Muitikio mdogo wa kusafirisha bidhaa nje ya nchi (Exportation)

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
5,018
12,758
Tqnzania tuna bidhaa nyingi za kilimo,uvuvi,misitu na madini zinazo hitajika nje ya nchi.

Kwenye kuagiza(Import) tumekuwa na kiwango kikubwa cha kuingiza bidhaa kuliko kusafirisha nje (export).

Kwenye kusafirisha mizigo kutoka nje ya nchi kuja Tanzania (Import) wafanyabiashara na waagizaji wa mzigo wanaweza kuagiza kontena moja Peke yake au kushare kontena moja zaidi ya watu 5.

Kwenye kusafirisha mzigo sio lazima mtu mmoja aweke mzigo wote peke yake mnaweza mkashare Container(LCL-Less than Container Load) kwa mizigo inayoendana na inasadia kupunguza gharama. Kama mtu anaweza kujaza Container peke yake (FCL-Full Container Load) ni vyema akapakia peke yake.

Hofu kubwa kwa wengi ni vibali,kodi na gharama za kusafirisha kontena kutoka Tanzania kwenda nchi husika.

Kwa wanao anza unaweza ukatumia kampuni yenye uzoefu na vibali husika, pia mtu anaweza akafatilia wizara husika wakati wa kutoa mzigo.

Changamoto ni uaminifu, mtu akipata mteja wa bidhaa fulani kwenye vipimo au sample anapeleka sahihi baada ya muda anaweka mzigo mchafu
 
Back
Top Bottom