Umuhimu wa Certifications

mastaklass

Member
Apr 5, 2024
9
9
Habari wanajamvi,
Natumai siku hii ya alhamisi imeenda vizuri. Binafsi Mungu amenipa uzima na nia ya kuandika hivi nnavyotaka kuvidondhosha hapa.

Nilikuwa namsikiliza dada mmoja Youtube leo akitema madini kuhusu remote work. Kwamba ina faida kwa waafrika, hasa katika mazingira yetu ya leo, ambapo ajira imekuwa ngumu sana.

Video hii hapa:

View: https://www.youtube.com/watch?v=kFMvUfMDzGA&t=3020s

Kwa ufupi, alizungumzia yafuatayo:

  • Kazi ya “remote” ni halali na inaweza kuwa kazi yenye malipo mazuri. Lorine alikuwa akitengeneza shilingi 160,000 za Kenya (Tshs 3m) kwa mwezi kama afisa wa rasilmali watu lakini sasa anafanya kazi za mtandaoni. (Akiwa huko, alichuma dola 3,000 kwa mwezi, baada ya makato yote).

  • Kuna tahadhari za kuchukua unaposaka kazi za nje. Hii ni pamoja na kuombwa kulipa pesa za vifaa au mafunzo mapema na kupewa kazi bila kupitia mchakato wowote.

  • Kazi za mtandaoni zina ushindani mkubwa, na zinahitaji ujuzi na uzoefu haswa. Makampuni ya mbali yanatafuta vipaji vya kina, nana mchakato wa interview unaweza kuwa mkali.

  • Wafanyakazi wa online ni online contractors. Maana yake ni kwamba unapoteza baadhi ya faida za mfanyakazi wa serikalini, kama vile bima ya afya na likizo ya kulipwa. Hata hivyo, kampuni za ughaibuni zinazoheshimika zina utaratibu wa kuwasapoti wafanyikazi wao.

  • Kuna tovuti nyingi zinazopatikana kusaidia watu kupata kazi kama hizi. Mzungumzaji anapendekeza kutumia tovuti kama vile Beyond the Savanna, We Work Remotely, Working Nomads nk.

  • Ni muhimu kuwa na CV ambayo inaendana ni mifumo ya ATS. ATS ni mfumo/programu ya kuchakata maombi ya kazi. Kampuni nyingi hutumia mfumo huu, ambao hauhitaji upekuzi wa mtu binafsi, na hutema CV/maombi ambayo hayajaandikwa vizuri.

Nilipokuwa namsikiliza, akili ilinikumbusha uzoefu wangu binafsi. Na kazi nilizopata ughaibuni (sijawahi kwenda huko). Mojawapo ya vitu unayohitaji, tofauti na CV iliyoshiba na skills zako, ni certifications.

Certifications ni vyeti unavyopata nje ya shule, inayoonyesha kuwa umebobea kwenye ujuzi fulani. kwa mfano, wahasibu wana CPA, ambayo ni mitihani kadhaa kuonyesha kuwa wanaweza. Dunia ilivyo sasahivi, inabidi uwe nayo kwenye sekta yako pia, vinginevyo ushindani utakumeza.

Kitu kingine, wabongo tuwe serious na committed (tuamue kufanya kazi kweli na kujitolea kufanikiwa). Nimeona karoho fulani ka kujivuta na kujikatia tamaa. Mara "Kiingereza janga la taifa", mara "elimu yetu ni duni". HAPANA. Amua kujifunza. Kijituma, na kutafuta fursa nje ya nchi/mkoa unamoishi.

Fursa zipo nyingi tu, ila inataka watu waliokomaa. Matawi ya juu yana tabia ya kuchuja wote ambao hawapo tayari kutafuta mafanikio kwa nguvu zao zote.

Ewe kijana unayesoma uzi huu, dunia imebadilika sana. Siku za ajira rahisi hazipo tena. Dunia imekuwa kijiji kidogo, kijiji kiganjani.

Amka sasa!!
 
Wote tuseme AMEN
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom