Wazoefu wa magari ya mazda demio

kind2

Senior Member
Mar 6, 2016
102
45
Kuna mwenye uzoefu na mazda demio generation, 2 ya 2005, napenda kujua uimara wake hapa bongo na upatikanaji wa vifaa. Pia gharama zake kuitoa bandarini. Ina 1.3L, CIF $2000
 
Hivi hata befoward Auto parts mall watakua hawana kabisa vifaa vya mazda?

Ukiambiwa tafuta TOYOTA, hiyo mazda spare zake ni shida, maana yake si kwamba hakuna spare kabisa, tatizo ni upatikanaji kwa urahisi. Uwe na gari ambayo hata ukiwa safarini ukipata tatizo spare yake unaipata kwenye duka la karibu hata kama itakua fake, lakini itakufanya ufike na baadaye utatafuta "genuine part". Sasa kama utategemea spare ya "befoward" na wewe uko say Manyoni unaelekea Mwanza, huoni tayari safari imekwama?
 
Back
Top Bottom