Bajeti 2017/2018: Ukweli kuhusu kiasi kilichoongezwa kwa lita baada ya road licence kuondolewa

Na 60 ni lita ikiwa ni matumizi ya kawaida kwa mwezi.

Gari ndogo lita 60 ni full tank, ambayo kama gari haina tatizo na ukanyagaji wa accelerator ni wa kawaida. Unanusa mwezi kbs. Labda kama una safari ndefu.
Hayo ni matumizi yangu ya RAV 4 tena Old model, kwa siku kwenda ofisini na kurudi ni 16 km. Nawekaga mafuta 60,000 mwanzoni mwa mwezi na 60,000 ingine katikati ya mwezi.
 
Ila serikali ni wajanja sana, kila wanachofanya lazima waweke element ya ukamuaji, sawa road licence wameiweka kwenye mafuta ili tulipe kadri tunavyotumia bara bara, sasa kwa nini wameiweka hadi kwenye mafuta ya taa?

Hii nadhani ni makusudi, siyo kwamba hawajui kwamba hakuna chombo cha usafiri kinachotumia mafuta ya taa, basi kama ni kuzungumzia kwamba yanabebwa kupitia barabarani wangeipa hata rate ndogo, eg sh10 au 5.
 
Mkuu utakuwa unaishi Magorofa ya mnazi mmoja halafu ofisini kwako magogoni yawezekana,wenzio hiyo hela ya wiki mbili tu na baby walker zetu
Kama unaishi bagamoyo au Kimara mwisho kwanini uchome mafuta mpaka Posta mpya wakati kuna usafiri wa umma?
 
Ukweli kuna unafuu mkubwa mfanio kwangu mimi natumia lita 60 kwa mwezi (TZA 120,000) ina maana road license ni TZS 40 x 60 x12 = 28,800 badala ya TZS 200,000. Hata hivyo napata shida kwani nililipia road license 29/5/2017 ambayo itaisha 28/5/2018 hivyo kwangu mimi imekula.

Kuna uwezekano vile vile wa magari mabovu yaliyopaki muda mrefu kurudi barabarani na hii itaongeza ajali za barabarani.
Hizo lita 60 waenda kilomita ngapi mkuu!!!

Jivike umiliki wa Lory!!
Jivike umiliki wa bus.
Bus kwenda na kurudi Arusha to Dar sii chini ya lita 400(makadirio ya chini) ukiingia kwenye kikokotoo inakuwa hivi:-
400x40x15x12=2,880,000.

HII NI KUONGEZA GHARAMA ZA UENDESHAJI.
Hatimaye mwananchi anatwikwa mzigo huu na MIBUNGE YA CCM INASHANGILIA UPUMBAVU HUU.
 
Sioni sababu ya kupingana, bajeti ni nzuri na uzuri unatokana na presha ya wapinzani, na kama yaliyotekelezwa ndiyo ilikuwa hoja kuu ya upinzani, kunaubaya gani wakikaa kimya? Nani alisema kuwa wapinzani kazi yao ni kupinga kila jambo?, hapo tunapotoka, kazi yao ni kuikosoa serikali inapokwenda kinyume na kuipongeza inapokwenda vizuri. Sasa unaesema wapinzani wakinyamaza ujue jpm kawakamata, si kweli, wewe unapugania maji, maji yameletwa utapiga kelele za nini? Utakuwa na lako jambo.
 
kuna mahusiano gani ya road licence na mafuta ya taa sasa ni kumwongezea mzigo mwananchi wa kawaida kwa hii kodi itakuwa inalipwa kwa kiasi kikubwa na watu ambao hawakuwa na magari
 
Hizo lita 60 waenda kilomita ngapi mkuu!!!

Jivike umiliki wa Lory!!
Jivike umiliki wa bus.
Bus kwenda na kurudi Arusha to Dar sii chini ya lita 400(makadirio ya chini) ukiingia kwenye kikokotoo inakuwa hivi:-
400x40x15x12=2,880,000.

HII NI KUONGEZA GHARAMA ZA UENDESHAJI.
Hatimaye mwananchi anatwikwa mzigo huu na MIBUNGE YA CCM INASHANGILIA UPUMBAVU HUU.
Wewe hutaki serikali ipate mapato? Vile vile tujue kuwa kwa kuongeza kwenye mafuta hii kodi inakuwa "indirect tax" ambayo haiumi kama "direct tax"
 
Nimeona mitandao ya kijamii inapotosha hasa kwenye ukurasa wa UKUTA.
Upotoshaji: Kuna ongezeko la shilingi 300 kwa kila lita. UKUTA

USAHIHI: Kuna ongezeko la shilingi 40 kwa kila lita soma kipande cha hotuba ya Waziri hapo chini.
Jiridhishe kwa kusoma Hotuba ya Waziri sehemu ya 69(ii)
Myatake: Tunapotosha ili iweje?

View attachment 521534

Inawezekana alitaka kujumlisha kodi zote zilizopo kwenye MAFUTA kwa sasa.All in all aliyebebeshwa mzigo ni RAIA zaidi kuliko mwenye uwezo.

Mama ntilie akipandisha ndoo yake ya samaki lazima atalipia maradufu.Tusubiri kupandishiwa nauli.Issue ya mafuta ni very sensitive,sielewi namna walivyofanya mahesabu yao,lakini in short tutalipa zaidi kuliko ile ya mwaka kwa mwaka
 
Wewe hutaki serikali ipate mapato? Vile vile tujue kuwa kwa kuongeza kwenye mafuta hii kodi inakuwa "indirect tax" ambayo haiumi kama "direct tax"
Acha kunihusisha na ujinga.

Mimi si muumini wa kulipa kodi

Maana serikali haifanyi matakwa yangu, wahusikeje kwenye mapato yangu?
 
Ukweli kuna unafuu mkubwa mfanio kwangu mimi natumia lita 60 kwa mwezi (TZA 120,000) ina maana road license ni TZS 40 x 60 x12 = 28,800 badala ya TZS 200,000. Hata hivyo napata shida kwani nililipia road license 29/5/2017 ambayo itaisha 28/5/2018 hivyo kwangu mimi imekula.

Kuna uwezekano vile vile wa magari mabovu yaliyopaki muda mrefu kurudi barabarani na hii itaongeza ajali za barabarani.
Lita 60 kwa mwezi ni lita 2 kwa siku. Gari yako inashindana na San Lag. Mimi kwa wiki natumia lita 40!
 
Ukweli kuna unafuu mkubwa mfanio kwangu mimi natumia lita 60 kwa mwezi (TZA 120,000) ina maana road license ni TZS 40 x 60 x12 = 28,800 badala ya TZS 200,000. Hata hivyo napata shida kwani nililipia road license 29/5/2017 ambayo itaisha 28/5/2018 hivyo kwangu mimi imekula.

Kuna uwezekano vile vile wa magari mabovu yaliyopaki muda mrefu kurudi barabarani na hii itaongeza ajali za barabarani.
Sasa kulipa 28,000 kwa mwezi badala ya road license 200,000 kwa mwaka hapo ni nafuu au imekua ghali zaidi?
 
Back
Top Bottom