Wanaoshinda kwenye computer/laptop na wanapata pesa huwa wanafanya kazi gani huko?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,500
4,791
Nina washikaji zangu ambao sipo karibu nao saana kiasi Cha kwamba hawawezi kuniambia mishe zao, mmoja tulisoma name o-level alifeli form two akaacha shule, yeye kapanga nyumba nzima hapo buhongwa-Mwanza, Kazi yake aieleweki anashinda ndani kwenye computer kuanzia asubuhi mpaka jionii, labda jioni ndio anatoka kwenda kujipumzisha, nikajaribu kumchombeza nimuulize aniambie labda anamchongo gani?

Nikamuuliza kuhusu freelencer, sijui Upwork vyote hivyo havijui ila alichonambia TU ni kwamba anauza coin/Bitcoin Kuna site anaenda kununua kwa bei rahisi then na yeye anaziuza kwa Bei ya juu, ni kama wakala tu, sijui ndio mambo ya cryptocurrency kidogo nikaanza kumuelewa, lakini Sasa maendeleo yake ni ya kutisha amenunua gari x-trail kanunua kiwanja million 12 mpaka nimeshangaa wakuu.

Mwingine yupo naye elimu yake ya form four tu lakini alinambia ana blog /website ya mziki lakini anaingiza pesa kubwa sana anajenga.

Nimeshindwa kuelewa kitu kimoja, wote hao hawana background yoyote ya mambo ya ICT, Lakini inaonekana wanachokifanya kinawalipa.

Je unahisi wanafanya kazi gani? Ili nasisi tujiongeze huko tupate hata laki mbili kwa mwezi. Najua JF Ni kisima Cha maarifa hatuwezi kubaniana nondo kama hizi.
 
Kwanza una uhakika hawana background yoyote ya mambo ya ICT?

Maana huko huwezi ukaenda ukiwa mweupe tu Mzee , lazima uwe na ABC za IT.

Na uwe umeiva kweli, maana kama freelancer utapewa task ufanye halafu utabaki unatonoa tu macho.
 
Back
Top Bottom