RC Mwassa awapa rungu maafisa tarafa na watendaji kata kusimamia miradi, kuinua uchumi, ukusanyaji mapato, kutatua kero na kujipanga kwa uchaguzi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
331
415
Atangaza neema Mei Mosi kwa watakaotatua migogoro na kero za wananchi kwa wingi na ufanisi mkoani Kagera

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa amesema Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata ni wadau muhimu sana katika kusukuma maendeleo kwani ndiyo wako karibu na wananchi na wana nafasi kubwa sana kusimamia miradi kwa kuhakikisha inafanyika kwa ufanisi, kuinua uchumi katika maeneo yao, kusikiliza na kutatua kero kwa kuwa na usuluhishi mzuri wa migogoro ya wananchi, kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato na kujipanga kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika baadae mwaka huu ili pasitokee dosari yoyote ile.

RC Mwassa ameyasema hayo Jana Jumanne Aprili 23, 2024 kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Bukoba mjini Bukoba wakati akifunga semina ya siku mbili iliyoandaliwa na TAMISEMI kwa ajili ya kuwaongezea uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu yao Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata wote wa Mkoa wa Kagera.

"Nyinyi Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata ni watu muhimu sana kule chini kusukuma maendeleo. Kasimamieni vyema ukusanyaji wa mapato kama maelekezo ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wizara ya TAMISEMI na kila mmoja apambane tuongeze mapato mana bila fedha hatuwezi kufanya maendeleo. Lakini lazima hizo hela mzisimamie na value for money (thamani ya fedha) ionekane katika hii miradi inayotekelezwa na lazima mfuatilie na kusimamia kwa ukaribu sana

"Lakini kasimamieni kuinua uchumi kupitia kilimo kwasababu kwasasa tunaleta miche ya kahawa, migomba, viungo, alizeti n.k nyinyi mna nafasi ya kusimamia kuhakikisha vinakua ili tupate maendeleo. Lakini niwaombe tukatatue migogoro ya wananchi mana mpaka mwananchi afike kwa DC au RC anakua ametua fedha nyingi lakini nyinyi mko pale na wananchi na hii migogoro muitatue toka ikiwa midogo kabla haijawa mikubwa mpaka kusababisha wananchi kuuana"

"Wote mnafahamu mwaka huu tunajiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mjipange kusimamia zoezi vyema na linakua huru na haki na hatutegemei dosari. Mhe. Rais Samia ameimarisha siasa na kila Chama kinafanya shughuli zake." Alisema RC Mwassa.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka viongozi hao wote waliopata mafunzo kufanya ukaguzi wa wanafunzi walichaguliwa kwenye shule za msingi na sekondari kama wapo ili kuondoa changamoto ya kuwekewa wanafunzi wengi kwenye taarifa na wakuu wa shule ili wapate hela nyingi ya uendeshaji (capitatio) huku akisisitiza kusimamia ulinzi na usalama wa maeneo yao na kuwa waadilifu na mfano bora katika jamii.

Katika hatua nyingine, RC Mwassa wakati wa ufungaji mafunzo hayo ametangaza mashindano ya utatuzi wa kero kwa viongozi hao na kuwaeleza kwamba atakayetatua kero nyingi na kwa ufanisi basi atampatia zawadi siku ya Mei Mosi mwaka huu 2024.
 

Attachments

  • IMG-20240424-WA0003.jpg
    IMG-20240424-WA0003.jpg
    346 KB · Views: 2
  • IMG-20240424-WA0005.jpg
    IMG-20240424-WA0005.jpg
    534.6 KB · Views: 2
  • IMG-20240424-WA0007.jpg
    IMG-20240424-WA0007.jpg
    478.5 KB · Views: 2
  • IMG-20240424-WA0011.jpg
    IMG-20240424-WA0011.jpg
    469.5 KB · Views: 1
  • IMG-20240424-WA0010.jpg
    IMG-20240424-WA0010.jpg
    443.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom