Yanayojiri Bungeni Dodoma: Ijumaa Tarehe 11 Aprili 2014 - Uwasilishaji wa Taarifa za Kamati

Wadau, anayewasilisha sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Namba 12, THUWAYBA E. KISASI. Ameanza kwa kutoa taarifa ya walio wengi ambapo ameanza Ibara ya Kwanza kwa kuondoa neno shirikisho na badala yake kuweka neno Jamhuri. Msingi wa marekebisho hayo ni hati ya muungano ambayo haitambui shirikisho badala yake inatambua neno Jamhuri. Pia amesema kuwa hakuna sehemu ya Tanzania iitwayo Tanganyika
 
Kuhusu Tunu za taifa, kamati imependekeza nyongeza ya tunu kama Amani, Muungano nk
 
Bi twaiba anasoma repoti ya kamati namba 12 kama ilivyoandaliwa kwenye kamati yao.
 
makamu mkiti wa kamati 12 Thuwaybah Kissasi anasoma maoni ya walio wengi mkiti ni Paul Kimiti
 
Hongera sana lusungo...duh, umejiunga na JF Januari 2014, una post 4,500 zaidi ya mimi niliyejiunga Mei 2008! Yaani kila siku unachangia post 45, wastani wa post mbili kwa saa bila kulala kuutetea mfumo tulionao (status quo). Keep it up, watu kama wewe CCM inawahitaji sana tu!

Nasikitika ulivyokosa hoja mpaka umehamia kwenye profile info za mtu....

Is this all? Reputable?
 
makamu mkiti wa kamati 12 Thuwaybah Kissasi anasoma maoni ya walio wengi mkiti ni Paul Kimiti
Pamoja sana Mkuu. Leo wanaong'ara ni wanawake. Nategemea pia atakayetoa maoni ya wachache ni mwanamke maana tangu jana mpaka leo, maoni ya wachache yanasomwa na wanaume tu
 
Wadau, kwanza kabisa naomba niwaombe radhi kwa kukosekana katika mjadala wa asubuhi kutokana na dharura ya kibinadamu. Ila kwa sasa tupo pamoja kuendeleza mjadala huu ulioanzishwa na ndugu yetu weston Songoro.​

Karibu sana tujuzane yanayojiri.
 
Wadau, anayewasilisha sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Namba 12, THUWAYBA E. KISASI. Ameanza kwa kutoa taarifa ya walio wengi ambapo ameanza Ibara ya Kwanza kwa kuondoa neno shirikisho na badala yake kuweka neno Jamhuri. Msingi wa marekebisho hayo ni hati ya muungano ambayo haitambui shirikisho badala yake inatambua neno Jamhuri. Pia amesema kuwa hakuna sehemu ya Tanzania iitwayo Tanganyika

Lissu na Jussa wako kamati gani? hatujawasikia kabisa.
 
Kupata haiwezi kumbuka hata wale 201 kuna Wanzanzibar ambao wanamuona tofauti na wazanzibar wa CCM.Na ukumbuke kwenye Bunge la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni almost nusu kwa nusu na waZanzibar CCM wanalijua hilo ndiyo maana wanawachezesha UPATU tu Wabunge wa CCM wadanganyika & Co.

Wale wa znz kundi la 201 unajua CCM ni wangapi? Je unawajua wajumbe vindaki ndaki wa CCM wasiojionesha wazi? Subiri ujionee ila nikiwa kama mwana CCM sijafurahishwa na suala hili la kubadilisha gamba na jina la kitabu kwa mabilioni mengi ya wananchi..
 
SURA YA SITA
maoni ya walio wengi Ibara ya 60(1) ni kwamba, wanapendekeza muundo wa serikali mbili ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar

Kuhusu vyombo vya utendaji wamependekeza serikali ya jamhuri ya muungano na serikali ya mapinduzi Zanzibar

kuhusu vyombo vya kutunga sheria, wamependekeza kuwe na vyombo viwili kuwa ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi

Kuhusu vyombo vya kutafsiri sheria (Mahakama), wamependekeza kuwe na Mahakama kama ilivyo kwenye katiba ya sasa
 
Kamati namba 12 kwa pamoja walikubaliana muundo wa serikali mbili ndiyo unaofaa kuendelea kutumika tanzania.
 
Mpk sasa nimeelewa kuwa kumekuwa na presha kubwa kwa wenyeviti wa kamati kujibu mapigo

Naona makamu mkiti anajibu hoja ya Duni Haji ila kwa woga.
 
Back
Top Bottom