Unataka kupata kazi mara moja? Bila kukataliwa na mtu au kampuni yoyote? Usitume au kuomba kazi. Njia rahisi ni hii

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
767
1,656
Greetings everybody!

Leo naenda kukufundisha ujuzi wa juu zaidi jinsi utakavyoweza kupata kazi kwa mtu fulani mwenye pesa au hata kampuni kubwa. Hapa inategemea tu confidence yako ipo vipi.

Nataka nisaidie watu wote wanaosota kuandika resumes na kutuma maombi wakitafuta kazi zisizokuwepo.

Yes siku hizi hakuna kazi kwasababu wanaotafuta kazi mara nyingi hawana uwezo wakuongeza VALUE katika kazi husika. Ufanisi ni mdogo sana.

Sababu ya ufanisi kuwa mdogo kati ya watu wengi wanaotuma maombi ya kazi kuanzia Jan hadi December ni kwasababu huko walipotoka (university/college) walikuwa wanajifunza mambo amabyo hayaongezi Value katika biashara.

Wengi wanaotuma maombi ya kazi wanadhani college degrees walizonazo ndiyo Skills zenyewe wakishindwa kuelewa Skills ni ule ujuzi wakuweza kufanya kazi inayoongeza valaue hata kama huna college degree.

Hapa unatakiwa ufahamu dunia ya sasa no one cares about your university degree.

Hizi degree zote ni outdated tu.

Business people like myself tunaangalia value unayoongeza katika Business. Tofauti na hapo we don’t care about your university degree.

Hapa kuna wataosema aaaah siyo kweli lakini niwaambie tu ukiwa unao uwezo wakuongeza value katika biashara ya mtu au shirika fulani trust me hakuna atakayekataa kukupa nafasi.

I’m speaking this from experience.

Acha kuwa mtu wakuandika resume na kutuma maombi kutafuta kazi.

Hutapata.

Bado unaendelea kunisoma?

Ok.

Sasa tuangalie mambo matatu (3) yakufanya ili upate kazi na kutengeneza pesa all day everyday.

1 • Jifunze kuwafanikishia watu wenye pesa mambo yao.

Ok ngoja nifafanue hii point.

Watu wengi wanaoendesha Business wanamambo mengi sana na wanayohitaji kufanikishiwa.

Kwa mfano mimi binafsi nimekuwa nikiwatafutia wafanyabiasha wa utalii hapa Arusha ( accommodation) kupata wageni toka nje wakulala kwenye apartment, lodges, campsites, hostels wanazomiliki.

Na nilianza kazi hizi si kwakuandika barua ya maombi.

Nikifahamu mtu falani ana biashara ya namna hii namfuata nampatia darasa jinsi nitakavyoongeza faida “value” kwenye Business yake.

Na hapa wala sihangaiki sijui aniajiri na kunilipa mshahara.

Nop.

Mimi ni entrepreneur. Nafahamu ukishakuwa na mentality ya kulipwa mshahara basi na akili inalala.

Mimi nalipwa kwa result.

Na ninajipangia mwenyewe jinsi nitakavyofanya kazi husika.

2 • Kuwa mzungumzaji mzuri unayefahamu kushawishi.

Wait.

Hapa kuna kitu nataka niseme. Watu wengi wanadhani kumshawishi mtu mwingine ni kama ulaghai fulani hivi.

You are wrong.

Kama wewe huwezi na haupo tayari kushawishi watu basi hutokaa upate pesa.

Persuasion ndiyo SKILL muhimu na ya juu zaidi ili ufanikiwe kwenye Business.

Pia fahamu wafanyabiashara wote waliofanikiwa wanayo hii talanta.

Hapa Point ya kuchukua ni kwamba inabidi uanze kuwasiliana na watu wenye biashara. Ni rahisi tu. Wewe waendee kwa lengo si lakuomba kazi nop unaenda kwa lengo lakuwaonyesha jinsi unavyoweza kuongeza value.

Kwa mfano juzi December 4, 2019 kuna boss mmoja hapa Arusha (he owns lodges in Arusha and Serengeti) nilikuwa namwonyesha jinsi ninavyoweza kumpatia wageni wakulala kwenye lodges zake kama atakubali kunilipa kwa kila result nitakayo achieve. Leo December 6 nimempatia wageni wawili wanaofikia fikia kwenye lodge yake for 6 days.

Umeona hapa?

Kwanza kabisa nimejitengenezea kazi. Kwasababu nafahamu hivi ndivyo Business people wanachotaka.

Haiingii akilini mtu akulipe mshahara kila mwezi wakati hakuna result yoyote unayoleta.

Ukiwa Na Mentality ya kutuma maombi na kuajiriwa katika Hii traditional way utasubiri sana. Na nikuambie tu hutoweza kuwa boss. Kwasababu huna idea how wealth is created.

3 • Focus kutoa result siyo kiasi gani unapiga kazi.

Hapa nataka nikuambie entrepreneurs hatujali masaa mangapi umefanya kazi kama hakuna result wewe ni bure tu.

Na hapa ndiyo maana watu wengi wanapofeli baada ya kupata kazi kama hizi nilizosema kwasababu wanadhani wakimwonyesha tajiri wanafanya kazi kwa bidii basi wataheshimika.

Nop. You are wrong my friend.

Fanya kazi ili tu unayoweza kutoa result tena kwa muda mfupi.

Kama huwezi hivyo unaweza tumia mbinu ya ku out-source kazi kuwapa wanaoweza na wakikamilisha tajiri anajuwa ni wewe ndiyo umefanya.

Unakuta watu wanakomaa na kazi kwa siku nyingi wakati wangeweza kumaliza ndani ya muda mfupi tu kama wange outsource hiyo kazi.

Hapa mfano mzuri ni mimi binafsi navyofanya kazi UpWork.

Sifanyi kila kitu mimi hasahasa nikipata gig ya bei kubwa $500+

Natoa baadhi ya kazi kwa watu ninaofahamiana nao hapa JF na kuwalipa kama tunavyokubaliana. Kwa huu ujanja kazi inakamilika haraka na mimi naonekana ni mtu ninayeweza kutoa result.

Wakuu, mwenye macho na aone. Mwenye masiko na asikie.

Ukiendelea kulia njaa basi hiyo ni tatizo lako mwenyewe.

Pia kama unahitaji kujifunza zaidi niandikie ujumbe I will see how I’m gonna help.

Cheers 🥂
 
Somo limeenda shule, hongera uko vizuri.

Yep.... nimeamua kuweka haya mambo wazi ili wanaohangaika kutafuta kazi wafahamu jinsi kazi zinavyopatikana.

Nafahamu watu wengi wanakwama kwasababu wanakosa perspectives.

Mimi ninaweza kumsaidia yeyote anayetaka kutengeneza pesa kwa kumwonyesha opportunity.

Im very good at identifying opportunities.

Karibu sana.
 
Back
Top Bottom