Upigaji wazaa Sifuri shule ya Sekondari Ngarenaro jiji la Arusha ,matokeo form IV

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Shule ya Sekondari ya Ngarenaro iliyopo kata ya Ngarenaro jiji la Arusha, imetia aibu ya Mwaka kwa kuongoza kuibuka na sifuri nyingi zipatazo 54 katika matokeo ya kidato cha Nne , yaliyotangazwa kitaifa jana.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya elimu wamebaini kuwa taizo la anguko la shule hiyo ni diwani wa kata husika ,Isaya Doita ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya elimu jiji la Arusha ambaye amejikita kutafuta maslahi binafsi kutoka kwa wakuu wa shule na walimu wa kawaida jambo linalosababisha walimu kubadilishwa kila kukicha wanaposhindwa kumpatia chochote.

Diwani huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo anadaiwa pia kujipangia utaratibu wa kulipwa posho pindi anapoenda kwenye vikao mbalimbali shuleni hapo,kinyume na utaratibu.

"Huyo diwani amekuwa kero sana kwenye maendeleo ya kitaaluma katika jiji la Arusha, maana anapenda pesa kuliko utendaji ndio maana hata walimu hawana morari wa kufundisha"

Katika hatua nyingine wazazi wa shule ya msingi Mwangaza na Ngarenaro zilizopo katika kata hiyo,wamemlalamikia afisa elimu wa jiji,BAKARI HUSEIN na Diwani DOITA,kuwalazimisha wazazi kulipa kiasi cha sh,5000 kupitia lipa namba kwa ajili ya kuni za kupikia chakula kinachotolewa na mfadhili ,Mount Meru Millers ambaye amekuwa akihudumia chakula kwa zaidi ya miaka mitatu bila kuwepo na usumbufu wowote huku wazazi wakishiriki kununua viamba upishi kupitia kamati zao za shule.

Hata hivyo hadi sasa wanafunzi hawajawahi kupatiwa chakula shuleni jambo ambalo linaoneshwa wazi ni dili la viongozi hao wawili kujipatia asilimia 10 ya fedha hizo .

Suala hilo limekuwa kero kubwa kwa walimu wakuu wa shule zote 49 za msingi jiji la Arusha, kushurutishwa kuhamasisha wazazi kulipa pesa hizo kupitia lipa namba ndipo wapewe chakula na mfadhili ,na kuacha majukumu yao ya kufundisha watoto wakifuatilia usajiri wa lipa namba tofauti tofatu.

Baadhi ya walimu wamelalamikia usumbufu wanaoupata kutoka kwa afisa elimu Bakari,wakidai huo utaratibu ni mpya na umelenga kuwanufaisha wao pindi wanapowalazimisha wazazi kulipa pesa kinyume na utaratibu.

Mmoja ya walimu wakuu alidai kuwa Afisa elimu huyo aliwahi kufanya ziara akiwa na Isaya Doita ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya elimu,katika shule ya Arusha,Ambapo waliomba pesa ya mafuta lakini mkuu wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Njololoi aligoma kutoa pesa hiyo jambo lililowakasirisha kiasi cha kumhamisha kituo cha kazi kwenda shule ya msingi Salei iliyopo kata ya Ungalimited.

images%20(4).jpg
IMG-20230130-WA0215.jpg
Screenshot_20230130-111735_WhatsApp.jpg
 
Nchi ya mazerooooo

Acha tuendele kulea ujingaujing

Na kukata mauno

Ova
 
Walimu hawako motivated, mitoto haina uwezo na ni mikorofi haina despline,wazazi nao hawatoi ushirikiano kwa walimu.mtoto akichapwa kidogo tu nchi nzima watu wanapiga kelele mwalimu aliyemchapa achukuliwe hatua.
Sasa kwa style hiyo mnategemea watafaulu kweli?
 
Sijapita hiyo mitaa muda mrefu kidogo, miss u!

Hata hivyo, hayo matokeo yao yana nafuu ukilinganisha na jamaa zangu huku Dsm!.
 
Hata mimi bro. Nilikuwaga na matembezi yangu ya hisani kutoka Kona Ilboru hadi Mbauda. Shortcut ni roundabout Florida hadi natokezea huko Ngarenaro. Yalikuwa maisha magumu
 
Walimu hawako motivated, mitoto haina uwezo na ni mikorofi haina despline,wazazi nao hawatoi ushirikiano kwa walimu.mtoto akichapwa kidogo tu nchi nzima watu wanapiga kelele mwalimu aliyemchapa achukuliwe hatua.
Sasa kwa style hiyo mnategemea watafaulu kweli?
Mkuu Umesema Kweli,bila nidhamu ya Watoto wetu ni ngumu sana kupata Matokeo mazuri.Pia Ushirikiano kati Wazazi na Walimu ni Muhimu pia.
 
Hawa watoto wanaowaita waalimu wao TICHA badala ya MAADAM AU SIR tusahau matokeo tofauti. Hakuna DISPLINE kwa watoto kwa waalimu wao ndio kisa wanawaita ticha. Sikuwahi kusikia wanafunzi wanawaita waalimu wao hivyo isipokuwa hiki kuzazi cha sasa. Aidha hizo shule zenye nidhamu na ufaulu wao mkubwa hawaiti walimu wao TICHA
 
Shule ya Sekondari ya Ngarenaro iliyopo kata ya Ngarenaro jiji la Arusha, imetia aibu ya Mwaka kwa kuongoza kuibuka na sifuri nyingi zipatazo 54 katika matokeo ya kidato cha Nne , yaliyotangazwa kitaifa jana.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya elimu wamebaini kuwa taizo la anguko la shule hiyo ni diwani wa kata husika ,Isaya Doita ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya elimu jiji la Arusha ambaye amejikita kutafuta maslahi binafsi kutoka kwa wakuu wa shule na walimu wa kawaida jambo linalosababisha walimu kubadilishwa kila kukicha wanaposhindwa kumpatia chochote.

Diwani huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo anadaiwa pia kujipangia utaratibu wa kulipwa posho pindi anapoenda kwenye vikao mbalimbali shuleni hapo,kinyume na utaratibu.

"Huyo diwani amekuwa kero sana kwenye maendeleo ya kitaaluma katika jiji la Arusha, maana anapenda pesa kuliko utendaji ndio maana hata walimu hawana morari wa kufundisha"

Katika hatua nyingine wazazi wa shule ya msingi Mwangaza na Ngarenaro zilizopo katika kata hiyo,wamemlalamikia afisa elimu wa jiji,BAKARI HUSEIN na Diwani DOITA,kuwalazimisha wazazi kulipa kiasi cha sh,5000 kupitia lipa namba kwa ajili ya kuni za kupikia chakula kinachotolewa na mfadhili ,Mount Meru Millers ambaye amekuwa akihudumia chakula kwa zaidi ya miaka mitatu bila kuwepo na usumbufu wowote huku wazazi wakishiriki kununua viamba upishi kupitia kamati zao za shule.

Hata hivyo hadi sasa wanafunzi hawajawahi kupatiwa chakula shuleni jambo ambalo linaoneshwa wazi ni dili la viongozi hao wawili kujipatia asilimia 10 ya fedha hizo .

Suala hilo limekuwa kero kubwa kwa walimu wakuu wa shule zote 49 za msingi jiji la Arusha, kushurutishwa kuhamasisha wazazi kulipa pesa hizo kupitia lipa namba ndipo wapewe chakula na mfadhili ,na kuacha majukumu yao ya kufundisha watoto wakifuatilia usajiri wa lipa namba tofauti tofatu.

Baadhi ya walimu wamelalamikia usumbufu wanaoupata kutoka kwa afisa elimu Bakari,wakidai huo utaratibu ni mpya na umelenga kuwanufaisha wao pindi wanapowalazimisha wazazi kulipa pesa kinyume na utaratibu.

Mmoja ya walimu wakuu alidai kuwa Afisa elimu huyo aliwahi kufanya ziara akiwa na Isaya Doita ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya elimu,katika shule ya Arusha,Ambapo waliomba pesa ya mafuta lakini mkuu wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Njololoi aligoma kutoa pesa hiyo jambo lililowakasirisha kiasi cha kumhamisha kituo cha kazi kwenda shule ya msingi Salei iliyopo kata ya Ungalimited.

View attachment 2500003View attachment 2500005View attachment 2500008
waziri2020 una majungu sana,unazunguka mbuyu mara matokeo ya sekondari,mara diwani mara wakuu wa shule mara afisa elimu,hueleweki umemlenga nani hasa.
Sio mara yako ya kwanza kuja na uzushi kuhusu Elimu Jiji la Arusha ukiwalenga baadhi ya watu na kuwachafua.
Bahati nzuri unafahamika jinsi ulivyo mtambo wa majungu na unaoshirikiana nao.

Bahati mbaya uliowataja kwa majina ni wachapakazi waaminifu na wenye mafanikio kwenye maeneo yao.
Wewe umeshindwa kwenye nafasi yako umebaki kupiga domo,endelea kujishushia heshima udharaulike zaidi.
 
Hata mimi bro. Nilikuwaga na matembezi yangu ya hisani kutoka Kona Ilboru hadi Mbauda. Shortcut ni roundabout Florida hadi natokezea huko Ngarenaro. Yalikuwa maisha magumu
Yaaan utokee Florida kaloleni kwenda Ngarenaro? Unakatishia makao mapya au?

Mbona naona hiyo short cut imekuwa ndefu

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom