Waafrika tuna uwezo mdogo wa kujiongoza kimaendeleo, Naomba unitajie nchi moja tu ya kiafrika inayoendeshwa na waafrika iliyo stable?

Mtoto wa masikini Kenya anaenda kwenye shule bora za umma kuliko Tanzania, Kenya fursa za ajira nzuri tofauti ni nyingi ndani ya nchi hadi nje ya nchi kutuzidi,
Wafanya biashara ndogo ndogo wanafanya bishara zao katika mazingira mazuri kuliko Tz, muuza mboga barabarani wa Kenya ana unafuu mkubwa wa maisha ukilinganisha na wa Tanzania
Kenya ni nchi ya pili kwa kuwa na makazi na watu wengi wenye umasikini wa kupindukia barani Africa baada ya Nigeria.
 
Umaskini wa kupindukia unapimwaje?
Nchi yenye uchumi mzuri haiwezi kuwa na makazi duni mengi kiasi hichi .
Uchumi wa kenya upo mikononi mwa familia za wana siasa.
 

Attachments

  • Screenshot_20240209-225430.png
    Screenshot_20240209-225430.png
    853.4 KB · Views: 5
Watu wameachana na mada na sasa wanajadili utofauti wa Kenya na Tanzania kimaendeleo. Ukweli ni kwamba nchi haziwezi kufanana kwani kila nchi duniani ina mema na mabaya yake.

There is no Eutopian country on earth.
 
Labda kama Kuna Kenya nyingine tofauti na hii niliyoishi. Kenya na Tz hazitofautiani sana kimaendeleo.
Labda nipost picha tu nikuonyeshe kuwa Kenya Wana matatizo kama sisi tu. Nairobi city inadecay Kila kukicha. Na hapo less a kilometer kutoka Kenya administration offices
dji_mimo_20240412_163930_0_1712958525521_photo.jpg
PXL_20240411_145129488.jpg
PXL_20240411_142745274.NIGHT.jpg
PXL_20240410_144357589.MP.jpg
 
Kiuchumi na Elimu hawa jamaa wametupita ila walichokosa ni undugu wa kuweza kuishi pamoja, Ukabila unawasumbua sana, hawana umoja, Kenya ni ya watu wa makabila flani ukiwa kabila tofauti maisha ni magumu.

Kuhusu suala la pesa kuikidhi mahitaji inategemeana na malipo, Hata Marekani na nchi za ulaya kodi ya chumba ni dola 700 takribani shilingi milioni 1 na nusu lakini malipo ya kazi mtu analipwa kima cha chini ni elf 18 kwa saa hizo ni kazi za kuosha vyombo, kusafisha meza za kula, n.k.

Na huko Kenya mishahara ipo juu kuzidi Tz ndio maana Kenya maisha yapo juu kwa Mtanzania

Pia Kenya wameanza kuwa wajanja mapema kuzidi Tz, kumbuka hao hata mambo ya Tv wameyjua tangu 1960s tofauti na sisi tumeanza 1990s, Kenya ndio nchi yenye wanadiaspora wengi zaidi kwa hapa Africa mashariki wamejaa zaidi huko Marekani na ulaya, Kenya ndio main exporters wa bidhaa za Tanzania ikiwemo maparachichi, n.k.
Uko sahihi.
Viwanda mama vingi vina matawi yake Kenya.
Mshahara wa barmaid Kenya ni karibia 200000Tsh wakati Tanzania ni 50000Tsh.
Kwa hilo sikukatalii.
 
Tatizo sio kabila tatizo ni umaskini. Kua na hela uone kama hutawaajiri hao unaoita wabaguzi
Kenya walitakiwa kuwa juu zaidi ,nimeishi kenya maana pia nimekaa mpakani.

Kenya wana maendeleo ila sio nchi nzuri ...Kenya kuna ubaguzi wa wazi ndugu yangu kuna makabila ukizaliwa basi una nuksi mazima hata furaa hupati usiwe mkamba ,mkisii ,wakale
 
Umewahi kuona omba omba Kenya wanaozunguka barabarani kama hapa Tanzania?
Umewahi kuona nyumba za tembe zilizoezekwa kwa majani Kenya?
Mtu anayejenga nyumba ya mabati na anayejenga nyumba ya tembe(udongo) iliyoezekwa kwa makuti nani anaweza kuwa masikini zaidi?
Raia wa Tanzania ambaye hana ajira ila anaishi kwa vizinga unataka kusema ni bora kuliko wa Kenya anayetapeli?
Umewahi kuona raia ambao kazinyao ni waokota makopo/chupa za maji Kenya?
Gharama za maisha Marekani ziko juu kuliko Tanzania, huko USA huwezi kupata wali nyama $1 lakini hiyo haimaanishi kwamba Tanzania maisha ni mazuri kuliko Marekani, unachotakiwa kufahamu ni kwamba uwezekano wa kupata pesa nyingi Kenya au Marekani ni mkubwa zaidi kuliko Tanzania kwa sababu fursa ni nyingi na mzunguko wa pesa ni mkubwa zaidi.
Ukiona mahali kuna ombaomba na wanaendelea kuwepo jua ya kwamba hapo mahali kuna mzunguko wa pesa ndio maana watu hawaoni shida kutoa pesa kuwapa ombaomba vinginevyo kama hakuna watu wa kujitolea pesa huwezi kuwaona hao ombaomba hata kidogo maana hawatopata kitu
 
Nimeishi kenya na kukaa mpakani sehemu inaitwa Daluni ,kule ukabila ni hatari sio nchi ya kukaaa .kabisa kama umezoea Tanzania .


Kenya ni ovyo kabisa haswa unakuta mtu anapewa huduma kwa kuitwa jina la kabila "utasikia huyu mkikuyu"

Labda Mombasa na Nairobi ila kaunti zilizobaki ni chefu.
Kwa hiyo tanzania tunapowaita Wamasai siyo ukabila?
 
Kenya hamna diversity kubwa makabila machache ndio tatizo ...Tanzania makabila kibao , narudia Tz ina mikao miwili yenye ubaguzi basi sasa nenda kenya kila jimbo lina sheria zake usije kushangaa
Mikoa ipi ina ubaguzi Tanzania?
 
Ukiona mahali kuna ombaomba na wanaendelea kuwepo jua ya kwamba hapo mahali kuna mzunguko wa pesa ndio maana watu hawaoni shida kutoa pesa kuwapa ombaomba vinginevyo kama hakuna watu wa kujitolea pesa huwezi kuwaona hao ombaomba hata kidogo maana hawatopata kitu
Dodoma haina mzunguko mkubwa wa pesa kuliko Nairobi
 
Back
Top Bottom