Waziri wa Ujenzi awaondoa Watendaji wa TEMESA Kivukoni Dar kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,884
12,134
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewaondoa Watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Meneja wa Vivuko Kanda ya Mashariki na Kusini Mhandisi Lukombe King’ombe na Mkuu wa Kivuko cha Magogoni - Kigamboni, Idd Stamili Juma kwenye nafasi zao na kuagiza kupangiwa kazi nyingine kwa kushindwa kusimamia kikamilifu huduma bora kwa wananchi wanaotumia usafiri wa kivuko kati ya Magogoni - Kigamboni.
WhatsApp Image 2024-04-29 at 19.07.09_8e61c811.jpg

WhatsApp Image 2024-04-29 at 19.07.09_a19703ec.jpg
Waziri Bashungwa ametoa maagizo hayo Mkoani Dar es Salaam leo Aprili 29, 2024 wakati akikagua huduma zinazotolewa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kusikiliza changamoto za wananchi wanaotumia usafiri wa vivuko kati ya Magogoni na Kigamboni na kuonyesha kutoridhishwa na utoaji wa huduma za Wakala huo.

Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour kupeleka timu mpya ambayo itashirikiana kwa karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora za vivuko katika maeneo hayo.
WhatsApp Image 2024-04-29 at 19.07.09_f3867b51.jpg

WhatsApp Image 2024-04-29 at 19.07.09_7e48928b.jpg
“Nikuagize Katibu Mkuu kuangalia namna ambavyo utawabadilishia mazingira na kuwapa

majukumu mengine Meneja wa Kanda na Mkuu wa Kivuko cha Magogoni - Kigamboni na kuleta Watendeji wapya ambao watamsaidia Mtendaji Mkuu wa TEMESA kusimamia mkakati mpya wa maboresho ya TEMESA”, Amekaririwa Waziri Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amemuelekeza Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala kuanza mara moja kufanya maboresho katika majengo ya abiria katika maeneo yote nchini yenye huduma za vivuko, ambapo ameelekeza kuanza kuondoa feni mbovu na kuweka mpya katika eneo la Magogoni - Kigamboni.

“Nimekagua na nimejionea mwenyewe sehemu ya jengo la abiria linahitaji maboresho na usafi, nimeona zile feni kwanza ikiwashwa unakimbia kwa lile vumbi lililopo unaweza ukapata madhara makubwa ya kiafya hivyo zile feni ziondolewe mara moja na nimechukizwa na majibu yaliyokuwa yakitolewa sidhani kama Wizara kupitia TEMESA tunaweza kushindwa mambo madogo madogo kama haya”, Amesisitiza Bashungwa.

Kuhusu changamoto za mfumo wa malipo wa kukatia tiketi wa N-Card, Bashungwa amesema kuwa tayari timu zimeshafanya uchambuzi wa changamoto hiyo na yenyewe Serikali inakwenda kuyafanyia kazi.

Kadhalika, Bashungwa ameagiza TEMESA kuhakikisha wananchi wote wanaopata huduma za vivuko katika eneo la Magogoni na Kigamboni pia wawe wanalipa nauli kama mchango kwa ajili ya kusaidia uendeshaji wa huduma hiyo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameeleza kuwa taasisi nyingi zilizopo kwenye Mkoa wake zinafanya kazi kubwa na ameitaka pia TEMESA kuongeza ushirikiano na Mkoa kwa kuwa wao wanajihusisha moja kwa moja na wananchi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala ameeleza kuwa kwa sasa Kituo cha Magogoni - Kigamboni kina vivuko viwili ambavyo ni MV Kazi na MV Kigamboni vinavyotoa huduma za uvushaji kwa saa 24 na kufafanua kuwa kivuko cha MV Magogoni ambacho kimepelekwa kwenye matengenezo makubwa utekelezaji wake umefikia asilimia 55.2.
WhatsApp Image 2024-04-29 at 19.07.09_cd58409c.jpg

Pia soma
 
Kuna mahali Watendaji ni kama tunashindwa kujiongeza

Hivi kweli pamoja na kukusanya bilioni kadhaa Kwa Mwezi unashindwa hata kubadirisha Feni kweli?🙌

Hata kufanya ukarabati wa kibanda cha abiria kununua ndoo 2 za rangi nayo inahitaji uje uelekezwe na Wanasiasa?
 
Inawezekana kuna ukiritimba kwenye mchakato wa manunuzi.
 
Hizo feni si kama za mgahawani au chumbani jamani?
Kweli hela zote hizo mnajilimbikizia kwenye familia zenu ila hata Dari na hata air conditioning mmeshindwa basi hata Feni kubwa hakuna
Bora yafukuzwe tu
 
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewaondoa Watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Meneja wa Vivuko Kanda ya Mashariki na Kusini Mhandisi Lukombe King’ombe na Mkuu wa Kivuko cha Magogoni - Kigamboni, Idd Stamili Juma kwenye nafasi zao na kuagiza kupangiwa kazi nyingine kwa kushindwa kusimamia kikamilifu huduma bora kwa wananchi wanaotumia usafiri wa kivuko kati ya Magogoni - Kigamboni.
Waziri Bashungwa ametoa maagizo hayo Mkoani Dar es Salaam leo Aprili 29, 2024 wakati akikagua huduma zinazotolewa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kusikiliza changamoto za wananchi wanaotumia usafiri wa vivuko kati ya Magogoni na Kigamboni na kuonyesha kutoridhishwa na utoaji wa huduma za Wakala huo.

Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour kupeleka timu mpya ambayo itashirikiana kwa karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora za vivuko katika maeneo hayo.
“Nikuagize Katibu Mkuu kuangalia namna ambavyo utawabadilishia mazingira na kuwapa

majukumu mengine Meneja wa Kanda na Mkuu wa Kivuko cha Magogoni - Kigamboni na kuleta Watendeji wapya ambao watamsaidia Mtendaji Mkuu wa TEMESA kusimamia mkakati mpya wa maboresho ya TEMESA”, Amekaririwa Waziri Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amemuelekeza Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala kuanza mara moja kufanya maboresho katika majengo ya abiria katika maeneo yote nchini yenye huduma za vivuko, ambapo ameelekeza kuanza kuondoa feni mbovu na kuweka mpya katika eneo la Magogoni - Kigamboni.

“Nimekagua na nimejionea mwenyewe sehemu ya jengo la abiria linahitaji maboresho na usafi, nimeona zile feni kwanza ikiwashwa unakimbia kwa lile vumbi lililopo unaweza ukapata madhara makubwa ya kiafya hivyo zile feni ziondolewe mara moja na nimechukizwa na majibu yaliyokuwa yakitolewa sidhani kama Wizara kupitia TEMESA tunaweza kushindwa mambo madogo madogo kama haya”, Amesisitiza Bashungwa.

Kuhusu changamoto za mfumo wa malipo wa kukatia tiketi wa N-Card, Bashungwa amesema kuwa tayari timu zimeshafanya uchambuzi wa changamoto hiyo na yenyewe Serikali inakwenda kuyafanyia kazi.

Kadhalika, Bashungwa ameagiza TEMESA kuhakikisha wananchi wote wanaopata huduma za vivuko katika eneo la Magogoni na Kigamboni pia wawe wanalipa nauli kama mchango kwa ajili ya kusaidia uendeshaji wa huduma hiyo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameeleza kuwa taasisi nyingi zilizopo kwenye Mkoa wake zinafanya kazi kubwa na ameitaka pia TEMESA kuongeza ushirikiano na Mkoa kwa kuwa wao wanajihusisha moja kwa moja na wananchi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala ameeleza kuwa kwa sasa Kituo cha Magogoni - Kigamboni kina vivuko viwili ambavyo ni MV Kazi na MV Kigamboni vinavyotoa huduma za uvushaji kwa saa 24 na kufafanua kuwa kivuko cha MV Magogoni ambacho kimepelekwa kwenye matengenezo makubwa utekelezaji wake umefikia asilimia 55.2.

Pia soma
Waziri hajatatua tatizo bali amewatoa mhanga watendaji ambapo kimsingi kasoro zote alizoziona ni ubovu wa mipango na uodhinishaji wa bajeti za kuendesha vivuko.

Kivuko ni kama daraja. Wananchi wapate unafuu na huduma bora
 
Taifa letu limegawanyika katika sehemu kuu 3
.Watumishi ambao huonekana kuwa hawafanyi majukumu yao na ambao hufokewa na kulaumiwa kwa sababu tu hawana pa kusemea
2.Watawala ambao wao huonekana kuwa hawakosei katika kila maamuzi yao
3.Kundi kubwa la chawa ambao husifia watawala na kuwaponda watumishi wa umma
 
Yaani viongozi wa Tanzania!! Kwa hiyo TEMESA mlikua hamuoni hizo kasoro hadi leo alivyokuja Waziri??..TUWE TUNATIMIZA WAJIBU WETU
 
Tatizo sio temesa mbona kipindi ja JPM kulikua na huduma bora mara dufu alivoondoka tu Jiwe upuuzi wa hali ya juu ukarudi tatizo ni uongozi wa juu watu hawaogopi hawawajibiki wapo wapo tu ila km viongozi wa juu hawacheki na kima pale huduma zingekua bora.
 
Watu wanawindana sana huko maofisini hadi kupelekea watendaji kuwa waoga kufanya maamuzi sahii
Ukishakuwa accounting officer una mandate ya kufanya manunuzi hata ya bilioni kadhaa, ndiyo uje ushindwe kumlipa hata imprest Kijana wako akafanya huo ukarabati?

Me nadhani ni kukosa ubunifu ama uwezo kuwa mdogo ( kushindwa kujiongeza)
 
Mkuu maofisa wengi wa serikali ni wazito sana kufanya maamuzi sahii.
Mfano unakuta kuna project ya maendeleo na ipo chini ya ufadhiri hivyo kuwa vat exempted lakini mradi utachelewa kwa kutofanyia kazi mchakato wa exemption within Serikalini.
Kwenye issue hii ya kivuko kuna mambo ya kufikirika kwani watendaji wengi wa serikali wanapenda manunuzi na kunauwezekano mkubwa waliomba kufanya ukarabati ila hawajajibiwa maombi yao.
Kwa kipindi cha sasa nahisi makusanyo yote ya wakala wa serikali yanakusanywa sehemu moja hivyo kupelekea watendaji wakuu kutokuwa na maamuzi ya moja kwa moja
 
Back
Top Bottom