Waziri Doto Biteko: Kuadimika kwa mafuta ilikuwa ni dili, tumewadhibiti

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,820
15,341
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Mh Doto Biteko amesema wakati anaingia kwenye wizara hiyo alikuta kila mara mafuta kuadimika na kusababisha usumbufu na foleni kubwa kwenye vituo vya mafuta kote nchini, hali hiyo ilikuwa inatokea kila unapofika muda wa kutangaza bei mpya!

Biteko amesema suala hilo alilikomesha mara tu baada ya kushika wizara hiyo kwa kuwaita, kukaa nao na kuwapa onyo kali wapiga dili wote kwamba hatawalea kama walivyokuwa wanalelewa na January Makamba kwani atasimamia sheria kama alivyoapa.

Mh. Biteko amesema anashukuru kwani mara baada ya kikao hicho wapiga dili waliufyata na hakujatokea upungufu wa mafuta nchini.

Mh. Biteko ameyasema hayo wakati akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wabunge wakati wa kupitisha bajeti ya wizara ya nishati bungeni.
 
1713516849490.jpg
 
Lakini foleni ya kupata mafuta hamna
Foleni itoke wapi sasa, yaani wanunue ranges, washindwe kununua wese? Sio kwa akili mbovu hizi zilizopo juu!

Ruto amesema maaskofu wasimpigie makofi kwakuwa bei ya mafuta kupungua hakuhusika kwa chochote ila ni soko la dunia....

Sijaona Ewura wakitangaza punguzo la bei ya mafuta, kwani nchi hii wanapata wapi mafuta yao?
 
Ina maana umesahau kwamba mafuta yalikuwa yanaadimika?
 
Sasa Bado Hajamaliza Kuondoa Makabdokando Bei Na Inajulikana CCM Ni Watu Wa Dili Chafu Hawataki Watanzania Wafurahie Maisha
 
Back
Top Bottom