KERO Usumbufu kwa wananchi kutoka kwa Wanajeshi Chuo cha Jeshi CTC Mapinga ni kero kubwa, TPDF shughulikieni hili

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mamsindo

Member
Jan 8, 2010
35
28
Kuna kero kwa wakazi tunaotumia barabara iliyopo mbele ya Chuo cha Jeshi la wananchi wa Tanzania CTC Mapinga, kitongoji cha Kiembeni, Kiharaka Bagamoyo. Ni barabara kubwa kutokea Mingoi kwenda Mbweni (kuvuka daraja la Mpiji). Wanawafyekesha wananchi majani nje la lango lao kuu na pembeni ya uzio wao kuelekea njia ya Mbweni.

Pia, kipindi cha mvua kama sasa, mchanga ambao unaletwa na maji, wanakamata wananchi, waukusanye na kupakia kwenye lori lao ambalo wameliweka hapo barabarani.

Tarehe 8/4 majira ya asubuhi, wamefyekesha wananchi kwa kutumia mabavu, na pia tarehe 30/4 majira ya jioni, wamebebesha wananchi mchanga kwa kutumia mabavu na wahanga wakuu wakiwa Bodaboda.

Ubabe huo unafanyika majira ya asubuhi na jioni wakati wananchi wakiwa wanapita barabarani mbele ya kambi hiyo kuelekea kwenye majukumu yao na jioni wakati wa kurudi. Na wamekuwa wakifanya hivi mara kwa mara.

Viongozi wa Kiserikali wa vitongoji vya Kiharaka, Kiembeni, Tungutungu na hata Mbweni wameshindwa kutatua kero hiyo ambayo ni ya miaka mingi sasa.

Tumechoshwa na hali hii. Sasa sisi wananchi tupite wapi? Je, kazi ya jeshi ni kuwatendea hivi wananchi?

Waathirika wengine ni wakazi wa Kitongoji cha Msongola na Minazi Minane.

Tunaomba uongozi wa Jeshi la ulinzi Tanzania(TPDF), lichukue hatua zinazostahili kwa askari wake na wahakikishe kuwa tatizo hili linakomeshwa.

Tunaomba uongozi wa serikali Wilaya ya Bagamoyo uingilie kati pia.
 
Hatua Zitachukuliwa Hakuna Vitendo Vya Hovyo Namna Hiyo Pia Serikali Haiwezi Kufumbia Macho Uhuni
 
Back
Top Bottom