Dtk. Biteko: Tumetekeleza agizo la Rais. Mgao wa Umeme imemalizika rasmi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
45,536
52,576
Akifungua Maonesho ya wiki ya Nishati,Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Biteko ametangaza kumalizika Kwa mgo wa Umeme Nchini.

Dk. Biteko amesema wamefanikiwa kutekeleza Agizo la Rais la kumaliza mgao wa umeme ndani ya miezi 6 ambayo walipewa.

Tanescoimefanikiwa kuwasha mitambo 3 ya kufua umeme bwawa la Mwalimu.

My Take
Wanaoumia Kwa mafanikio haya ni Chadema,saizi.wamehamia kwenye uzushi na Kiki ya Magari ya Serikali na umbea wa Mange Ili kujinusuru kisiasa.

====

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amefungua rasmi maonesho ya Wiki ya Nishati katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma ambapo amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha Sekta ya Nishati kutokana na nyenzo na maelekezo anayoyatoa ambayo yamempambanua kama kiongozi anayetatua matatizo ya wananchi kwa kutenda zaidi na sio maneno.

Dkt. Biteko amesema maelekezo ya Rais, Dkt. Samia pamoja na nyenzo anazozitoa kwa Wizara ya Nishati zimepelekea nchi sasa kuwa na umeme wa kutosha na kwamba hakuna mgawo tena huku kukiwa na mitambo ambayo ipo standby kuwashwa pale inapotokea hitilafu kwenye mitambo mingine ya uzalishaji umeme.

Aidha, kwa mikoa ambayo ipo nje ya gridi ya Taifa ikiwemo Katavi, Rukwa, Kigoma, Lindi na Mtwara, amesema kuwa yote itaunganishwa kwenye gridi ya Taifa kwani Rais, Dkt. Samia ameshatoa fedha za kutekeleza miradi ya umeme itakayoiunganisha mikoa hiyo na gridi ambayo tayari inaendelea.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko ameipongeza TANESCO kwa kuendelea kuimarisha utendaji kazi wao ikiwemo utatuzi wa changamoto za umeme akitolea mfano athari iliyotokea katika gridi ya umeme usiku wa siku ya Pasaka kutokana na hitilafu kwenye mfumo wa kudhibiti kiwango cha maji kwenye mitambo ya Kidatu ambapo tatizo hilo lilipaswa kushughulikiwa kwa siku tatu lakini TANESCO ilifanya jitihada na kutatua changamoto hiyo kwa muda wa masaa kadhaa.

Pamoja na pongezi hizo Dkt. Biteko ametoa angalizo kwa kampuni tanzu za TANESCO kuhusu utendaji kazi wao ikiwemo Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC) ambapo kampuni hiyo ilitoa ahadi ya kuanza uchorongaji wa visima vya Jotoardhi katika eneo la Ngozi Mbeya tarehe 1 Aprili 2024 lakini bado hawajaanza kazi hiyo hivyo amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati kuisimamia ipasavyo kampuni hiyo ili nchi iweze kupata umeme wa Jeothemo.
 
Hawa kina Etwege na Crimea watasema pongezi ziende kwa jiwe kwa kujenga bwawa la umeme la Nyerere!
Hao ni loosers ,wanaumia sana maana Jiwe aliwaaminish hakuna wa kukamilisha miradi Wala kuanzisha mipya.

Sasa Samia sio tuu amekamilisha Bali hakuna kilichosimama na hakuna visingizio sekta zote ni 🔥🔥,Jiwe alishindwa akawa anasingizia Sgr na bwawa 😂😂
 
Hao ni loosers ,wanaumia sana maana Jiwe aliwaaminish hakuna wa kukamilisha miradi Wala kuanzisha mipya.

Sasa Samia sio tuu amekamilisha Bali hakuna kilichosimama na hakuna visingizio sekta zote ni 🔥🔥,Jiwe alishindwa akawa anasingizia Sgr na bwawa 😂😂
Bwawa la umeme la Nyerere bado halijakamilika, SGR nayo bado haijakamilika, Airport Mwanza bado, Daraja la Kigongo Busisi bado
 
Bwawa la umeme la Nyerere bado halijakamilika, SGR nayo bado haijakamilika, Airport Mwanza bado, Daraja la Kigongo Busisi bado
Kwa nini Mwendokasi alishindwa kukamilisha Kwa miaka 5 aloyokaa?

Bwawa limekamilika
Sgr Dar-Dom imekamilika
Kigongo -Bisisi linamalizika disemba
Airport ya Mwanza inajengwa upya baada ya kutekekezwa na Mwendazake na wakina Mayanga walipiga hela
 
Bwawa la umeme la Nyerere bado halijakamilika, SGR nayo bado haijakamilika, Airport Mwanza bado, Daraja la Kigongo Busisi bado
Chadema wangeweza kuyafanya haya yote kwa nusu saa tu!, chadomophobia ikikukumbu na ufahamu huwa unahama kwa 100%.
""CHADOMOPHOBIA""NI JANGA KWA TAIFA, HAWA HUWA HAWAONI JEMA!. WALA WEMA KWA TAIFA.
 
Back
Top Bottom