Usiende kukopa kwa hizi kampuni maarufu za mikopo hasa kwa Watumishi wa Umma

Mangungo II

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
18,022
26,364
Naam!!

Kitambo sijaandika Uzi humu. Mara nyingi ni mchangiaji ila Leo nimepata sababu ya kuandika kitu hapa labda kitawasaidia watu au kuwakumbusha tu.

Kama wewe ni mtumishi wa umma au una ndugu kapata ajira hivi karibuni. Naomba nikuusie.

USIJE JARIBU KUOMBA MKOPO Kwa hizi hizi kampuni maarufu Hasa zile tatu kubwa najua mnazijua nisingependa kutaja majina yake hapa maana mods wa wenge Fulani hivi.

Nachelea kuandika haya sababu ishu iliyomkuta CO-WORKER Mwenzangu.

Alienda kopa kwa Hawa ma LOAN SHARK kampuni Moja inamilikiwa na mama lupaso(inavyosemakana).
Hilo ilikuwa 2014 mkopo uliisha 2017.

Saa kituko kwamba salary ya mwezi huu ilipoingia akakuta Hela pungufu. Kucheki kwenye mfumo wa ESS akakuta amekatwa na Ile kampuni aliyokopa kipindi kile. Tena bonge la deni possibility ya kuisha no miaka 5 ijayo.

Hapa alipo kachanganyokiwa Hana hamu. Kwa MUJIBU wa yeye anasema hajawahi kopa tena kwenge kampuni since 2017 imekuwaje kaingiziwa deni kwenye mshahara wake na hata hio Hela wanaoyosema anadai hajawahi iona mahali kokote.

Hapa Kuna cases kwamba hizi kampuni hata ukimaliza lipa mkopo wako wanaendelea kukata na kukupa deni lingine mkopo ambao hata hujawahi chukua.

Kwakuwa Wana data zako tayari wanaweza kukutapeli wakati wowote.

Au pia yawezakana kampuni hizi wanadili na maafisa utumishi kukudhulumu mshahara wako. Na mbaya zaidi watu Hawa Wana mkono mrefu. Unaweza nenda zuia wasikate kote, kwa Afisa utumishi, polisi, takukuru, mahakama kote wakatembeza TAKRIMA.

Njia salama za mikopo

1. Nenda benki yeyote(japo nao jau kimtindo is afadhali).

2. Jiunge SACCOSS hasa hizi kubwa kubwa Wana mikopo yenye riba nafuu hasa ukiwa mwanachama wao.

Tutahadharishe.
 
Lakini huwa stori hizi sizielewagi sana... Ukiingia mkataba makato si yanapitishwa na afisa utumishi? Na kama kuna makato nisiyoyatambua si ni kwamba namfuata afisa utumishi? Na kama hatayazuia makato hayo si naenda kufungua jalada?... Au?
 
Wahuni walipita mlango wa nyuma wakatoa makato 2017 kabla deni halijaisha!!!! Sasa riba ya miaka 7 saba asikwambie mtu mmmmaezako!!! Hapo mpaka unye she kama mvua
 
Back
Top Bottom