KERO Wakazi wa Mbutu (Kigamboni, Dar) tuna changamoto kubwa ya Barabara, mamlaka ziko wapi?

  • Thread starter Anonymous (ae48)
  • Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest

Wakazi wa Mbutu Kigamboni tuna changamoto kubwa ya Barabara, mamlaka ziko wapi?
 
Mimi ni Mkazi wa Mbutu Kigamboni kwa namba ya Wanambutu, changamoto ya Mbutu, barabara ya kutoka Dege kwenda Mkwajuni mpaka kwenye machimbo ya vifusi ni hatari:

Kwanza naomba niwafahamishe yafuatayo;
1. Barabara zote za Kigamboni zitakazojengwa material yake nikimaanisha kifusi chake kitatoka Mbutu
2. Baadhi ya material ya ujenzi wa SGR yalitoka hapo.
3. Daraja la Tanzanite na yametoka kwetu.
4. Barabara ya Kimbiji material yametoka kwetu Mbutu.
5. Viwanda vya cement vinachukua materia kwetu.
6. Barabara zote na madaraja yaliyoharibiwa na hizi mvua wanategemea kifusi kutoka Mbutu

Jambo la kushangaza sisi ndio tuna Barabara mbovu kupindukia, tunajiona kama hatuna Mwakilishi wa kutusemea. Tumetelekezwa magari ya kifusi usiku kucha yanaharibu Barabara.

Picha/video:
7a9bbca5-4077-4988-bbd6-500a44dfa601.jpeg

baea2588-e6d9-443e-aa89-188ab7a14f50.jpeg

Maelezo ya Picha/Video: Hii ni barabara ya Mbutu, Block E

Tunaomba ujumbe huu uwafikie wengi hasa mamlaka za juu ili wafanye uamuzi wa kutusaidia.
 
Kuna ujenzi wa Barabara za lami unataka kuanza kwq dege mbutu Kilometa 1.6 pia barabara ya atani dege kilometa 1.7.
 
Kwani kuna mtu aliwalazimisha kukaa huko? ama umasikini wenu tu na kutofikiria, wenzenu wenye akili wanatengeneza miundombinu kwanza kabla ya kuuziana maeneo sasa kwa utaratibu huo mnamlaumu nani? Pambaneni na hali zenu.
 
Back
Top Bottom