KERO Watumishi Halmashauri ya Momba walazimishwa kuhudhuria Sherehe za Muungano kwa gharama zao

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na sintofahamu kwa watumishi wa Halmashauri hii kulazimishwa kuhudhuria sherehe za Muungano zinazotajiwa kufanyika maeneo ya Kamsamba kuanzia tarehe 25/4/2024 na kilele chake ni tarehe 26/4/2024.

Agizo linawataka watumishi hao kufika maeneo hayo kuanzia saa 2:00 asubuhi siku ya tarehe 25/4/2024 na kukesha kuamkia siku ya Muungano tarehe 26/4/2024 bila kujua suala la usafiri na huduma zingine za kibinadamu n.k.

Wahanga wakubwa ni Walimu wanaotokea kata Za Jirani na Kamsamba, Wakuu wa shule wote na Maafisa Elimu Kata wote kwa Halmashauri nzima.

Je, hii ni sawa?

Kwanini mamlaka ziwalazimishe watumishi kusherehekea Muungano?

Sheria ipi inalazimisha mtu kusherehekea Muungano huu?

IMG_1206.jpeg
 
View attachment 2974132
Duuuuu kwani wasipoenda watawapiga viboko
 
Hii sio sawa, ni ukandamizaji mkubwa wa haki za watu
 
Kwa nini wamechelewa kulalamika?
Ina maana leo walimu wa huko wameamkia viwanjani kwenye maadhimisho!!🤣
 
Hii serikali ina nyanyasa sana walimu wake na hasa kuwalazimisha kuwahusisha kwenye mambo ambayo hata hayawahusu , inamaana watumishi wa serikali ni walimu pekee? Au wanaponzwa na wingi wao ?

Serikali iache huu unyanyasaji walimu nao wana haki sawa kabisa na watumishi wengine na wana hitaji kuheshimiwa kama watumishi wengine
 
Hii sio sawa, ni ukandamizaji mkubwa wa haki za watu
Tatizo kubwa pia CWT kugeuka kuwa wakala wa serikali maana hapa kama chama cha wafanyakazi kilitakiwa kitoe tamko kuzuia huu unyanyasaji unaendelea kuota mizizi maana kuanzia mbio za mwenge ni walimu na tunako elekea nahisi hadi ziara za chama wataitwa walimu waende
 
Nilipita pahala huku kwetu nikakuta wanafunzi na walimu wao wamekusanyika sehemu kuna kama hafla fulani kwa bahati nzuri nikamuona mwalimu mmoja ninayemjua nikamuuliza kulikoni hapo akaniambia ni maandalizi ya siku ya muungano kesho(leo)
 
Kumekuwa na sintofahamu kwa watumishi wa Halmashauri hii kulazimishwa kuhudhuria sherehe za Muungano zinazotajiwa kufanyika maeneo ya Kamsamba kuanzia tarehe 25/4/2024 na kilele chake ni tarehe 26/4/2024.

Agizo linawataka watumishi hao kufika maeneo hayo kuanzia saa 2:00 asubuhi siku ya tarehe 25/4/2024 na kukesha kuamkia siku ya Muungano tarehe 26/4/2024 bila kujua suala la usafiri na huduma zingine za kibinadamu n.k.

Wahanga wakubwa ni Walimu wanaotokea kata Za Jirani na Kamsamba, Wakuu wa shule wote na Maafisa Elimu Kata wote kwa Halmashauri nzima.

Je, hii ni sawa?

Kwanini mamlaka ziwalazimishe watumishi kusherehekea Muungano?

Sheria ipi inalazimisha mtu kusherehekea Muungano huu?

View attachment 2974132
Mwenye kujua faida za muungano ni sir-100
 
... Acha kazi anzisha biashara zako ambazo hautakandamizwa Wala kubugudhiwa. ...
Mbona kwenda kusimamia uchaguzi hamkatai ilihali nyie sio wanasiasa.
Ukikubali kuolewa sharti ulale bila nguo
 
SIO waalimu tu karibia taasisi nyingi wanaenda kwa gharama zao. Naona na wanafunzi wa veta pia wanaenda kwa gharama zao.

Ni either serikali iache kufanya hizi shughuli Au kila mtu ajilipie. Mana kulipia watu nchi nzima nibora ifanye vitu vya msingi
 
Kwa hiyo wewe ni sawa na yule ambaye akisha zaliwa na mama yake kisha akalelewa akawa mtu mzima anaanza kumwambia mama yake hata mimi nina uwezo kukuzaa si dio?
Kama ni mwanamke yupo sahihi kama huo uwezo anao.

Sitashangaa kama wewe ni mwalimu.
 
Back
Top Bottom