SoC04 Vita dhidi ya Ujinga: Elimu kombozi kwa maendeleo ya jamii

Tanzania Tuitakayo competition threads

Jerry Farms

Member
Jul 18, 2022
59
41
Ni nyumbani kwa mzee Masalu! Ubishi mkali unatokea kati ya mzee Masalu na kijana wake ambaye hataki Shule. Hataki shule kwa madai ya kua haoni mwanga mbele!

Hali hii imeanza kuota mizizi katika jamaa nyingi za kitanzania, wazazi na vijana wameanza kuwa na wasiwasi na shaka juu ya dhana nzima ya usomi! Hapa madai yamekua ni je kijana akisoma ana "connection", ndugu, hongo ama anamjua nani atakaemuunganisha na ajira!

Kwa umbali kuna ka ukweli kiasi chake! Hemu tutazame ripoti ya hali ya ajira na rushwa Tanzania! Ni masikitiko, lakini yote haya ni matokeo ya; mtazamo hasi juu ya usomi, rushwa na mfumo wa elimu tegemezi.

Ni kweli wasomi wengi wako mtaani, hata dhana ya elimu ya ujuzi haina nguvu sana kama mwelimishwaji hana nyenzo zingine wezeshi kuyakabili mazingira baada ya kuhitimu elimu tajwa( rasilimali fedha,ardhi nakadhalika. Ujuzi pasipo na fedha na rasilimali zinginezo ni upotevu wa muda!

Je lawama kwa serikali ndilo jibu? Hapana, hapana...hapana kubwa. Ila ni MABADILIKO tu ndiyo yatakayo tuondoa katika hali hii. Je ni mabadiliko yepi?

Uhakiki wa maudhui ya Elimu inayotolewa kwa jamii.
Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na wataalamu wa kisekta toka kada mbali mbali Kubuni programu ya maktaba za kielekloniki zitakaweza kufikiwa na jamii kupitia simu janja.Katika maktaba hizi maudhui yote yatakayowekwa yawe yamehakikiwa na wataalamu ili kuepusha upotoshwaji wa elimu.

Kwa kuzingatia hali ilivyo sasa sio kila elimu ni elimu kweli kweli! Katika mitandao taarifa nyingi zimekua zikipakiwa zikiwa zimechanganyikana taarifa sahihi na taarifa za upotoshaji. Jamii ikiichwa ikala taatifa hizi pasi na udhibiti kuna hatari ya kuwa na jamii iliyoelimika kwa maarifa yasiyo sahihi hivyo changamoto ya ujinga.
•Wizara ya elimu, iwajibike kupokea maudhui na kuyahakiki kisha kuyaingiza katika maktaba yake ya kielektroniki.

•Umma ujulishwe juu ya uwepo wa maktaba hii, Umma ukae ukijua kua ili kupata taarifa sahihi/elimu sahihi waingie kwenye mfumo rasmi wa maktaba iliyochini ya udhibiti wa wizara ya elimu na kuelimika juu ya jambo walitakalo kwa usahihi.

Elimu inayolenga kutatua changamoto za kimazingira.
Mashamba darasa ya kilimo na ufugaji kuanzia darasa la tatu, vikarakana katika shule za msingi( elimu kwa wahitimu wa darasa la saba kabla ya kujiunga sekondari) n.k Samaki mkunje angali mbichi! Ni nahau ya zamani yenye maana kubwa na hapa ina enea kwa usahihi.

Elimu inayoendana na mahitaji yaliyopo katika jamii.
Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini shule itoe fomu 100 za kujiunga nayo alhali ina nafasi 40 tu! Hiki ndicho kinachofanyika na vyuo mbali mbali. Vyuo vinatakwimu ya mahitaji ya wataalamu katika jamii namba XXX lakini kinadahili wanafunzi mamia kwa maelfu katika fani husika! Ni kichekesho lakini si afya kwa jamii. Sasa imefika wakati kwa taasisi za kielimu zikishilikiana na wizara ya elimu kufanya tafiti na kuja na data kamili zinazoonesha ni fani zipi zinazohitajika katika jamii na hivyo kuwekeza nguvu kubwa huko. Itaghalimu nini kusitisha kwa muda kutoa kozi XYZ kama wasomi wa fani hio wamejaa mtaani na kuwekeza nguvu kubwa katika fani TTX. Ni hesabu ndogo tu lakini tatizo ni elimu kutoka katika huduma mpaka biashara. Msingi wa utoaji wa elimu urejewe sasa.

Vita juu ya rushwa katika taasisi za elimu.
Watumishi waaminifu wameisha mtaani? Kwa nini tatizo la rushwa haliishi basi? Vyombo vya utoaji haki havina budi kuja na mpango kabambe wa kupambana na rushwa katika nyanja mbali mbali. Vyombo vya utungaji sheria vije na sheria kali zaidi na uwajibishwaji uanzie ngazi ya chini, ikiwezekana mbadhirifu asiishie kufukuzwa kazi bali mali zake binafsi kutaifishwa na kukatwa mafao yake baada ya kustaafishwa. Sheria zitungwe na ziwe kali zaidi hata kwa wale wanaopitisha mirandi inayokuja kubadirika kuja kuwa mizigo kwa walipa kodi...mpitishaji wa mradi basi aji "commit" kuwa tayari kushtakiwa pindi mradi husika utakapo enda mrama au apewe pongezi pindi mradi ukienda sawa.

Elimu pamoja na rasilimali wezeshi
Tumekupa ujuzi haya kajiajiri! Ni maneno anayopewa kijana asiye na hata senti 100 mfukoni alietumia miezi sita akisoma kozi ABC! Inatafakarisha kidogo. Ni muda sasa kwa halmashauri kuwaatamia wahitimu wa fani mbali mbali katika halmashauri zao. Baada ya elimu ya ujuzi wa kwa mhitimu kuwepo na mfumo wezeshi ambapo wataalamu( waajiliwa) kupewa vikundi vikundi kuvisimamia katika mradi husika. Mfano vijana wamepewa elimu ya kilimo, basi bwana/bibi shamba apewe kikundi hiko akisimamie na kilete matokeo. Hapa halmashauri hazina budi kutenga maeneo ya kijasiliamali kwa ajili ya kuatamia wasomi kutoka katika maeneo yao. Kila halmashauri itakaguliwa na kupewa hati kulingana na utendaji wake.

Uzalendo na utashi wa moyoni kwa viongozi
Hapa rejea taarifa za mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG)...uzalendo hauletwi kwa kuimbwa majukwaani...uzalendo ni vitendo. Imani bila matendo Imekufa( Yakobo 2:1 nakuendelea). Uzalendo hauwezi kuingizwa katika mioyo ya wananchi kama kila siku wanaskia ubadhirifu unaendelea kwa kasi ya 5G!

Mabadiriko ya kimtazamo kwa wazazi na wasomi wa baadae.
Kusoma ili kuja kuajiliwa ni kujidanganya! Ajira ni chache wasomi ni wengi. Ni wajibu wa mzazi na mtoto kuwekeza katika elimu inayolenga uzalishaji mali na si kukariri maendeleo ya mataifa ya nje! Elimu ya Marekani ilipata uhuru mwaka gani? Au waziri wa kwanza wa Burundi aliitwa nani? Ama kilimo cha mpira Brazili nakadharika havina nafasi katika karne hii. Historia sio mbaya, lakini isichukue asilimia 90 ya masomo. Mwanafunzi ajifunze yale tu yanayoweza kumsaidia,mfano kwa kuangalia mazingira ya Tanzania ni kipi kinaweza kufanywa. Kama ni historia ya kilimo basi wanafunzi wafundishwe kilimo kwa vitendo( kilimo cha mahindi, mpunga, mkonge au uchimbaji wa madini n.k basi waingie katika uhalisia...Elimu ya makaratasi n hatari kwa taifa letu.

HITIMISHO
Ni muda muafaka sasa kwa wazazi, walezi, taasisi za kielimu na wizara husika kuja na mfumo wa elimu unaoendana na mahitaji ya jamii husika. Wizara mbalimbali kwa kupitia fedha tengwa kwa ajili ya maendeleo zianzishe programu ya ufundishaji wa ujuzi unahitajika katika jamii husika, hamasa kubwa ifanywe kuwapata wananchi wa maeneo husika na kuwapatia elimu kombozi. Hapa tunamaanisha kama ni jamii ya watu wanaojihusisha na ufugaji, wizara ya kilimo iwekeze katika elimu ya ufugaji katika eneo hilo, kama ni jamii ya wachimbaji basi elimu ya uchimbaji itolewe huko, kama ni uvuvi ama utalii vivyo hiyo elimu iende sambamba na mahitaji ya eneo husika. Kila eneo lina uhitaji wa ujuzi unaoendana na shughuli kuu zifanyikazo kwayo, mabadiriko ya kimafunzo ni sasa.
 
Umma ujulishwe juu ya uwepo wa maktaba hii, Umma ukae ukijua kua ili kupata taarifa sahihi/elimu sahihi waingie kwenye mfumo rasmi wa maktaba iliyochini ya udhibiti wa wizara ya elimu na kuelimika juu ya jambo walitakalo kwa usahihi.
Yas ujulishwe na uhamasishwe pia. Udadisi ukuzwe tangu watu wakiwa wadogo. Maana wadadisi ndio watakaotumia hizo maktaba na UDADISI NDO AKILI.

Elimu inayoendana na mahitaji yaliyopo katika jamii.
Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini shule itoe fomu 100 za kujiunga nayo alhali ina nafasi 40 tu! Hiki ndicho kinachofanyika na vyuo mbali mbali. Vyuo vinatakwimu ya mahitaji ya wataalamu katika jamii namba XXX lakini kinadahili wanafunzi mamia kwa maelfu katika fani husika! Ni kichekesho lakini si afya kwa jamii. Sasa imefika wakati kwa taasisi za kielimu zikishilikiana na wizara ya elimu kufanya tafiti na kuja na data kamili zinazoonesha ni fani zipi zinazohitajika katika jamii na hivyo kuwekeza nguvu kubwa huko. Itaghalimu nini kusitisha kwa muda kutoa kozi XYZ kama wasomi wa fani hio wamejaa mtaani na kuwekeza nguvu kubwa katika fani TTX
Sure thing, soko ndio liamue tunazalisha kipi bas.

mpitishaji wa mradi basi aji "commit" kuwa tayari kushtakiwa pindi mradi husika utakapo enda mrama au apewe pongezi pindi mradi ukienda sawa
Hahahaaah, kwamba iwe haki, mradi ukifanikiwa apewe zawadi na mradi ukifeli apewe adhabu. Itaongeza uwajibikaji. Viwe tu vya haki hivyo vitu.

Ni wajibu wa mzazi na mtoto kuwekeza katika elimu inayolenga uzalishaji mali na si kukariri maendeleo ya mataifa ya nje! Elimu ya Marekani ilipata uhuru mwaka gani? Au waziri wa kwanza wa Burundi aliitwa nani? Ama kilimo cha mpira Brazili nakadharika havina nafasi katika karne hii. Historia sio mbaya, lakini isichukue asilimia 90 ya masomo. Mwanafunzi ajifunze yale tu yanayoweza kumsaidia,mfano kwa kuangalia mazingira ya Tanzania ni kipi kinaweza kufanywa. Kama ni historia ya kilimo basi wanafunzi wafundishwe kilimo kwa vitendo( kilimo cha mahindi, mpunga, mkonge au uchimbaji wa madini n.k basi waingie katika uhalisia.
Kwenye suala la kuondoa baadhi ya vitu kwenye elimu tusikurupuke. Labda kama hizo elimu zitamzuia (muda) kujifunza hayo mengine ya uzalishaji. Kiongozi aliyesoma historia ya kilimo cha matunda Israeli ana nafasi nzuri ya kutumia masomo kuelekeza watu wake katika kilimo cha matunda Njombe. Elimu isiminye tu uwanda wa mjifunzaji kujitanua kadri muda unavyomruhusu.

Ni muda muafaka sasa kwa wazazi, walezi, taasisi za kielimu na wizara husika kuja na mfumo wa elimu unaoendana na mahitaji ya jamii husika. Wizara mbalimbali kwa kupitia fedha tengwa kwa ajili ya maendeleo zianzishe programu ya ufundishaji wa ujuzi unahitajika katika jamii husika, hamasa kubwa ifanywe kuwapata wananchi wa maeneo husika na kuwapatia elimu kombozi.
Umenena vema
 
Yas ujulishwe na uhamasishwe pia. Udadisi ukuzwe tangu watu wakiwa wadogo. Maana wadadisi ndio watakaotumia hizo maktaba na UDADISI NDO AKILI.


Sure thing, soko ndio loamue tunazalisha kipi bas.


Hahahaaah, kwamba iwe haki, mradi ukifanikiwa apewe zawadi na mradi ukifeli apewe adhabu. Itaongeza uwajibikaji. Viwe tu vya haki hivyo vitu.


Kwenye suala la kuondoa baadhi ya vitu kwenye elimu tusikurupuke. Labda kama hizobelimu zitamzuia (muda) kujifunza hayo mengine ya uzalishaji. Kiongozi aliyesoma historia ya kilimo cha matunda Israeli ana nafasi nzuri ya kutumia masomo kuelekeza watu wake katika kilimo cha matunda Njombe. Elimu isiminye tu uwanda wa mjifunzaji kujitanua kadri muda unavyomruhusu.


Umenena vema
Shukrani saana....bila uthibiti wa maarifa tutaangamiza taifa. Tunaweza kuwa na wasomi wenye elimu potoshi.
 
Back
Top Bottom