ULIWAHI KUPOTEZANA NA MTU MLIEKUTANA KWENYE GARI?

mtoto mdogo

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
501
130
Habari Rafiki,
Umewahi kupanda usafiri wa uma kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine?

Kwa bahati nzuri ukakutana na mtu mkazoeana kweli halafu wakati wa kushuka mkapotezana na hukuweza kupata mawasiliano yake?

Uzi huu ni sehemu ya kumtafuta.
Post kisa chako na JF watatusaidia kuisambaza na Fb utampata tu.

 
Kuna usalama wa taifa nilisafiri naye kwenda Makambako, nina imani yupo salama huko alipo, nimekumbuka maongezi yetu
 
Yeah. Nimemkumbuka mpenzi wangu wa zamani Samira, tulikutana kwenye basi la Hood tukitokea Moshi kuja Dar. Yule binti alikuwa ni mrembo hatari. Ilikuwa mwaka 2009, kipindi hiko ndio nimemaliza chuo huku yeye akiwa ndio kamaliza form six.
Mapenzi yetu yalianza kwa kugombania kukaa siti ya dirishani. Dem alikuwa ni mtata hatari, nikatumia diplomasia, nikamwacha akae.
 
Yeah. Nimemkumbuka mpenzi wangu wa zamani Samira, tulikutana kwenye basi la Hood tukitokea Moshi kuja Dar. Yule binti alikuwa ni mrembo hatari. Ilikuwa mwaka 2008, kipindi hiko ndio nimemaliza chuo huku yeye akiwa ndio kamaliza form six.
Mapenzi yetu yalianza kwa kugombania kukaa siti ya dirishani. Dem alikuwa ni mtata hatari, nikatumia diplomasia, nikamwacha akae.
Mlipotezanaje sasa
 
Dah....Shazia....tulipanda wote Basi la Kamata... Kutoka Dar hadi Arusha....1967.... Siku 3 zile za safari zilikuwa za furaha Sana.......uko wapi Shazia? 😍😍
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom