wanakuwa na kausumbufu kadogo, hakikisha gari lako umelibandika vi reflector vidogo. Mbele vyeupe na Nyuma vyekundu, Zambia utalipia insurance kulingana utakaa siku ngapi hapo (Transit status), kisha utalipia Carbon Tax, na vitu vingine vidogvidogo, ukianza procedure hizo za paper work say saa moja na nusu au saa mbili basi ikifika saa tano utakuwa umemaliza na unaweza kuanza safari yako

Umbali wa kutoka Tunduma/ Nakonde mpaka Lusaka unaweza kukuchukua masaa 18 mpaka 20, kuna sehemu za kujaza mafuta kwenye miji mikubwa ya njiani kama Serenje, KapiliMposhi nk, uwe makini na speed kwa upande wa Zambia hasa kutoka Tunduma/Nakonde mpaka Kapilimposhi njia sio nzuri sana,
Kutoka Lusaka njia nzuri ni ya kupitia Botswana, hivyo utaelekea njia ya Livingstone mpaka Kazungula hapo kuna kivuko cha kuingia Botswana, ukishaingia Botswana utaitafuta Gaborone kwa kupitia miji ya Maun, Serowe, Francistown, Palapye, Mahalapye, Mochudi kisha Gabs,

Kutoka Gaborone mpaka Border ya South africa ni Umbali wa kutoka Mwenge mpaka Posta Mpya, na hiyo Border inakuingiza moja kwa moja Gauteng Provence ambayo ndio ina Jos na Pretoria, kutoka Gabs mpaka Jos ni six hrs

PLZ: Kwa safari ndefu kama hizo usisahau Spare tyres hata mbili, spanner zote muhimu zinazofungua gari yako Fix na combine, wheel spanner ile ya msalaba pamoja na jack, set ya Screw drivers, set ya fuse zinazotumika kwenye gari yako, hydraulic na engine oil, ikiwezekana set ya bulb pia uwe nayo
Kidumu cha maji na dumu la liter 20 la Petrol,
Asante mkuu nimejifunza kitu hapo. Hasa swala la police kwa u jumla
 
Mkuu,
Naona watu Youtube (comments za kila upande wa dunia) wamepongeza askari wa trafiki wa Tanzania kwa kutoangalia sura wala rangi ya mtu, wote wanapungiwa mkono kusimama kila baada yamwendo mfupi.

Pia safari ya kilomita 3,000 ya huyu jamaa mwingine toka mji wa Lubumbashi katika jimbo la Katanga DRC Congo kupitia Zambia, Tanzania mpaka Kenya na kutupatia maelezo yenye mwangaza juu ya bima ya gari kimataifa, vibali, mapumziko njiani,mafuta, hali ya hewa/mvua n.k ili kupita nchi mbalimbali kwa gari ukiwa umejitayarisha kukabiliana na mambo-tajwa muhimu.
C.C mdau C.T.U
Daring abroad : Kenyan businessman drives from Lubumbashi via Zambia, Tanzania to Kenya

Source: KTN News Kenya

mkuu achana traffic tatizo lilikuwepo pale migration na customers ndipo jamaa alikuwa ana lalamika
 
Zingatia usibebe Sembe kutoka hapa Botswana kuna gari nyingi zimekamatwa Francis Town na walibeba na kule kama unatoka na simu za mtaani ni shida katika Tokwen boarder wanakagua sana kuhusu siraha zinazotoka pale kwa hiyo jitahidi safari yako iwe sio ya kuvunja sheria kule
Jf ni kila kitu
Mkuu zingatia tairi za hiyo gari usitumie ilizokuja na gari pitia Lusaka hapo Nakonde kuna road toll,bima,council hizo. kukata nadhani hazizidi 100 usd unapita Living Stone kazungura kuelekea Botswana kuingia Botswana unalipia usd 50 kwa kuingia na utakaporudi hautalipia tena utaruhusiwa kupita hizo karatasi kupata ni saa moja tuu pita boarder iliyo karibu na Gaborone kuingia haina magari mengi hata utakapotoka. South Africa kuingia haulipii kitu kupata document pale umbali kutoka Tunduma mpaka pretoria ni 2700 km..
 
Back
Top Bottom