Utofauti kati ya kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye ubongo(Brain) na kumbukumbu zinazohifadhiwa na akili (Mind)

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,757
107,107
MATE;
Previous I wrote a topic centered on Illusion projection and I discussed a bit about how the brain process and encode memory, So this Topic will be serving as a stand-alone sequel of that Topic. Will be focusing on memory stored in brain and Soul respectively.

Kuna hivi vitu viwili tunaweza kua tunavichanganya pindi tunapokua tunataka kuvitumia, vitu hivyo ni kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye Ubongo(Brain) na kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye Akili (Mind). Sababu ni kwamba tunachanganya tofauti ya ubongo na akili. Ubongo ni mfumo endeshi (operating System upande wa Hardware yaani physical body) wa mwili wa binaadamu ambao umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Ubongo wa mbele, wa kati na wa mwisho….. Roho (Soul) imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Mind, Intellect na Impression, tunaweza kusema soul ni mfumo endeshi wa mwanadamu ambao unashughulikia mambo ya kiroho na mazingira/Nature (operating system inayoongoza upande wa Software katika mwili wa mwanadamu). Mind ndio inahusika kwenye kufikiria, hasa kwenye kutambua lipi baya na lipi jema.

Memory ni kisehemu katika ubongo ambapo taarifa (data au information) zinachambuliwa, zinahifadhiwa na kutolewa pindi zinapohitajika. Lakini pia Memory/kumbukumbu ni uwezo wa kukumbuka mambo ya zamani kama vile tabia/habits, uzoefu/experience, maarifa/skills, hisia, facts nk. Ubongo na Akili vyote vinatumika katika kuhifadhi kumbukumbu lakini zimetofautiani katika utendaji kazi, hivyo hapa tutaangali jinsi ubongo unavyokusanya taarifa na kuzihifadhi pia na akili jinsi ikusanyavyo.

Taarifa zinazotunzwa na Ubongo(Brain)

Katika ubongo wa mwanadamu sehemu inayohusika kuhifadhi kumbukumbu inaitwa Hippocampus ambapo kama sijasahau inapatikana katika ubongo wa kati, Ubongo wa mwanadamu hukusanya taarifa(data) mbalimbali kwa kupitia milango mitano ya fahamu ambayo ni Pua (Taarifa za harufu), Ulimi (radha), Macho(taarifa za picha), Masikio (taarifa za sauti), na Ngozi (taarifa kuhisi/sense). Kumbukumbu za mwanadamu zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Kumbukumbu ya muda mfupi (short-term memory) hii utunzwa kwa muda mfupi sana kichwani yaweza kua sekunde,saa au siku na hutokea labda pindi umepishana na mtu barabarana kadri unavyotembea utasahau kama ulikutana na mtu huyo au ukiwa unasoma namba labda za simu baada ya muda utazisahau na Kumbukumbu ya muda mrefu (Long-term memory) hii hutokea pindi kitu ulikiona mara kwa mara au mlitumia muda mrefu kua pamoja hata kwa nusu saa.

Chukulia kwamba ubongo ni CPU ya computer na Flash/Hard Disk yako ni mlango wa fahamu, CPU haina chochote ndani tofauti na sehemu ya kuhifadhi computer ambayo inaitwa Cache Memory hivyo basi unapoweka flash kwenye computer na kufungua vile vitu vilivyomo ndani ya Flash CPU itaviona ba kuvifungua kwenye kioo chako cha computer, lakini pia vile vitu ulivyofungua hua vinatunzwa ndani ya CPU katika eneo hilo liitwalo Cache Memory ili pindi utakapotaka kufungua kitu ulichokifungua muda uliopita computer isichukue muda mrefu lakini jinsi unavyokaa muda mrefu bila kufungua kile kitu ndio Cache memory inakipoteza taratibu.

Sasa kama ilivyo CPU ubongo pia hua haukasanyi data bali huletewa data kwa kutumia milango hiyo ya fahamu niliyoitaja na kuzifanyia (executing data), mfano kama macho yalimuona mtu Fulani sehemu falani mkaongea na kuondoka ubongo wako kupitia macho utachuku data kuhusu mtu huyo kama vile urefu wake, unene,rangi yake,jinsi alivyovaa nk nk piakupitia masikio ubongo utachukua sauti yake, mambo mliyoongea, kama kapaka mafuta Fulani basi ubongo kupitia mapua yako utachukua data hizo kuhusu harufu na kuzihifadhi kwenye Hippocampus.

Blending in….

Kwa siku moja ubongo huhifadhi mabilioni ya taarifa kichwani so kama ulimuona mtu sehemu mkaongea kidogo mkaachana kadri ya muda unavyoenda Folder lililotunza taarifa zake kichwani linazidi kua mbaaaali zaidi kabisa Sasa ikitokea siku umemuona tena Yule mtu labda baada ya miaka kumi ubongo kupitia macho,masikio na mapua utachukua taarifa ya picha ya mwili mzima, sauti yake nk kisha inafananisha/Matching/inaScan vitu hivyo kule kwenye Hippocampus ili kuona kama kuna taarifa zinazomuhusu mtu huyo baada ya kuScan itakuletea machaguo/suggestion kadha zilizofanana na taarifa za mtu huyo sasa hapo utaanza kuchukua zile taarifa za machaguo uliyoyaaona ndani ya kichwa na tarifa za huyo mtu aliyopo mbele yako ndio utaanza kusema sasa hivi wewe sio Fulani, wewe au ni Fulani hapo ubongo unakua unapekua mafaili chapchap ili kupata matokeo mazuri sasa kama Yule mtu anakukumbuka akikuambia “hunikumbuki ni mimi Fulani tulikutana sehemu Fulani mwaka Fulani” ubongo utayachukua hayo maneno na kuyaScan na kupata folder zima la mtu huyo nawe ndio utajikuta unasema aaahaaa ni wewe ilikua hivi na hivi..
Hivyo basi kumbukumbu zote zinazohifadhiwa na ubongo ni kwa ajli ya kumuwezesha mwanadamu kuyakabili mazingira yake na vyote vinavyomzunguka .
NB: Taarifa zinazokusanywa huitwa data lakini zikishachambuliwa na kufanyiwa kazi huitwa Information, so ukimuona mtu anakua ni data ubongo ukimchambua jinsi alivyo basi anakua information. Au ukiwa na daftar lenye maandishi unataka uyahamishie kwenye computer huitwa data lakini pindi ukishaziweka ndani ya computer zitaitwa Information (Wazungu wanaita Disambiguation?, lugha yetu haijitoshelezi katika kutoa tafsiri)​

Kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye Akili (Mind)

Roho
(Soul) imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Mind/Akili, Intellect na Impression.Mind ndio inahusika kwenye kufikiria, hasakwenye kutambua lipi baya na lipi zuri ,Mind imegawanyika katika pande tatu ambazo ni Conscious mind, Unconscious mind na Subconscious Mind …..Subconcious Mind hii ndio sehemu kuu ya Roho (Soul) ambayo kazi yake ni kurekodi shughuli zetu zakila siku ziwe za kimwili au kiroho. Huku juu tumeona jinsi Ubongo unavyokusanya taarifa kupitia milango ya fahamu na kuzihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadae…Akili pia (subconscious mind) hukusanya na kutunza kila taarifa sema kumbukumbu zinazotunzwa na akili huhifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya kiroho.



BIOS (Basic Input/Output system) hiki ni kifaa kidogo ambacho hua kimepachikwa kwenye motherboard ya Computer, kinabeba na kuhifadhi taarifa za Computer husika kama vile jina la computer nk lakini pia kazi yake ni inaongoza mzunguko wa data kati ya Operating system na baadhi ya vifaa vingine vilivyounganishwa kama vile Video Adapter,Hard disk , Keyboard,mouse nk Bila hii chip huwezi kuwasha computer. Sasa basi Soul ni kama Bios chip ya mwanadamu, mwanadamu bila roho si mwanadamu maana Subconscious Mind ndio imebeba taarifa zake zote kama vile wapi alipotoka, wapi alipo, wapi anaenda, vitu upendavyo, hisia, tabia, vitu unavyofahamu kila anachotenda mwanadamu iwe kwa kuwaza,kuongea,kuona,kunusa,kuhifadhi Subconscious Mind hurekodi na kuhifadhi nk nk. Subconscious Mind pia inauwezo wa kuingia kwenye ubongo na kuchukua taarifa/kumbukumbu zote zilizopo humo na kuzihifadhi ila ubongo hauwezi kuingia kwenye Subconscious Mind na kuchukua taarifa.



Kila kilichorekodiwa na kuhifadhiwa kwenye Subconscious Mind huja kutimika katika maisha ya mwanadamu, kila unachokiwaza,kuongea au kutenda sana basi Subconscious Mind huwasiliana na Nature kisha itakua inakulete yale inayoyaona kwako mara nyingi. Kwa mfano ukiwa unawaza kwa muda mrefu kwamba kitu Fulani kitakutokea basi Subconscious Mind inawasiliana na nature kwamba mtu huyu anahitaji na kupenda kitu Fulani basi nature itakuletea kitu hicho ndio maana unashauriwa kujiwazia mambo mazuri tu, na kama hupendi vitu Fulani vikutokee basi usijaribu kukitenda kitu hicho maana nature itakua inakuletea kitu hicho mara kwa mara kwakua Subconscious Mind inakua imesharekodi kwamba unapenda kitu hicho. Ukifa Mungu hana haja na Mwili wako anachukua tu Roho yako maana humo ndio kuna kila taarifa.

Akili na ubongo vyote vinahifadhi kumbukumbu ila akili ikihifadhi kitu basi hakipotei daima lakini ubongo hua unafuta baadhi ya kumbukumbu kama nilivyoeleza, akili inaweza kuchukua taarifa za ubongo ila ubongo hauwezi, akili inaunganisha ubongo,mwili, mazingira/nature na mambo ya kiroho. Kama ubongo ni hardware basi akili ni Operating System.

Alamsiki…..

Da’Vinci

-Excelsior​
 
Kwa nyongeza ni kwamba hii njia ya ubongo kusachi vitu ndio hutumiwa na Search Engine mbalimbali kama vile Google,Bing,Yahoo,duckDuckGo nk pindi unapokua unatafuta taarifa kwenye intrnet. Mfano, Taarifa ya vitu vingi inahifadhiwa kwenye servers za Google HQ hivyo unapotaka kutafuta kitu huwezi kufunga safari na kwenda Google HQ kupekua kwenye servers zao kuhusu taarifa Fulani.

Wanachofanya wanakuwezesha wewe mtumiaji kuweza kuingia kwenye server zao kupitia Search Engine yao ya Google. hivyo unaposachi kitu kwenye Google, Google inachukua yale maneno kama “Keywords” kisha itasachi hizo key words kwenye Severs na kutafuta folders zote ambazo zimefanana na hizo keywords kisha itakuletea machaguo/suggested post wewe mtumiaji kazi yako itakua kufungua folder moja moja ili upate kile unachotaka
 
Hadi utakapoeleza akili ni nini na inapatikana sehemu gani ya mwili ndio nitaweza kujadili hoja zako.
It's simple akili ipo(Mind)Ipo ndani ya Soul. Soul ipo ndani ya Ubongo. It's a software part in the brain that can't be seen...But you can feel and see its Function/Role
Ni kama vile Nafsi/Spirit ipo ndani ya Moyo ila huwezi kuiona
Otherwise iwe utofauti kati ya kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye roho na ubongo na hiyo roho inapatikana wapi ndani ya mwili!
Nadhani nimekujibu
 
Nimefurahi kuona umepata muda wa kufuatilia kwa kina na kutafakari kuwa akili ni nini? Zinakaa wapi? Na zinapatikanaje?

unapotaka kujifunza kubali kuwa huru, pima hoja kwa kutokuhusisha imani.

Haya tuanze na title ya uzi wako,

"Utofauti kati ya kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye ubongo(Brain) na kumbukumbu zinazohifadhiwa na akili (Mind"​


Katika title umeandika kuwa kuna kumbu kumbu zinazo hifadhiwa kwenye ubongo na kumbu kumbu zinazohifadhiwa kwenye akili (mind), hapa umemaanisha kuwa akili zina exist nje ya mwili wa binadamu yaani akili sio sehemu ya ubongo, kwamba akili na ubongo ni vitu viwili tofauti (duality),
Huu mtazamo wako ndio ule ule aliokuwa nao bwana RENE DISCARTE karne ya 16 kama sikosei, ni baada ya wanasayansi kuanza kujaribu kuelezea akili ni nini?

Nitajie kumbu kymbu zinazokaa kwenye mind according to your theory nikupe proof kuwa akili inapatikana kwenye ubongo

Nitajie mkuu
 
Me kwa upande wangu naona akili ni Kama battery ya ubongo. Yani Kila kiumbe kina ubongo. Ila uwezo wa kutumia ule ubongo ndio tunaita akili, hii inatokana/inaathiriwa zaidi na mazingira tunayoishi na tunayokutananayo.

Kwa mfano ngombe Ana ubongo, nyani, Simba, chui, mbuzi na viumbe vyote vina ubongo ..lakini namna wanavyotumia bongo zao kufikiri ndio tunaita akili lakini itaathiriwa na mazingira yao Kama wao. Na kwa binadamu pia ..hakuna asiye na ubongo Ila kwa Nini Kuna watu wanaweza kufanya mambo makubwa ilihali wote tuna ubongo?

Hapo ndio uwezo wa akili unapoibuka, Yani akili ni Kama vile computer zilivyo na version mbali mbali window xp,7,8,8.1pro, 10 na Sasa 11 ndivyo akili ilivyo ..Yani uwezo unatofautiana. Jinsi unavyoweza kutumia ubongo wako ndio tunaita akili.

NB: Viumbe vyote vina ubongo lakini siyo Kila kiumbe chenye ubongo kina akili.
 
Scientific ubonge ndo engine light ya uhai wa mwanadamu ubongo unapokufa kila kitu kinakufa moyo unaweza kuzima lakin usife ubongo ukizima unakuwa umekwenda na Maj my point soul roho n imagination tu Hakuna roho kwenye mwili soul au roho n imagination tu
Mleta mada yeye theory yake kwa kifupi ipo hivi, mwili wa binadamu ni sawa na hardware (kompyuta isiyo na window) ukiufaunyia installation ya window (akili/roho) ndio unakuwa mtu mwenye akili

Anamaanisha akili ziko nje ya ubongo
 
Me kwa upande wangu naona akili ni Kama battery ya ubongo. Yani Kila kiumbe kina ubongo. Ila uwezo wa kutumia ule ubongo ndio tunaita akili, hii inatokana/inaathiriwa zaidi na mazingira tunayoishi na tunayokutananayo.
Kwa mfano ngombe Ana ubongo, nyani, Simba, chui, mbuzi na viumbe vyote vina ubongo ..lakini namna wanavyotumia bongo zao kufikiri ndio tunaita akili lakini itaathiriwa na mazingira yao Kama wao. Na kwa binadamu pia ..hakuna asiye na ubongo Ila kwa Nini Kuna watu wanaweza kufanya mambo makubwa ilihali wote tuna ubongo? Hapo ndio uwezo wa akili unapoibuka, Yani akili ni Kama vile computer zilivyo na version mbali mbali window xp,7,8,8.1pro, 10 na Sasa 11 ndivyo akili ilivyo ..Yani uwezo unatofautiana. Jinsi unavyoweza kutumia ubongo wako ndio tunaita akili.

NB: Viumbe vyote vina ubongo lakini siyo Kila kiumbe chenye ubongo kina akili.
Akili sio kama betri , ila ubongo ndio unafanya kazi kwa mfumo wa umeme,

Utofauti kati ya ubongo wa mbuzi na binadamu ni kwamba binadamu ana ubongo mkubwa kuliko hata wa tembo, pia ubongo wake wa mbele ni mkubwa huu ubongo ndio unadeal na logical decision, ila ubongo wa mbele wa mbuzi ni mdogo sana

Sijui unanipata mkuu?

Kuhusu nani kafanya mambo makubwa nani hajafanya hiyo ni mada nyingine unazungumzia habari za memmory zinavyoweza kumfanya binadamu ayabadili mazingira
 
It's simple akili ipo(Mind)Ipo ndani ya Soul. Soul ipo ndani ya Ubongo. It's a software part in the brain that can't be seen...But you can feel and see its Function/Role
Ni kama vile Nafsi/Spirit ipo ndani ya Moyo ila huwezi kuiona

Nadhani nimekujibu
Plan Paris , hapa hajajibu swali lako? Tuelimishe kabla hatujameza hii theory ya Da'Vinci . Else tuelezee alternative theory yako ili tujifunze kwa mapana. Asante ni kwa maarifa.
 
Mind is not a storage facility for it is not a physical organ but rather, a logical processing tool. Hakuna storage yoyote inayoweza kufanyika kwenye mind. Hicho kitu hakipo leo na hata milele.

Kiwa mfano, mtu anaweza akawa na Ubongo usio na akili, kwa mfano mtu kichaa, lakini mtu hawezi kuwa na akili bila ya kuwa na ubongo. Leo umeniangusha sana kwenye post yako hii
 
Mind is not a storage facility for it is not a physical organ but rather, a logical processing tool. Hakuna storage yoyote inayoweza kufanyika kwenye mind. Hicho kitu hakipo leo na hata milele.
Kiwa mfano, mtu anaweza akawa na Ubongo usio na akili, kwa mfano mtu kichaa, lakini mtu hawezi kuwa na akili bila ya kuwa na ubongo. Leo umeniangusha sana kwenye post yako hii
Je umesema haya kwa mujibu wa tafiti au kwa mujibu wa uelewa wako. Je Subconscious mind ni nini? Na inafanya kazi gani???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom