Watendaji wa kata ni Makada wa CCM au ni watumishi wa umma? Naona Arusha wamevaa sare za chama na wanaandamana

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
912
4,246
Mrisho Gambo ameongoza maandamano ya madiwani, wenyeviti wa mitaa na watendaji wa kata.

Kwa ufahamu wangu watendaji wa kata ni watumishi waajiriwa wa serikali kama walivyo waalimu sambamba. Je, ni sahihi wao kama watumishi wa umma kuvaa nguo za chama na kuandamana?

Lakini maandamano si walisema pia kwamba yanakwamisha maendeleo? CHADEMA wametembea na kijiji CCM umeona sasa mziki wa Mbowe na Lisu unazoa watu wameamua kuabdamisha viongozi, kwanini wasifanye maandamano ya wananchi?
 
Ni kiherehere na hii inalazimishwa , na sheria ziko wazi, mtumishi wa umma marufuku kujihusisha na siasa
 
Watendaji wa vijiji, mitaa, kata, afisa tarafa, ded, das na Ras wote ni CCM machoni. Ukivaa gwanda au ukashabikia chadema ndani ya saa 48 unakuwa umeanza kupata misukosuko.

Walimu, manesi na madereva aka kada za wangi utahamishiwa bush tu.
 
Back
Top Bottom