Wakati unakua, nini kwenu mlikuwa mnatoaga nje asubuhi na kukirudisha ndani jioni muda wa kufunga mlango kabla ya kulala?

Kwetu bwana , kulikuwaga na pikipiki ya babu, miaka hiyo mzee alishindwa kulitengeneza, likawa limekaa tu, sasa linalazwa ukumbini.

Asubuhi mnaamka nalo kulitoa kwanza liwapishe, jioni ndo kitu cha mwisho kuingizwa, hata kama umelala bahati mbaya mzee atakuamsha ukaingize piki piki yenu.

Basi ilinikera kwelikweli haha haaa!

Vipi wewe
Mi nilikua naliwasha natest mpaka siku ya mwisho likamuua mzee nimewasha mimi ilikua Honda Paris Dakar.
 
Ninachokumbuka godoro langu lilijua kunitesa toka nianze kuwa na akili mpaka darasa la sita ila Mungu mwema darasa la Saba nikapumzika ikawa kazi ya matron mpaka kidato cha pili.
 
Kibuyu fulani hivi kikubwa kimekarwa kwa juu mdomo, kinatumika kukojolea, asubuhi kutoa nje ni zamu na kuingiza ndani ni zamu. Sasa amka na wenge lako ukibebe vibaya kikuponyoke kijipige ardhini ndani ndo utajua kwanini uliwekewa kichwa juu ya shingo
 
Aisee mimi sitasahau mtiti wa kumtoa Mzee kikongwe nje kumuanika na kumrudisha ndina kila atakapo nilikonda sana kipindi hicho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom