Unafanya kazi inayoendana na Taaluma uliyosomea au ndiyo mambo yamekuwa mengi?

Unafanya kazi inayoendana na Taaluma uliyosemea au ndiyo mambo yamekuwa mengi?

  • Ndiyo

  • Hapana

  • Kwanza Hata Kazi Sina

  • Nilichosomea Hakinisaidii

  • Nilipoteza Muda Wangu Chuoni

  • Kikubwa Uhai


Results are only viewable after voting.

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,435
8,254
Wengi tumebahatia kusoma na tuliamua kuchagua kusoma masuala fulani ili yaje yatusaidie kwenye ajira. Kwako Mdau, wewe ulichosoma ndicho unakifanyia kazi kwasasa?
 
Wengi tumebahatia kusoma na tuliamua kuchagua kusoma masuala fulani ili yaje yatusaidie kwenye ajira. Kwako Mdau, wewe ulichosoma ndicho unakifanyia kazi kwasasa?
Serikali ishaanza kuwa dalali haswa inatumia watu wa kujitolea bila posho
 
Kumbuka pale kwenye duties and responsibilities kuna kipengele cha majukumu mengine utapangiwa na supervisor wako so kazi yoyote hakuna itakayo kushinda
 
Kama ulichokisomea unakipenda kweli kweli basi hata ukikosa ajira utatengeneza namna ya kujiajiri ili uweze kukifanya vema.

Mfano, kama ulisomea udaktari ukakosa kuajiriwa muhimbili au kairuki, unaweza kuwa dokta wa majumbani mbona watu kibao wanaumwa majumbani ila wanaokwenda kuwaona na kuwapa msaada ni wachungaji tu madokta hawajatengeneza mfumo.

Muhasibu, kama umekosa ajira ya uhasibu unaweza kujiajiri kwa kuwa auditor wa kampuni private kuwapangia vitabu vyao na mambo ya TRA.

Kama ni mwalimu unaweza fungua tuition center yako.

Kama ni engineer unaweza jiunga na wenzako mkaingia sekta ya ujenzi na kupata kazi kama subcontractors au kusimamia ujenzi wa nyumba za watu soko linauhitaji wa wataalamu wa ujenzi why ukose kazi.

Kama mtu wa human resources unaweza tengeneza kampuni inayodeal human services kama wafanya usafi, mahousegirl, wapishi na kadhalika then ukawa na contract za kuwapa na kuwalipa kwa kuwatafutia kazi kwenye majumba ya watu. Na kadhalika.

So sidhani kama inashindikana wewe kutumia elimu yako ya chuo kwa kujiongeza ingawa ni ngumu mwanzoni especially kama hakuna mtu wa kukuongoza na kukupa directions but ukishasoma codes za mtaa hautaweza kukwama zaidi utafanikiwa kufika mbali.
 
Wengi tumebahatia kusoma na tuliamua kuchagua kusoma masuala fulani ili yaje yatusaidie kwenye ajira. Kwako Mdau, wewe ulichosoma ndicho unakifanyia kazi kwasasa?
Hakinisaidii direct ila kwenda chuo kulinipa uelewa fula i ambao nautumia kwa ninachokifanya sasa
 
Back
Top Bottom