Umuhimu wa mtu kama Bocco Simba unaonekana

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,518
34,322
Kwa Hali ya mambo ilivyo ndani ya Simba hivi Sasa Kuna umuhimu wa kuwa na Kepteni mwenye sifa kama za Bocco.

Mohamed Hussein ni mkongwe ndiyo, Lakini sidhani Kama ana nguvu kubwa ya ushawishi kwa wachezaji wenzake.

Nakumbuka wakati Yanga wamevurugikiwa Kwa kuondoka Kwa Manji, Mwinyi zahera kama kocha aliibeba Yanga mabegani mwake yeye mwenyewe peke yake.

Leo Simba wanaye kocha "professional" Lakini ana kundi kubwa la viongozi wasio na ushawishi klabuni.

Suluhisho ni kuwa na Nahodha atakayeweza kutuliza dhoruba ya mtikisiko huu isiathiri wachezaji. Mohamed Hussein sidhani kama anaiweza kazi hiyo...
 
Nakubaliana na hoja Zimbwe hana kariba ya uongozi( mkimya mno , hana lugha ya kimamlaka, hana constant communication na marefarii awapo uwanjan )plus anakosa advantage ya lugha linapokuja kwenye mechi za kimataifa , ukiacha Bocco Che Malone ana personality nzuri ya kiuongozi.
 
Zimbwe ni bonge la mchezaji pale Simba. Ni mtu sahihi kabisa kuwa nahodha. Ni mzoefu, msikivu, mtulivu, mwenye juhudi kubwa na mwenye ushawishi mkubwa miongoni mwa wenzake. Yote kwa yote, ni mchezaji mwenye uhakika wa namba ndani ya Simba huku akicheza dakika zote 90.
Asipokuwa yeye nahodha, nani sasa awe nahodha?
 
Wachezaji wana fatique! Hata angekuja kepteni kutoka Real Madrid, bado hali ingekuwa ni ile ile tu. Kila mechi lazima Chama, Kapombe, Zimbwe, Inonga, Che Malone, na Saidoo wacheze!!

Ukienda kwa Yanga, mambo ni tofauti kabisa. Ni Djugui Diarra pekee ndiyo anaonekana kucheza mechi nyingi.
 
Swala unahodha tumelalamika muda mrefu Ila viongozi tulionao ndio vichwa ngumu. Simba unahitaji mtu anayeweza kutuliza timu na kufokea wachezaji wazembe.
Umeielewa hoja yangu. Nadhani Mohamedi Hussein amepungukiwa ule ukaka.

Timu ikiwa Iko poa yeyote anaweza kuwa Kepteni. Timu ikiwa kwenye dhoruba hutakiwa Kepteni mwenye haiba ya ukaka mkubwa.
 
Hapana... Zama zake zimepita na heshima aliyoipa Simba kama mchezaji na Kepteni haitasahaulika.
Basi ngojeni kidogo Chasambi akue atapewa kitambaa huwa ni kiongozi mzuri uwanjani kwa Sasa malizieni na Zimbwe
 

Attachments

  • Screenshot_20240329-200830.jpg
    Screenshot_20240329-200830.jpg
    237.5 KB · Views: 2
Hali inazidi kua mbaya mpaka mashabk wa Simba tumeanza kumkumbuka bocco 😂😂😂 wakat tulikua tunasema Amezeeka Akalee wajukuuu
 
hv onani hawamsemi kama aache masihala uwanjani?. viongozi hawasemwi kuwa waache kupokea wachezaji magarasa wa bure?
 
Tena wengine walisema anaroga wachezaji. Hii inasikitisha sana.
Badala tupinge uongozi uliopo,tunatafuta vitu visivyoeleweka
Hakuna kiongozi anayecheza uwanjani.

Mifumo ya Simba na Yanga ni ya kisiasa HAIELEWEKI na sisi tunaikalia kimya.

Tunazungumzia uongozi wa uwanjani na kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ambako ndiko ushindi unapopatikana.

Kepteni ni muhimu sana kwenye timu wakati kama huu.

Mnyiha wa Mbozi hakuna kumkumbuka Bocco kama mchezaji Lakini alipokuwa Kepteni uongozi wake ulionekana.

Unajua kuwa baada ya kocha mtu anayetakiwa kusikilizwa na kuheshimiwa ni Kepteni wa timu??
 
Zimbwe ni bonge la mchezaji pale Simba. Ni mtu sahihi kabisa kuwa nahodha. Ni mzoefu, msikivu, mtulivu, mwenye juhudi kubwa na mwenye ushawishi mkubwa miongoni mwa wenzake. Yote kwa yote, ni mchezaji mwenye uhakika wa namba ndani ya Simba huku akicheza dakika zote 90.
Asipokuwa yeye nahodha, nani sasa awe nahodha?
Msako wa mchawi wa kibonde Simba unaendelea, hapa anatafutwa mtu mmoja wa kumuangushia jumba bovu, kwa kudai ni Tshabalala sijui sio nahodha mzuri , hapo bado sio jibu la kuporomoka kwa simba.

Mi ni uto lialia na naona tu Simba haina muunganiko au formation huu mwaka wa tatu, timu haina mipango ya goli inacheza tu kama Mameload kumiliki Mpira kwa masifa bila faida na haina targets na wachezaji hawana morali wala umakini, Ngoma namuona kakaa vizuri ila hakabi kwa nguvu yuko rojorojo. Kanoute anaonekana ana stress, Selemba yuko satisfied lolote liwalo na liwe, Kibu D anataka kupiga chenga timu nzima ya wapinzani aende akafunge mwenyewe maana anaona wenzake wanazembea na hawaelewi. Team spirit ya mbumbumbu FC iko na Kibu Denis na Chama tu labda kidogo na Saidoo ila wengine wote tucheze tu ilimradi Mpira uishe tukarelax!!

Kepten Tshabalala sio sababu ya kuporomoka Simba, lawama ziende kwa kocha mkuu na kocha msaidizi, na kwa Mo, viongozi wa timu na mashabiki. Hivi mishahara wachezaji wa simba wanalipwa on time!? I doubt on that😊
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom