Mbunge Ntate Awasisitizi Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata Kuwekeza Katika UTT

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,994
961
Mbunge wa Viti Maalum (Anayewakilisha Wafanyakazi Nchini) Anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Janejelly James Ntate, leo tarehe 10 Oktoba, 2023 ameendeSemina ya Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Semina hiyo iliyohudhuriwa pia na baadhi ya viongozi wa CCM Wilaya na Mkoa, imefanyika katika Ukumbi wa Arnatoglou, Ilala Jijini Dar es Salaam.

Semina ya Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa wote wa Mkoa wa Dar es Salaam iliendeshwa na Taasisi ya Kifedha ya Serikali inayojulikana kama Unity Trust of Tanzania (UTT).

Mbunge Janejelly Ntate amesema lengo la Semina hiyo kutoka UTT - AMIS ni kusikiliza maoni yao na changamoto zao katika utekelezaji wa majukumu yao.

Unity Trust of Tanzania (UTT) ni taasisi ya Kifedha iliyopo chini ya Serikali inayojihusisha na Uwekezaji wa kuuza vipande au hisa au hatifungani.

"Nimewanunulia vipande/Hisa vyenye thamani ya shilingi Elfu-20, kwa Watendaji wote wa Kata katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa Kata zote na mpaka kufikia kustaafu kwao kutawasaidia kuwa wamefika mahali pazuri kiuchumi" - Mhe. Janejelly James Ntate, Mbunge wa Viti Maalum.

"Kwa niaba ya watumishi wa umma napenda kutoa shukurani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya uongozi wake amefanya mageuzi makubwa hasa katika maslahi ya wafanyakazi na UTT kwa kuja kufanya Semina bure kwa Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa. Watumishi tuko pamoja na Rais Samia na kura tutampigia kwa kishindo ifikapo 2025.

Mwisho

WhatsApp Image 2023-10-10 at 16.06.08.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-10 at 16.06.09.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-10 at 16.06.09(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-10-10 at 16.06.09(2).jpeg
 
Back
Top Bottom