Wanachuo wote waliowahi kusoma na wanaosoma UDSM tuandamane kwa kudhalilishwa kwa Dr. Shukuru Kawambwa

Nini kimetokea kwa huyo prof na ni prof gani?
 
Bila picha na video ni umbea
 
Hapo sawa nimepata picha
 
Kiukweli yule jamaa hakuwa na busara, nilihuzunika sana.
Profesa alionesha nini maana ya usomi na utu uzima.

Vp jamaa aliimaliza siku ile salama kweli? Tunaomba updates na wasifu wa yule jamaa.
Alikuwa anajiamini sana aysee
 
Nchi hii hatunaga wasomi,tuna waganga njaa tu.

We andamana kuelekea kwenu nyumbani ukatatue matatizo ya ukoo wenu.
Tz hii hii ya ccm.by the way.

Inaitwa mbwa wa mzee CHIKO ambwekea mtoto wa mzee CHIKO ambaye amekulia bording hivyo mbwa alikuwa hajamark harufu yake.
 
Mzuka wanajamvi!

Haiwezekani mzee profesa na aliyehodhi mamlaka na madaraka za juu nchini na kulitumikia taifa letu kwa weledi adhalilishwe na kijana mbele ya camera na kusukumwasukumwa.

Natoa rai kwa wanachuo wote waliosoma na wanaosoma UDSM kwa pamoja tukutane na tuandamane kupinga na kulaani udhalishaji huu kwa msomi profesa na mzee mwenye hekima na busara kurekodiwa na kuitwa dalali wa viwanja.

Vijana tuheshumuni mamlaka, wazee na wasomi wa taifa letu. Kitendo hiku cha professor kudhalilishwa kimelitia doa sana taifa.

Pia tuige mfano mzuri wa Professor alivyotulia bila kubishana na yule kijana mpuuzi.

Professor maintained his cool, local and international exposure and hundle the situation in a conducive manner. He clearly indulged and embarked in a critical anger management manoeuvre and manifesto.

What a character we should learn from this humble gentleman.

Siku mkimgusa Mwalimu wangu wa Kilimanjaro institute of technology mnitag
 
Manufaa yatakuwa nini baada ya kuandamana
1.Haki itendeke kwa prof siombwa kulipwa fidia ya udhalilishaji
2.Huyo mpemba afikishwe mahakamani na sheria ichukue mkondo wake
3.hayo machimbo ya mchanga yafungwe na vibali vifutwe kulinda mazingira
4.Njia haramu inayopita shambani kwa prof ifungwe na uharibifu uliotokea mhusika alipe gharama za ukarabati
5.itungwe sheria ya kulinda watu wenye heshima dhidi ya udhalilishaji,
 
Amepata alichostahili. Mimi nikiendaga Bagamoyo watu mbalimbali nimekuwa nawasikia wanamlalamikia Shukuru Kawambwa kuwanyang'anya maeneo yako ya ardhi. Lisemwalo lipo na kila uovu una mwisho mbaya.

Ili ujiridhishe na nachosema panga safari nenda Bagamoyo kata ya Kilomo (KITOPENI) waulize wakazi wa huko watakupa taarifa zake
 
Hapana huwezi mjambazia professor tena wasayansi sio tu sayansi engineer, lazima tuandamane na hili tutalifanya nchi nzima, na itungwe sheria ya kulinda watu wenye heshima.
Ina maana wananchi wengine hawastahili kuheshimiwa? Kila binadamu anastahili heshima. Walimu wako chuoni wamekupotosha. Fikiri kabla ya kusema.
 
Back
Top Bottom