Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
27,166
39,486
Ndugu wana JF,

Kwa muda mrefu kumekuwa na masuala mbalimbali yahusuyo kujilipua (kwenda nje ya nchi) ambayo watu wanauliza mmoja mmoja kwa lemgo la kutaka msaada na ushauri namna ya kufika na jinsi ya kuanza maisha huko nje.

Kutokana na kutoa msaada kwa wengi (binafsi) kwa kutumia njia binafsi nimeona nifungue uzi huu ili kuweka mambo yote wazi kwa kadiri itakavyowezekana na kualika wengine pia waweze kutoka maoni yao.

Ndugu zangu nchi yetu ya Tanzania ki uwezo bado ni changa, fursa za kutoka ni chache na hata changamoto ni nyingi. Huko kwa wenzetu fursa ni nyingi ndio maana imekuwa chanzo cha kuvuta wahamiaji wengi sana toka mataifa masikini.

Nchi masikini wenzetu huko mbele raia wao wamejaa haswa kutokana na moyo wa kusaidiana na kuvutana.

Nimeamua nilete hoja hii kama ambavyo wenzetu hufanya huko Nairaland ya Nigeria ili kila mtu mwenye ujuzi au ufahamu juu ya namna ya kutoka (kujilipua) atoe msaada kwa wengine kwenda huko... si lazima wewe binafsi usaidie mtu binafsi NO, hata mbinu tu za jinsi ya kufika huko.

Kabla sijaingia kwenye kiini cha mada naomba nitoe faida na changamoto za kujilipua.

FAIDA
1. Fursa nzuri za kiuchumi na kujiinua hasa ukiwa na malengo.. Wakuu binafsi nimeishi Marekani kwa miaka nane. moja ya faida nilizopata huko ni kujiinua kiuchumi.... binafsi wakati naenda kusoma huko nilijiwekea malengo ya kujenga ghorofa nyumbani, kufungua mashine za kusaga na kukoboa nafaka pamoja na kumiliki fuso za mizigo.

Kipato cha mfanyakazi wa kule ni kikubwa mno kushinda hata cha baadhi ya maboss wetu hapa... hivyo nilijitahidi nilipokuwa kule malengo yangu yaimie... ni kweli baada ya muda huo nilifanikiwa kutimiza yote.

2. Huduma nzuri za afya, Elimu, Sheria, miundombinu.

CHANGAMOTO
1. Changamoto kubwa kwa kuwa kule ni upweke (ku feel home mara kwa mara japo wakati mwingine ukizoea hutoweka)

2. Xenophobia hii ni kwa baadhi ya nchi tu, sio zote.

USHAURI WA WAPI UENDE NA NAMNA GANI UENDE
Kwa wale wahitaji wa masuala ya maisha kujijenga na kuchuma nashauri nchi hizi, USA, UK, NORDIC COUNTRIES, NA WESTERN EUROPE COUNTRIES. kwa Afrika nashauri SA.

Jinsi gani utaenda namna ni nyingi. Naorodhesha baadhi hapo chini.
1. Kwenda kimasomo ambapo unaweza tafuta sponsors then ukapata scolarship itayokuwezesha kupata visa na kujilipua huko baada ya masomo.

2. Kutafuta mwenzi wa nje ambaye atakualika huko kisha mtaoana na kukuwezesha kupata resident permit na baadae uraia.

3. Kuhamisha mataji na biashara njia hii unakubaliwa popote alimradi uwe na biashara halali.

4. Kwenda kwa shughuli za utamaduni

Wenzetu wakenya na wanigeria wameunda mfumo wa kualikana wao kwa wao, kwamba mtu anakutumia barua ya mwaliko, then unakwenda ukifika huko anakutafutia mtu mnaoana kisheria tu ili upate karatasi kisha kila mtu anasika hamsini zake.

Wapendwa mambo ni mengi siwezi andika yote ndio maana nimeanziasha uzi huu tutaendelea kujuzana kwa kairi michango ya watu itakavyokuwa na maswali yatayojitokeza.

Nawakaribisha nyote. Na wote wenye maujuazi au mauzoefu ya huko mbele. Karibuni tusaidiane tujenge taifa letu. Tuwasaidie vijana wakasake fursa.
 
Mkuu inategemea unataka kwenda inchi gani kujilipua. Zipo inchi zipo ulaya lakini utatamani ubaki Africa..sasa wewe nidokeze unataka uende inchi gani?
Mkuu hii ni thread maalumu kwa kupeana uzoefu wa majuu na namna ya kwenda. Ni maalumu kwa wenzetu wanaohitaji kwenda huko. Sio mimi ninayehitaji nimeweka kwa niaba ya wengine. Nimeshaishi USA for 8 years na Denmark.

So ili kupunguza wimbi la thread za ushauri ni vizuri tutiririke hapa ili wengine wajifunze.
 
Binafsi uzi huu nauunga mkono 100% Lakin pamoja na hayo bado kuna changamoto nyingi kufikia hatua ya kuondoka nchini, kuna mambo mengi ambayo niya msingi hasa upande wa Serikali yetu tukufu hasa upande wa Idara ya uhamiaji.

Tz yetu mtu kupata the tu cheti cha kuzaliwa ambacho ni haki ya Mzawa mpaka jasho likutoke, na ikiwezekana na rushwa juu utoe. Ukienda Migiration ili kuanza mchakato wa passport utahenya vibaya.

Kupata card ya chanjo ya homa ya manjano mpaka utahenya.

Lakini pia changamoto nyingine ni mtu kupata Nauli kamili ya kukufikisha mahari unako taka kwenda. Binafsi ninacho elewa wakirahisisha hayo mambo ya juu, naona Tanzania inaweza kubaki na wazee tu.

Sasa nchi gani hii isiyo toa ajira, Mali asili ni nyingi lakini hatujui wala hatuoni uthamani wake, Vyeo vya juu wanapeana wao kwa wao

HAKI YA MUNGU MIMI SIKU NIKIONDOKA NDO BASI TENA. BORA NIKAFIE KWA FARAO KULIKO KANANI AMBAKO SIJAWAHI FIKA.
 
Binafsi uzi huu nauunga mkono 100% Lakin pamoja na hayo bado kuna changamoto nyingi kufikia hatua ya kuondoka nchini, kuna mambo mengi ambayo niya msingi hasa upande wa Serikali yetu tukufu hasa upande wa Idara ya uhamiaji. Tz yetu mtu kupata the tu cheti cha kuzaliwa ambacho ni haki ya Mzawa mpaka jasho likutoke, na ikiwezekana na rushwa juu utoe. Ukienda Migiration ili kuanza mchakato wa passport utahenya vibaya,

Kupata card ya chanjo ya homa ya manjano mpaka utahenya.

Lakini pia changamoto nyingine ni mtu kupata Nauli kamili ya kukufikisha mahari unako taka kwenda.
Binafsi ninacho elewa wakirahisisha hayo mambo ya juu, naona Tanzania inaweza kubaki na wazee tu,
Sasa nchi gani hii isiyo toa ajira, Mali asili ni nyingi lakini hatujui wala hatuoni uthamani wake, Vyeo vya juu wanapeana wao kwa wao

HAKI YA MUNGU MIMI SIKU NIKIONDOKA NDO BASI TENA. BORA NIKAFIE KWA FARAO KULIKO KANANI AMBAKO SIJAWAHI FIKA.
Mkuu ni kweli. Uhamiaji hawatoi passport bila reason. Nafikiri tungebadili huu utaratibu tuwe kama wenzetu ambao passport kwao ni haki ya msingi na unaweza miliki tu.
 
Europe kumekua kugumu sana kuingia siku hizi, ninaona wadada wengi wanaopata mwaliko wa miezi sita wanaingia online dating wakifika nchi hiyo kwani ni rahisi kukutana na mhusika wakati ukiwa pale, wakishaonana dinner mbili tatu anamweleza kuwa amekuja for visiting na inabidi arudi bongo. Kama date amekolea basi atamfuata bongo na mambo yanaendelea kutoka pale.
 
Mkuu hii ni thread maalumu kwa kupeana uzoefu wa majuu na namna ya kwenda. Ni maalumu kwa wenzetu wanaohitaji kwenda huko. Sio mimi ninayehitaji nimeweka kwa niaba ya wengine. Nimeshaishi USA for 8 years na Denmark.

So ili kupunguza wimbi la thread za ushauri ni vizuri tutiririke hapa ili wengine wajifunze.
Mimi nataka kwenda Denmark. Naomba jinsi ya kuingia na fursa zilizopo huko zisizohitaji elimu.yaani nguvu kazi.
 
Mimi nataka kwenda Denmark. Naomba jinsi ya kuingia na fursa zilizopo huko zisizohitaji elimu.yaani nguvu kazi.
Denmark ni nchi ya scandinavia. Ni nchi yenye maisha ya raha na amani sana japo ni nchi ndogo. Njia rahisi kwenda huko unaweza kwenda as tourist then ukifika huko unapambana upate wa kumwoa hata kwa makaratasi tu ili upate kibali cha ukaazi.
 
Back
Top Bottom