Wakati unakua, nini kwenu mlikuwa mnatoaga nje asubuhi na kukirudisha ndani jioni muda wa kufunga mlango kabla ya kulala?

mweki

Member
Nov 8, 2014
6
16
Kwetu bwana , kulikuwaga na pikipiki ya babu, miaka hiyo mzee alishindwa kulitengeneza, likawa limekaa tu, sasa linalazwa ukumbini.

Asubuhi mnaamka nalo kulitoa kwanza liwapishe, jioni ndo kitu cha mwisho kuingizwa, hata kama umelala bahati mbaya mzee atakuamsha ukaingize piki piki yenu.

Basi ilinikera kwelikweli haha haaa!

Vipi wewe
 
Huku kwetu bwana, nyumba zetu hizi katika hali ya kawaida, ndani ya nyumba mnaingia watu, kuku na vitoto vya mbuzi. Nje limewekwa sanzu zito kuzunguka nyumba/makazi yote (Uzio wa miiba na miti aka boma). Kwenye boma huko nje wanalala ng'ombe, punda na mbuzi wakubwa kunakuwepo na kaboma kadogo ndani ya boma kubwa kwa ajili ya ndama ili kuwazuia wasinyonye usiku.
Asubuhi kunapokucha tu, majira ya saa 11-12 asbh, lazima uamke tu (taka usitake) ili kuvitoa nje au kuruhusu vitoto vya mbuzi na kuku vitoke nje kunyonya na kuku wakaokoteze(kubangaiza)kwani huko nje mama zao wanaita kwa sauti kubwa mfululizo (hakukaliki) na ndani vitoto vinaitikia mtindo mmoja. Lazima asbh. uamke uvitoe nje na jioni unawarudisha kwa utaratibu huo huo ili ili asbh. kesho tena ngoma ianze. Inachosha sana hasa ukizingatia ukija likizo (shule za bweni) unategemea kulala walau kupitiliza kidogo kwani shuleni huko tuliamshwa kwa nguvu na kaka wa shule. Sasa tena hapa ni vitoto vya mbuzi (N'dare/mbalelo) na kuku (Ormotonyii).
Inasumbua sana ila hatuna jinsi inabidi tukubaliane na hali.:Cheergi:
 
Kwetu bwana , kulikuwaga na pikipiki ya babu, miaka hiyo mzee alishindwa kulitengeneza, likawa limekaa tu, sasa linalazwa ukumbini.

Asubuhi mnaamka nalo kulitoa kwanza liwapishe, jioni ndo kitu cha mwisho kuingizwa, hata kama umelala bahati mbaya mzee atakuamsha ukaingize piki piki yenu.

Basi ilinikera kwelikweli haha haaa!

Vipi wewe
Godoro, ilikua lazima usiku liloane halafu asubuhi linatolewa nje kuanikwa, jioni ndiyo linaingizwa ndani.
Kama kweli hujipendi, jaribu kuniamini ujione ulivyo fala.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom