Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 1,970
- 4,138
Amani iwe nanyi.
Huwa nikiiangalia hii timu ya simba na aina ya wachezaji wake wa sasa hivi kisha nikiilinganisha na ile simba ya kampa kampa tena ya Kocha Patrick Aussem au Didier Da rosa huwa najiuliza ,Je hawa wachezaji wa sasa hivi wangepata kweli namba katika vikosi vya wakati ule.
Tatizo kubwa la Simba ni wachezaji wenye viwango duni.Leo hii tuna wachezaji wasio weza hata kutuliza mpira, kupiga pasi zilizonyooka, wasioweza kupiga mashuti na hata kukimbia.
Uongozi wa Simba unatakiwa ubadilishe timu yake ya maskauti wanaosaka wachezaji. Wachezaji wengi walioletwa katika hii miaka miwili ni magarasa ,tuambiane tu ukweli.
Simba inatakiwa iwape mkono wa kwaheri kina Jobe,freddy,Ngoma,Kennedy,Saido,Onana,Babacar Sarr n.k hawa wanatakiwa waachwe wakatafute changamoto mpya.
Mwisho nimpongeze kocha Abdelhaqq Benchikha kwa kuona kuwa Simba inampotezea muda tu na kuamua kuachana nayo. Huwezi ukawa na wachezaji kama kina Onana , beki Kennedy na washambuliaji kina Jobe na Freddy halafu utegemee timu ifanye vizuri.
YANGA BINGWA TENA.