Dar to Pretoria na gari private: Ushauri na changamoto zake plus gharama

Yaani gharama za kwenda anakata go n return (ndege)
Hapo hujaangalia za kurudi na service ya gari yake akiwa bongo kabla ya safari, akiwa SA kujiandaa kurudi na akishafika bongo

Gari ya cc 2.5 appx utatembea 8-9 km kwa kutumia lita 1 ya Petroli, sasa piga hesabu kutoka Dar mpaka Pretoria ni kilomita ngapi kwa njia utakazo pita? Hapo utapata atleast an idea ya kujua utatumia Petrol lita ngapi kwenda na kurudi.

Mkuu nakushauri hizo gharama zote utakazotumia njiani jumlisha na petroli ni bora ungeziunganisha ukapanda ndege
 
Njia rahisi sana nenda hadi Mtwara pale ofisi ya mkuu wa mkoa kuna ofisi ya ushirikianao Tz na msumbiji pale watakupa visa ya Msumbiji nenda hadi boda ya Kilambo pale utavushwa mto ruvuma na matishari ukiingia Msumbiji ambaa na nayo mpaka boda ya south pale utafanya utaratibu wa kingia bondeni, mengine akili mkichwa
 
Sio kweli gari gani ya kisauzi zilingane mwaka iwe sawa na ya kijapani..gari za japani hizi zinazokuja ni matoleo ya zamani sana wakati Sauzi gari ya 2006 au 7 model unauziwa kama gari ya zamani na bei itapungua ya japan bei ipo juu vile vile...gari za kijapan durban na messina zipo bei ndogo 1000usd mpaka 1500 sasa Sauzi gari ya hiyo bei itakua choka au imegongwa..

Wahindi wa Durban wanauza bei chee kwakuwa gari za kijapani sauzi hazitakikanwi n soko Lao ni la wasumbiji ila gari za kisauzi mpya 0 mileage 20,000,000 ya kitanzania kwa gari za saloon
 
Iyo makala safi sana ya kutoka south mpk Juba, ila nmecheka sana polisi wetu kumbe kwenye kizungu hawanaga story nyingi. Ni just go
 
Bila Shuka Durban ni Free port unaruhusiwa kupeleka kitu chochote kikashukia pale wao wanachotaka ni kodi kidogo kwa kila gari itakayoshuka pale na wanatoa miezi sita gari iwe ishauzwa au kutoka nje ya SA ndio maana gari ikifika muda wa kuongeza umekwisha wanauza hata kwa bei ya japan soko la japan cars ni Botswana,Zambia,Namibia, Zimbabwe na Mozambique bandari haina longo longo wala SARS ukishalipia kitu basi hakuna kufatana tena ndio maana mizigo mingi hata pale ni Transit inashushwa Durban sio gari tuu ni vitu vingi tofauti..
 
Mkuu Isanga family shukrani kuna kitu hapa nataka kujua ntakuwassup...

Pia unaeza ukaenda hadi Botswana kisha ukapita Francis town hadi Thabazimbi ( South Africa) nayo ni njia fupi isiyo na magar! Lkn uwe na tahadhari ya Mafuta hasa toka Nakonde Zambia hadi Kabwe au Kapirimposhi kuna karibu KM 600 hamna fuel station!!!!!! All the best mkuu!!!!!
 
Pia unaeza ukaenda hadi Botswana kisha ukapita Francis town hadi Thabazimbi ( South Africa) nayo ni njia fupi isiyo na magar! Lkn uwe na tahadhari ya Mafuta hasa toka Nakonde Zambia hadi Kabwe au Kapirimposhi kuna karibu KM 600 hamna fuel station!!!!!! All the best mkuu!!!!!
Mpika viko vituo, mkushi viko vituo, serenje viko vituo, huko koteni nyuma ya kapirimposhi.
 
NASHAURI TU KAMA NI MZIGO UNAFANANA RANGI NA SEMBE USITHUBUTU, TUNAKUPENDA SANA!!!! HILO TU NDO LANGU.

wakongwe salaam nina mpango wa kuwasha ndinga kutoka Dar mpaka Pretoria South Africa hivi karibuni

dhumuni hasa kuna mizigo miwili mitatu nataka nikafanye shopping kwa ajili ya biashara (mobile phones)


mizigo hiyo nina mpango wa kusafiri nayo kwenye gari kwa maana niweke kwenye buti

lengo la kwenda na gari ni kwanza kufanya utalii wa Africa lakini pia kuendesha kwa mwendo mrefu maana passion yangu kubwa ni kuendesha mwendo mrefu

gari ninayotaka kuitumia ni Toyota Mark X yenye cc 2500

sasa wakongwe naomba ushauri katika nyanja zifuatazo

(1) mafuta niandae kiasi gani kwenda na kurudi (max)

(2) sehemu gani korofi katika njia hiyo ki miundombinu na kiusalama

(3) mipakani regulations kama unatoka na mzigo wa biashara toka pretoria kwenda dar inakuwaje?

(4) vitu gani vya muhimu ambavyo ni lazima niwe navyo standby

(5) na safari inakadiria kuchukua siku ngapi (max)


(6) mwisho kabisa ni changamoto gani nitarajie kukutana nayo kwenye njia hiyo

(7) lakini pia ni mazuri gani nitarajie kukutana nayo kwenye safari hiyo
 
Ni very very expensive i have experience nimeshawahi kwenda huko na Road Trip utajuta Zambia kuivuka wanapenda sana rushwa askari wa huko
 
Mkuu zingatia tairi za hiyo gari usitumie ilizokuja na gari pitia Lusaka hapo Nakonde kuna road toll,bima,council hizo. kukata nadhani hazizidi 100 usd unapita Living Stone kazungura kuelekea Botswana kuingia Botswana unalipia usd 50 kwa kuingia na utakaporudi hautalipia tena utaruhusiwa kupita hizo karatasi kupata ni saa moja tuu pita boarder iliyo karibu na Gaborone kuingia haina magari mengi hata utakapotoka. South Africa kuingia haulipii kitu kupata document pale umbali kutoka Tunduma mpaka pretoria ni 2700 km..
mkuu unahesabu cku ngap kufka
 
Back
Top Bottom