Ushawahi jaribu kupika vitu vipya ukatoa boko?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,197
4,120
Mie napenda kujaribu vitu vipya jikoni, mfano pishi jipya au hata viungo vipya au mchanganyo mpya wa viungo na pishi.

Japo kuna nyakati mara chache siyo mara nyingi huwa nikijaribu mchanganyo mpya wa pishi jipya naharibu ila mara nyingi natoa kitu hadi najisifu.

Kuna pishi nililiona mtandaoni nikalijaribu likawa zuri sana. aliyekuwa anapika alikuwa anaita viliba sasa sijui hili ni jina la kiluga au rasmi (linahusisha ngano)

Basi nikajiona fundi nikaongeza viungo vingine ili kupata radha zaidi wee nimeharibu hata haliliki limekuwa la hovyo kabisa.
 
Napenda sambusa. Siku moja nikaona sio mbaya nikijipikilisha mwenyewe sambusa zangu kwa mara ya kwanza

Nikanunua nyama,manda na mazaga mengine Aise kuifunga ile sambusa ilikuwa ni moja ya mtihani mkubwa sana kwangu

Ajabu nikiangalia videos za watu wanavyoifunga naona ni rahisi lakini mie nilikuwa naishia kutetemeka mikono 😂

Nikijaribu kuifunga iwe na shape ya sambusa kuna kaupenyo kanabaki huku kwenye kona ya sambusa loh!!
 
Nilipika mchanganyiko wa Viazi unakwangua unachanganya na karot hoho na mayai aisee 😂😂
 
mimi ni mpenzi wachapat zote (kusukuma na maji) niliona shindano moja mshindi alipika chapat za kusukuma akamix na vitunguu vya maji nikasema wacha nijaribu niliharisha the whole night sitaki huo upuuzi
 
SINTOSAHAU ENZI NIPO CHUO MWAKA 2020 SIKU NIMEISHIWA KILA KITU GHETO NIKASEMA ACHA LEO NIFUNGE SIKU KWA KUPIKA UJI WA MCHELE NISIJE FIA HUMU NDANI,AISEE KILE KITU NILICHOTENGENEZA SIJUI KILIKUWA NI NINI 😭😭
 
Tambi unaweka mayai ila mayai yanatakiwa kuwa chini, juu unaweka Nutella na kachumbari, aisee tamu balaa.

Ila alipika babe wangu, abarikiwe mno🙃😄
 
Niliwahi kujichanganya kupika pilau dah sijui nilizidisha nini maana kitu kilitoka boko, cheusi halafu kina harufu tatanishi sana
 
Napenda sambusa. Siku moja nikaona sio mbaya nikijipikilisha mwenyewe sambusa zangu kwa mara ya kwanza

Nikanunua nyama,manda na mazaga mengine Aise kuifunga ile sambusa ilikuwa ni moja ya mtihani mkubwa sana kwangu

Ajabu nikiangalia videos za watu wanavyoifunga naona ni rahisi lakini mie nilikuwa naishia kutetemeka mikono 😂

Nikijaribu kuifunga iwe na shape ya sambusa kuna kaupenyo kanabaki huku kwenye kona ya sambusa loh!!
Umenikumbusha juzi kati jirani alikua anazipika,akaniita nisaidie kuzifunga.Dah Kila nikifunga lazima Kona ibaki wazi.Kiufupi nilishindwa kama wewe.
 
Umenikumbusha juzi kati jirani alikua anazipika,akaniita nisaidie kuzifunga.Dah Kila nikifunga lazima Kona ibaki wazi.Kiufupi nilishindwa kama wewe.

Hahahaha ila ukiangalia mtu anafunga inaonekana rahisi tu
 
Pilau kuku, hahaha sijui hata nilipika nini licha ya kupewa maelekezo kwenye simu kila hatua
 
Back
Top Bottom