Waziri Doto Biteko: Kuadimika kwa mafuta ilikuwa ni dili, tumewadhibiti

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Mh Doto Biteko amesema wakati anaingia kwenye wizara hiyo alikuta kila mara mafuta kuadimika na kusababisha usumbufu na foleni kubwa kwenye vituo vya mafuta kote nchini, hali hiyo ilikuwa inatokea kila unapofika muda wa kutangaza bei mpya!

Biteko amesema suala hilo alilikomesha mara tu baada ya kushika wizara hiyo kwa kuwaita, kukaa nao na kuwapa onyo kali wapiga dili wote kwamba hatawalea kama walivyokuwa wanalelewa na January Makamba kwani atasimamia sheria kama alivyoapa.

Mh. Biteko amesema anashukuru kwani mara baada ya kikao hicho wapiga dili waliufyata na hakujatokea upungufu wa mafuta nchini.

Mh. Biteko ameyasema hayo wakati akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wabunge wakati wa kupitisha bajeti ya wizara ya nishati bungeni.
Mbona bei bado ziko juu au mmedhibiti kitu kipya
 
Hongera Biteko,
naona hata dili la umeme ni kama limeisha hivi, tuna takriban siku nne umeme hauja katika,maana ilikuwa on off,on off,Ilikuwa kero sana.Wametuunguzia vitu,wameua biashara za watu,they don't care.Yaani ilikuwa kama nchi haina mwenyewe vile.
 
Back
Top Bottom