A
Anonymous
Guest
Habari wakuu,
Inasikitisha sana kuona kiongozi wetu badala awe mstari wa mbele kuwajali na kushirikiana na watumishi, yeye amekuwa ndio mtu wa kuwavunja ari, moyo, kukatisha tamaa na zaidi amekuwa ni mtu anayeongoza kutegeneza migogoro hali inayopelekea kuharibu upelekaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Huyu kiongozi, hajawahi kuheshimu wala kufuata misingi ya utawala bora na ameshagombana na wakurugenzi kadhaa ambao wamepita na kufanya kazi katika halmashauri ya Momba, ameshaingia migogoro na wakuu wa wilaya kadhaa waliopita na kufanya kazi katika halmashauri ya wilaya ya Momba, ameshagombana na maafisa utumishi wote waliowahi kuhudumu katika halmashauri ya Momba ameshagombana na wabunge wote waliowahi kuhudumu na zaidi huyu anayehudumu sasa vita kubwa ikiwa ni ubunge 2025, ameshagombana na maafisa watendaji wengi na kuchochea wahamishwe kwenye kata yake, ameshagombana na maafisa kilimo wengi na kuchochea wahamishwe katika kata yake na maeneo mengine ya halmashauri, ameshagombana na kila viongozi wa idara kuanzia ngazi ya wilaya mpaka kijiji.
Mbaya zaidi amekuwa ni mla rushwa mkubwa kiasi cha kuathiri maendeleo ya taasisi mbalimbali na halmashauri Kwa ujumla. Hakuna ujenzi ambao hajawahi kuingilia iwe shule, vituo vya afya visima n.k. Kuna mradi wa maji kwenye kata yake ambao ulihitaji kuchimbwa kisima kipya na kujengwa tanki jipya lakini hakuna kilichofanyika badala yake lilikarabatiwa tanki lililokuwepo na kisima kinachotumika ni cha kanisa katoliki hali inayopelekea kuathiri huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi. Kuna wakuu wa shule kadhaa waliwajibishwa kwa sababu ya kushindwa kukamilisha miradi kwenye taasisi zao kwa sababu huyu mwenyekiti aliwaomba rushwa Kwa vitisho ikiwemo shule ya sekondari Uwanda.
Mbaya zaidi alishawahi kunukuliwa akisema katika hadhara ya watu kwamba Rais Samia hajawahi kumkubali na analazimika kutokuonyesha kwa viongozi wa juu kwa sababu ya kulinda ugali wake kitu ni hatari kwa serikali na ustawi wa Chama Cha Mapinduzi.
Mwisho nashauri chama changu cha mapinduzi na serikali kwa ujumla, ufanyike uchunguzi juu ya haya niliyoyabainisha na ikiwezekana maamuzi magumu yafanyike ili kulinda hadhi ya chama, watumishi kudhalilishwa na kuonewa pasipo sababu za msingi.