Waziri Bashungwa Akagua KM 20 za Barabara wa Miguu, Aagiza TANROADS & TARURA Kushirikiana Kusimamia Ubora

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,033
974
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amewaagiza Mameneja wa Mikoa wa Wakala wa Barabara (TANROADS) kushirikiana na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) katika usimamizi wa Ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara ikiwemo kushirikiana katika upimaji wa ubora na viwango vya ukarabati wa barabara ya changarawe.

Bashungwa ameeleza hayo leo tarehe 29 Machi 2024 baada ya kutembea kilometa 20 kwa miguu Wakati akikagua Ujenzi wa Barabara ya Bweranyange - Kafunjo kwa Kiwango cha Changarawe wilayani Karagwe Mkoani Kagera.

“Namuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa Kagera kushirikiana na Meneja wa TARURA Mkoa Kagera na Maneneja wote nchini kushirikiana katika kuimarisha usimamizi wa maetengenezo ya barabara za vijijini ambapo TARURA wanaitaji utalaamu kutoka TANROADS kwenye vipomo” amesisitiza Bashungwa

Aidha, Waziri Bashungwa amemtaka Meneja wa TARURA wilaya Karagwe kusimamia Wakandarasi wote wanaotekeleza matengenezo ya barabara, kusimamia mashariti ya mikataba ikiwa ni pamoja na kushirikisha Madiwani na Wananchi katika maeneo ambayo wanatekeleza miradi.

“Muwashirikishe Madiwani wa kata huska, wawe na BOQ na wajue fedha iliyotolewa na Serikali katika eneo lake na kufahamu fedha hiyo itajenga barabara yenye kiwango gani, karavati ngavi na mambo yote Mkandarasi anayopaswa kuyatekeleza” amesema Bashungwa

Vile vile, Waziri Bashungwa amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha za ukarabari wa Kiwango cha Changarawe Barabara za Bweranyange - Kafunjo km 20, Katojo - Ihembe - Rugu km 26, Kituntu - Rwakiro km 6 na Bweranganye Sekondari - Akagando km 6.

Kwa upande wake, Meneja wa TARURA wilaya Karagwe Eng Kalimbula Malimi amesema matengenezo ya barabara ya Bweranyange - Kafunjo km 20 kwa Kiwango cha Changarawe utagharimu milioni 904.5 ambapo kazi ya utekelezaji inaendelea.

Naye, Diwani wa Kata ya Nyabiyonza, Thomas Rwentabaza ameishukuru Seikali kwa kuwezesha matengenezo makubwa ya barabara hiyo ambayo ilikuwa haijawahi kutengewa fedha yoyote.

WhatsApp Image 2024-03-29 at 16.15.08.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-29 at 16.15.08(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-29 at 16.15.09.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-29 at 16.15.09(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-29 at 16.15.10.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-29 at 16.15.11.jpeg
 
Back
Top Bottom