Welcome to the World of Philosophical Quotes (Misemo ya Kifalsafa)

Hekima ya Mwenyezi Mungu

20210717_192623.png
 
Tunakutana na watu, tunawapenda, tunawaamini ,tunawajali na kuwathamini lakini mwisho hugeuka kuwa maadui zetu.

Usichoke kupenda na kutafuta marafiki, watakaogeuka kuwa maadui achana nao kwani ipo siku watakuja kukutafuta mashariki na magharibi na wasikuone, songa mbele wewe ni wa thamani hata kwa wengine.
 
Usipoteze siku yako kwa kuwekeza kwenye huzuni.Siku unayoanza kwa matatizo, mambo yako ovyo, huna kitu ndiyo siku unapaswa kuwa na furaha maishani mwako; kwasababu, pamoja na changamoto hizo, bado upo hai.Kumbuka, ukiishiwa kodi hujaishiwa dunia, ukiishiwa hela, hujaishiwa pumzi, ukiachwa na umpendaye hujaachwa na Moyo, macho, akili na kila kitu kilichokusaidia kumpata; hata dunia mlipokutania bado haijakuacha_
*Wewe jiamini, jisemee "mimi ni mshindi" pamoja na changamoto hizo bado unaye Roho Mtakatifu wa Mungu afanyaye kazi ndani mwako. Usijidharau.
 
Back
Top Bottom