Ulishawahi kumwaga chakula au mboga yote muda mfupi kabla ya kula, ulifanyaje kuokoa jahazi?

Black Opal

JF-Expert Member
Jan 22, 2023
201
263
Wapishi mko njema?

Kwenye harakati za upishi ajali ni kawaida sana, ila zikidi wewe utakuwa hujui kupika ukatafute kitu kingine cha kufanya.

Sasa bwana, kwa upande wangu, kuna kipindi tulikuwa tunahama nyumbani na kazi zilikuwa nyingi, moja ya jukumu langu ilikuwa ni kupika maharage (nikikupia uharage lazima ukae) wakati mwingine alikuwa anakorofisha wali.

Basi nikakorofisha harage likiwa limekolea nazi freshi, ile natoa kwenye sufuria nihamishe kwenye hotpot si sufuria ikateleza, uharage wote ukaishia mguuni. Aisee niliungua vibaya sana, na harage la nazi tatu likaenda hivyo, ikabidi twende kwa mama ntilie kununua ya kupima ndio tulie wali😅😅😅😅.


Vipi ilishawahi kutokea kwako hii? Iliokoa vipi jahazi watu wapoze njaa?
 
Back
Top Bottom