Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,359
- 11,238
Vita vilipoanza baada ya shambulio la oktoba 7 na kwa kujua ukubwa wa jeshi la Israel haikutarajiwa kufikisha hata wiki moja kabla Israel kukamilisha malengo yake ambayo na kuwafuta Hamas na kuwapata mateka wote waliokuwa wameshikiliwa na Hamas.
Watu wa Gaza zaidi ya 35,000 mpaka sasa wameshauliwa na uharibifu ni mkubwa sana.Kwa nguvu iliyotumika Israel ilitaraji ingewadhoofisha Hamas na kukubali matakwa yao kubwa ikiwa ni kujisalimisha na kupatiwa mahitaji ya kila siku kama chakula na maji ambavyo Israel imevitumia kama silaha ya kivita.
Kinyume na matarajio Hamas hawajarudi nyuma katika madai yao mawili muhimu ambayo ni Israel kuondosha jeshi Gaza na kuruhusu watu warudi majumbani kwao popote walipohamishwa Gaza.
Watu wa karibu na Netanyahu kwa kuona hilo ni kama tangazo la kushindwa vita wameamua kuyakataa matakwa ya Hamas kwenye mikutano yote ya usuluhishi na imeamua kuendelea na vita kwa kuivwamia Rafah hata baada ya kunasihiwa na dunia nzima kutotekeleza mpango huo.
Hata hivyo chochote itakachofanya Israel kwa sasa hakitaipatia ushindi katika vita hivi vinavyoelekea kumaliza mwezi wa saba sasa.Hiyo ni kwa vile pamoja na kwamba Hamas wengi wameuliwa lakini kuna askari wengi wa siri wameongezeka tena sio Gaza tu bali ulimwenguni kote.
Hamas inaungwa mkono na wanafunzi wa vyuo vikuu vingi Marekani na nchi nyengine.Zaidi ni kuwa imegundulika kuwa wanaoiunga mkono Palestina na kuwaunga mkono wanafunzi kuendelea na upinzani ni watu wa karibu na raisi Biden wa Marekani.
Chochote itakachofanya Israel eneo la Rafah kama ilivyotahadharishwa kutapelekea mauwaji makubwa na madhara yatakayochochea maandamano zaidi na kupelekea Israel kuelemewa na upinzani utakaifanya iache vita kwa kutaka au isitake.
Serikali ya Marekani pamoja na kuiunga mkono Israel kwa muda mrefu haitokubali upinzani dhidi ya Israel uharibu usalama na uchumi wa nchi hiyo zaidi na hasa katika kipindi cha uchaguzi unaokaribia.
Ikumbukwe Marekani tayari imekaribia kusalimu amri katika kuisaidia Ukraine na suala kubwa ni ukosefu wa pesa na silaha baada ya kutoa kwa muda mrefu huku kukiwa na matokeo hasi.
Israel ikikaribia kuingia Rafah rasmi na kwa nguvu kubwa imeamua kufungia kituo cha Aljazeera ili kuficha uhalifu utakaotokea huko.Hilo huenda lisisaidie kuzuia taarifa hizo kuufikia ulimwengu na kuongeza hamas za upinzani dhidi yake ambao tangu hapo uko juu sana.