Wanaume tunapenda kuhitajika

flamini

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
511
513
Oyaa wazee wanawake wakisasa kuna kitu ibaidi waelewe,kwa sababu wanawake wa kisasa hawawafanyi wanaume kujihisi wanahitajika tena.

Siku hizi, warembo wetu wamepata kipato zaidi ya wanaume, wanahitimu kwa asilimia kubwa zaidi kuliko wanaume, na wana uhuru mkubwa zaidi kuliko wanawake wa miongo iliyopita. Hilo si jambo baya. Uhuru mpya wa wanawake wetu unapaswa kusherehekewa.

Hata hivyo, wanawake wetu na wengine ulimwenguni wanapaswa kutambua kwamba, kibaiolojia, wanaume bado wanavutiwa na wanawake ambao wanamfanya mwanaume kujihisi anahitajika. Katika enzi za kisasa, means kuwa wanaume wa kisasa hawatoi tena kitu ambacho wanawake hawana (kwa mfano, pesa, elimu)

Kwa hivyo hatua ya asili ni kwa wanaume wa sasa hivi ambao wamekosa kuhitajika ni kutafuta wanawake ambao wanamfanya mwanaume kujihisi anahitajika. Njia rahisi ni kwa mwanaume kutafuta chini kiuchumi.

Mwanaume wa jiji kubwa, akipata mshahara wa millioni kwa mwezi hawezi tena kuwavutia wanawake wa kisasa ambao pia wanapata zaidi ya millioni au sawasawa. Kwahiyo kama mwanaume ufanye nini ? Anaweza kwenda katika kijijini na kumchumbia msichana wa kijijini maskini... Au atafute wa mjini ambae hajamvutia ila ni maskini zaidi yake.

Ukweli kwamba anachumbia "nje ya daraja lake"
 
Mkuu inawezekana kuna namna umeongea ukweli ila ndani ya thread yako ni kama imeonesha kuna low self esteem . Ni kama kuna aina ya wanawake unawatamani ila kuwapata huwezi sababu ya kipato cha "around 1 million"..

Nikuambie tu ukweli, toka enzi hizo social classes zilikuwepo na si kila aina ya mwanamke au mwanaume kila mtu alikuwa ana access nayo. Kwa hiyo jitahidi tu ku_deal na wanaoendana na hali yako kuepuka stress
 
Tafuta kigezo kingine mkuu, hicho kigezo cha 'kuwa na mwanamke uliyemzidi' hakifai siku hizi

Ila kuna ukweli hapa

Kuna mahali niliona wanawake wanavyotongoza, anajifanya simu yake mbovu anakupa umtengezee, basi unajiona mwambaaa.... kumbe anaigiza kukujaza bichwa

Lakini siku hizi wanasema unatakiwa uwazidi dhambi.... sa sijui wanamaanisha nini😅
 
Back
Top Bottom