Waafrika tuna uwezo mdogo wa kujiongoza kimaendeleo, Naomba unitajie nchi moja tu ya kiafrika inayoendeshwa na waafrika iliyo stable?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,095
Nigeria - uchumi mzuri ila kuna ukabila wa hali ya juu sana kila siku biashara na nyumba za wa igbo zinabomolewa na kuchomwa bila notice ama notice ya masaa mawili, kuna makundi yenye itikadi kali za kiisalam za kuua wakristo, n.k.

South Africa - Asilimia 85 ya ardhi bado inamilikiwa na makaburu na wazungu, uchumi nao asilimia kubwa ni hao hao, wafrika wapo wengi kwa idadi tu

Haiti - Hawa walikuwa wa kwanza kupata uhuru kuzidi Dominika majirani zao lakini leo hii Dominica ni kama ulaya, Haiti ni kama uswazi

Kenya - Ukabila upo Rais ni aidha awe mkikuyu ama mkalenjini, FULLSTOP !! hata kwenye vyeo na makazini hayo ndio makabila yanayopewa uzito zaidi, Wakenya wana uchumi mzuri kuzidi hata Tanzania yenye resources kibao lakini ukabila unawapasua vipande

Rwanda - Kagame ni Dictator hataki ushindani kabisa, wahutu ni takribani asilimia 85 ya idadi ya warwanda lakini watutsi ambao ni talribani asilimia 10 tu ndio wana vyeo vingi vya juu na ajira kwenye taasisi za juu kuzidi wahutu

Ghana - nchi hii ya kwanza Afrika kupata uhuru angalau ina maendeleo japo haifikii Nigeria na Sauzi lakini bado wanasumbuliwa na ufisado, wapo nyuma kwenye miundombinu, upatikanaji wa maji, huduma za serikali, , bado kuna shule watoto wanakaa chini, n.k.

BOTSWANA - Tuwape muda wana uelekeo mzuri, wana maendeleo ya kati lakini wanakuja kwa speed kali, ndani ya miaka 40 wanaweza kuwa pearl of Africa,
  • Wanajitahidi sana kudhibiti ufisadi na kuwashughulikia mafsiadi
  • watumishi wa serikali wanaowajibika
  • hakuna ukabila
  • kuna amani
  • misaada ya nje wanaendeleza huduma za kijamii sio upigaji
  • mikopo wanawekeza na kuexport rasilimali wapate mapato na kufuta madeni
  • mapato yanawekezwa kwenye kukuza huduma za kijamii bila ufisadi
 
Nigeria - uchumi mzuri ila kuna ukabila wa hali ya juu sana kila siku biashara na nyumba za wa igbo zinabomolewa na kuchomwa bila notice ama notice ya masaa mawili, kuna makundi yenye itikadi kali za kiisalam za kuua wakristo, n.k.

South Africa - Asilimia 85 ya ardhi bado inamilikiwa na makaburu na wazungu, uchumi nao asilimia kubwa ni hao hao, wafrika wapo wengi kwa idadi tu

Haiti - Hawa walikuwa wa kwanza kupata uhuru kuzidi Dominika majirani zao lakini leo hii Dominica ni kama ulaya, Haiti ni kama uswazi
Botswana
 
Botswana, Kenya
Kenya walitakiwa kuwa juu zaidi ,nimeishi kenya maana pia nimekaa mpakani.

Kenya wana maendeleo ila sio nchi nzuri ...Kenya kuna ubaguzi wa wazi ndugu yangu kuna makabila ukizaliwa basi una nuksi mazima hata furaa hupati usiwe mkamba ,mkisii ,wakale
 
Kenya ipo stable? Hivi Kenya ina tofauti gani na Tanzania kimaendeleo?
Kenya wangekuwa mbali sema ukabila wa wazi wazi ,miji mingi wamejenga ila bado wanasumbuliwa na ujinga wa ubaguzi .

Ile 2007 walipigana kuonyesha ni watu wa ovyo.
 
Kenya wangekuwa mbali sema ukabila wa wazi wazi ,miji mingi wamejenga ila bado wanasumbuliwa na ujinga wa ubaguzi .

Ile 2007 walipigana kuonyesha ni watu wa ovyo.
Wako mbali kutuzidi, ubaguzi uko kila sehemu duniani wanasiasa wanapoona kuna fursa ya kuutumia hufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom