Neema ya BWANA
Member
- Jun 25, 2023
- 45
- 31
Utangulizi
Zipo teknolojia nyingi sana ambazo ni kama zimetupita barani Afrika hususan nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Taifa la Tanzania. Katika teknolojia hizi zilizotupita kidogo, ipo teknolojia ya kifaa cha ajabu ambayo hatupaswi tuendelee kuiacha itupite, na kifaa hiki si kingine bali ni simu. Ndiyo, ni Teknolojia ya Simu; simu yako hiihii unayotumia kusomea andiko hili au pengine unayotumia kuwasiliana na uwapendao.
(Chanzo Picha: Global TV)
View: https://youtu.be/o9Mq7PYUjT0?si=dqGLkbmKdalgzyWQ
Simu ni kifaa cha ajabu, kilichobeba teknolojia mbalimbali kwa wakati mmoja, hivyo kuifanya uhitaji wake kuwa mkubwa zaidi kuliko teknolojia yoyote ile duniani. Hapa nazungumzia simu janja, ambayo mwanadamu yeyote anapoikosa anakuwa kama aliye gizani nyuma ya dunia, kwani yapo mambo mengi atashindwa kufanya.
Wapo watu mbalimbali mitandaoni ambao wamekuwa wakiwasilisha changamoto zao ili waweze kusaidiwa mfano mitaji ya biashara na mahitaji mengine muhimu, lakini cha ajabu baadhi yao huishia kuambiwa: "si uuze hiyo simu ukatatue changamoto yako?"
Ukweli wa mambo ni kwamba, inawezekana kabisa kuwa simu ina thamani kwa mmiliki kuliko kiasi kadhaa cha fedha, kwani simu inapotumika vizuri kwa njia halali, inaweza kumsaidia mmiliki kuingiza kipato kizuri sana kwa siku nyingi na kwa muda mrefu.
Kama kuna biashara na uwekezaji muhimu zaidi unatakiwa kuanzishwa nchini Tanzania ili kuwa Tanzania Tuitakayo; basi ni VIWANDA VYA UTENGENEZAJI NA UZALISHAJI SIMU; lakini kutokana na hali ya bara letu la Afrika kuwa changa katika teknolojia ya simu; ili tutengeneze simu zenye kiwango na ubora wa hali ya juu, inatupasa viwanda hivi vigawanywe katika makundi matatu ambayo ni:-

- Viwanda vya hatua ya mwanzo kabisa yaani viwanda vya utengenezaji wa malighafi ngumu (hard raw materials) za simu kama vile nyaya, vioo, majalada, haptic engines, uchakataji wa madini simu kama vile copper, zink, gold, n.k. (mobile hardwares)
- Viwanda vya hatua ya kati vya utengenezaji wa malighafi tepe (soft raw materials) za simu kama vile softwares, language programs, font style designing, camera programs, n.k. (mobile softwares)
- Viwanda vya hatua ya mwisho ya utengenezaji simu ambavyo vinahusika na Mawazo ya Ubunifu (Idea), Utengenezaji Taswira (Imaging and Sketching), Uthibitishaji wa Michoro (Sketch Proof), Uumbaji Michoro (Physical Product Sampling), Majaribio (Physical Product Test) na Uundaji wa Simu mpaka iingie sokoni. (Manufacturers)
Kwanini viwanda vya utengenezaji na uzalishaji simu ni muhimu kwa TANZANIA TUITAKAYO?
Kwanza, simu ni chombo cha mawasiliano ambacho kinaunganisha dunia. Mataifa na Makampuni makubwa duniani, yanahusika sana na utengenezaji na uzalishaji wa simu au viambata vya simu; mfano Microsoft na Apple. Lakini pia mataifa makubwa yaliyoendelea, yanajihusisha sana na Masuala ya Vyombo vya Mawasiliano; Japan (Sony), Korea Kusini (Samsung na LG), Marekani (Microsoft, Apple, Motorola na Google Pixel), Finland (Nokia), Ujerumani (Siemens), China (Huawei, Infinix, Vivo, Oppo na Tekno), n.k.
(Chanzo Picha: Freepik)
Pili, simu ni maktaba na album nzuri ya uhifadhi wa matukio, kumbukumbu, picha, nyaraka, sauti, n.k. Kwa kutumia simu, tunaweza kuhifadhi nyimbo, vitabu, picha, na kumbukumbu nzuri; za kwetu na tuwapendao.
(Chanzo Picha: Guiding Tech)
Tatu, simu ni mkusanyiko wa idhaa mbalimbali; redio, television, magazeti, n.k., ambayo hutuwezesha kupata habari kwa wakati kutoka duniani kote. Simu huweza kufanya kazi kama chombo cha habari.
(Chanzo Picha: Slash Gear)
Nne, simu huchukua nafasi ya kompyuta. Kutokana na wepesi na urahisi wa kubeba, kuishika pamoja na uwezo wake makubwa wa kuhimili teknolojia mbalimbali, simu imechukua nafasi kubwa ya kazi za kompyuta mfano uandishi (typing) wa nyaraka kwa njia ya simu ni rahisi kuliko uandishi kwa njia ya kompyuta, vilevile usomaji wa nyaraka kwa njia ya simu ni rahisi kuliko usomaji wa nyaraka kwa njia ya kompyuta; kwani simu zinatuwezesha kusoma au kuandika nyaraka wakati wowote mahali popote.
(Chanzo Picha: Coin Market Cap)
Tano, simu huchukua nafasi ya mashine mbalimbali kama vile scan machine. Hii ni kwasababu, simu inayo uwezo wa kuhifadhi programu mbalimbali zikiwemo programu zenye uwezo wa kuscan nyaraka na kuileta kwenye format ya PDF.
(Chanzo Picha: Bruceb Consulting)
Sita, simu inachukua nafasi ya taa. Mara paap! Umeme unapokatika, kifaa cha kwanza ambacho wengi huwa tunakikimbilia ni simu, ili kuwasha tochi na tuweze kupata mwanga (nuru)
(Chanzo Picha: MOSAIC Lille)
Saba, simu huweza kutumika kama dira ya kumwongoza mgeni katika eneo husika. Hii, ni pale ambapo mgeni anaamua kuitumia ramani (map) kwenye simu yake ili iweze kumwonesha mahali anapokwenda.
(Chanzo Picha: Dreams Time)
Nane, simu inachukua nafasi ya saa na kalenda. Miaka ya nyuma, saa na kalenda zilikuwa zinatumika kweli kwa ajili ya kuonesha muda, siku, mwezi na mwaka, tofauti na miaka ya sasa ambapo saa na kalenda zimebaki kuwa urembo wa mkono au pambo la ukuta kwa wengi, kwani asilimia kubwa ya watu hutumia simu zao kusoma saa, siku, mwezi na mmwaka.
(Chanzo Picha: Scott Stein, CNET)
Tisa, simu ni kifikishi cha watu kwenye teknolojia. Dunia ya sasa ambayo imezungukwa na teknolojia mbalimbali kama vile mitandao ya kijamii, platforms na forums mbalimbali ikiwemo Jamii Forums, zinahitaji simu yaani simu janja ili tuweze kuzifikia.
(Chanzo Picha: Alamy)
Kumi, simu ni kichapuzo kizuri cha talanta na vipaji, kwani kupitia simu tunaweza kukuza vipaji vya uandishi, uchoraji, muziki, uigizaji na uzungumzaji au usimulizi kwa hadhira.
(Chanzo Picha: Walmart)
Kumi na Moja, simu huweza kutumika kama chombo cha miamala na benki ya kuhifadhia fedha, kwa kutumia Mobile Money Apps, fedha mtandao, Huduma za kifedha za taasisi za fedha na mitandao ya simu.
(Chanzo Picha: Concept Phones)
Kumi na Mbili, kamera za simu huweza kutumika katika huduma mbalimbali iwapo itakuwa kamera ya kawaida, kamera ya CCTV au Kamera ya Thermal. Huduma hizi huweza kuwa za afya, ulinzi, usalama, n.k.
(Chanzo Picha: Atlantis Blog - Atlantis Worldwide)
(Chanzo Picha: Medical News Today)
(Chanzo Picha: Black View)
Hitimisho
Hivyo basi, uwekezaji wa VIWANDA VYA UZALISHAJI NA UTENGENEZAJI SIMU ni muhimu kwa Taifa la Tanzania ili iweze kuwa Tanzania Tuitakayo; Tanzania yenye ajira nyingi kwa wenyeji na wageni, Tanzania ya Mapinduzi Makubwa ya Viwanda na Tanzania yenye uchumi imara barani Afrika na duniani kote.
Mpendwa msomaji, tafadhali naomba uniorodheshee faida na kazi nyingine za simu janja, ambazo sijaziorodhesha katika andiko hili ili tujifunze pamoja.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.