geranteeh
JF-Expert Member
- May 21, 2015
- 266
- 619
Za siku wakubwa. Leo naomba niwaletee uzi ambao asili yake ni kutoka kwenye group letu la whatsapp la ISAL Motors juu ya malalamiko kwamba kuna gari fulani ni bora kuliko ingine kwamaana ya kudumu na kutokusumbua. Naomba niwaambie kitu kimoja trust me hakuna gari mbaya bali huwa tunajiuliza tunanunua magari kwa sababu zipi waafrika na wazungu tofauti yetu ndo iko hapa.
Wengi wananunua gari sababu eti ina mwonekano mzuri yaani unamkuta mtu anakwambia yani mi gari fulani naipenda tu yani hata nikiwa vipi ntakuja tu kuinunua. Mwingine labda sababu kuna wenzake wengi wanazo mfano vijana wa mjini kuna kipindi huwaambii kitu kuhusiana na Alteza wakazinunua kama njugu baadae upepo ukabadilika ukaamia kwenye crown lakin nakumbuka wakati tunakua kulikua kuna kipindi cha chaser sijui baloon ikaja mark two yan kuna mtu ananunua gari sababu tu its on trending. Alaf kuna mtu ananunua gari fulani sababu tu ataonekana mtu wa hadhi fulani wazungu wanaita for prestige kama sikosei yani ile sifa tu kwamba fulani anamiliki gar fulani kali sana.
Trust me yani kama unanunua gari kwa sababu yoyote kati ya hizo nikizozitaja hapo juu andika wewe utakua ni mtu wa kulia kila siku unless uko na pesa ndefu ambayo si ya mawazo. Yes kuna mwanangu (sitomtaja jina) aliwahi pata ajali pale maeneo ya dar free market ni ajali ambayo wengi watakuwa wanaikumbuka. Yeye alikua na subaru WRX alimgonga mwamba alikuwa na crown kama sikosei. Siwezi elezea hii ajali lakini ile subaru ya jamaa yangu ilipasuka rejeta kioo kilikua na ufa pia alivunja taa na rim ilipinda ya tairi ya mbele moja. Huwez amini jamaa aliagiza WRX mpya afu fresh kabisa coz ni chizi subaru. Mtu kama huyo mwanangu naomba ni mu exclude maana huwez mkuta akikaa akilalamika kwamba labda prado zinachomokaga tyre au zina ubovu fulani ambao hautibiki.
Nishawahi sikia sana watu wakilalamikia nissan x trail na kuna mzee anayo namba b mpaka leo anapeta nayo na hana presha nkimuuliza ananiambia ina shida za kawaida tu kama changamoto nyingine kwenye magari mengine ambazo zinatatulika. Kiufupi wabongo alieturoga ni mtu mmoja maana huwa hatuna sana udadisi wa mambo. Hizi nissan tunazozilalamikia kila siku kwamba gari mbovu sijui nini ndo gari zilizojazana Nairobi na wanaishi nazo vema kama tunavoishi na toyota hapa Tz sasa ushawahi jiuliza shida iko wapi? Nadhani kuna picha mpaka hapo umeipata akilini mwako wakati nakuleta kwenye mada halisi.
Yani bila kupepesa macho niseme tu wabongo huwa hatujui ni nini tunataka kwa wakati gani na kwa matumizi gani. Yani ukishajua haya. Yote basi hutokaa ukalalamika kuhusiana na gari yoyote utakayoimiliki katika maisha yako. Mimi naamini hakuna gari mbovu au yenye shida fulani kwani zimepita na kukaguliwa vitu vingi sana mpaka kufikia wewe unaendesha hiyo gari. Kuna uzi fulani niliusoma twitter jamaa alisema point kubwa sana ingawa sitoielezea kwa mtiririko aliouongea ila ntaielezea kwa namna nilivoelewa kwamba unamiliki ngamia umeishi nae sana ila baadae ukaja kumiliki farasi lakini matunzo yake unayompa ni kama yale ya ngamia mfano ngamia anatoboa wiki hanywi maji wala chakula alaf umekuja kumiliki farasi unaenda nae kama ulivokua unaishi na ngamia trust me broh utasema hawa wanyama ni legelege sana wala si wastahimilivu. Point yangu hapo igeuze kwenye gari mfano unamiliki starlet zile za zamani alaf ukaja kumiliki crown alaf utunzaji wake unaendelea na mazoea ya starlet trust me utaishia kusema hizi gari ni mbovu zina shida fulani fulani na fulani kumbe ni ww tu.
Kuna hii kasumba imekuja kwamba hizi Nissan dualis huwa zinaungua sana sasa ndugu yangu uliponunua corola yako limited ukaenda kwa fundi mtaani akakuwekea mziki taa kali sijui ukaweka na makolokolo kibao alaf maisha yalaemsa ukaona dualis watu wengi wanazo au ukapenda ilivo basi ukajaaliwa ukainunua then ukarudi kwa yule fundi wako ukamwambia "Nifanyie kama ulivofanya kwenye corola kipindi naiununua maana nilifaidi sana mziki na taa nlikua naona vema" alafu ikaja kuungua hiyo dualis kweli utalalamika kwamba gari ni mbovu zinaungua? come on ndugu zangu hakuna kitu ka hiko.
Hivi ni wangapi ambao gari aliyoinunua aliifanyia tafiti au aliisoma kabla ya kuimiliki au hata baada ya kuinunua alitumia muda kusoma kile kipeperushi cha maelezo na maelekezo ya gari? Kiufupi kama huijui gari yako na unaishi nayo basi shukuru Mungu kwa kukulinda kipindi chote ulichokuwa nayo. Si kwamba nawananga wakuu wangu bali ni katika kupeana elimu tu ili mwisho wa siku wote tuwe safe alaf baada ya hapo ndo tuseme ni mipango ya Mungu lakini si sasa kipindi tunafanya uzembe.
JE NI KWELI KWAMBA KUNA GARI ZINA SHIDA?
Kiufupi mimi huwa siamini katika hili bali nachoamini ni kwamba kila gari imetengenezwa kwa mazingira fulani ambayo ukiyatumia abadani hutokuja kuwa mlalamishi . Kiufupi ni kwamba pindi unapotaka kununua gari kikubwa angalia vitu viwili kwanza angalia mfuko wako utaweza kuhudumia gari hiyo? Mfano mzuri ni hizi gari ambazo ni tofauti na toyota mfano Mazda, Isuzu, Honda, Nissan, BMW, FORD nk kwa hapa Bongo huwa vifaa vyake bei ziko juu sasa jiulize nitakapomiliki gari hii ntaweza kuhudumia kwenye upande wa service? Matokeo yake ndo pale unapoimiliki alaf kwenye service unanunua vifaa ambavyo havina ubora kisa tu ni bei rahisi kwakweli kama ni shock up mjomba basi kila baada ya miezi mitano utakuwa unafunga mpya then mwisho wa siku utalalamika bwana hizi gari ugonjwa wake ni shockup maana kila siku nanunua mpya je ni original? Kuna mwingine atakwambia gari fulani ugonjwa wake ni engine zake zinakufa sana je mnatumia Recommended engine fluid au ndo unaenda dukan unaagiza tu. Nadhani point yangu imeeleweka hapo kikubwa kabla ya kununua jiulize utaweza kuimudu? Trust me guys kama gari ukifunga parts genuine au service ukafanya vile inavotakiwa basi watu wakipiga story za vijiweni we utakua unacheka tu na kutabasamu.
Pili angalia pindi unapotaka kununua gari angalia matumizi yako ni yepi je hilo gari litaweza kuhimili mikiki mikiki ya ruti zako? Mfano mtu anamiliki crown afu ruti zake kuiona lami ni kipengele yani yeye ni kupiga shimo mwanzo mwenga broh unachokitafuta utakipata. Kuna gari zimetengenezwa kwaajili ya mikiki mikiki ya off roads na kuna gari zimetengenezwa ni very luxurious yani. Mfano mzuri wengi huwa wanapenda kununua magari kwa wahindi sababu muhindi gari anaendeshea mjini tu yan gari inaweza ikakaa wiki nzima isigonge shimo yani ni palepale city center na ukimkuta mhindi ana gari ya offroad basi anapigaga shimo kwelikweli na wenzetu ni vile tu wengi wana uwezo unakuta ana gari mbili moja ya mjini ingine ni ya safari za kashkash sasa kama umejiona wewe ni mtu wa mazingira ya lami inataftwa kwa tochi au kila siku ni lazma njia yako upige shimo basi fanya maamuzi sahihi kabla hujaanza kulalamika. Na nafurahi kuona sikuhizi wauzaji au waagizaji wa magari huwa wana andaa threads mbalimbali za kuelezea magari na kutoa ushauri wa matumizi yake ni vile tu wabongo wengi sisi ni wavivu kusoma.
Mwisho naomba nielezee kuhusiana na hii kasumba ya spea. Watu wengi huwa wanalalamika Sana kuhusiana na kupatikana kwa spea original za magari. Wakuu dunia sasa ni kijiji hakuna spea ambayo haipatikan ni swala la pesa yako tu but zinapatikana vema kabisa. Binafsi mtu akinitafta na kuulizia spea hata kama inaonekana mpya kabisaa mimi namwambia ni mtumba na kama ni mpya namwambia ni mpya chaguo liwe lakwake but kununua spea mtumba ni safe zaidi kuliko og ambayo huna uhakika nayo kwamba ni kweli og. Now days watu wanakuletea mzigo wenyewe kabisa na wanakwambia ni mpya yenyewe baada ya simu kadhaa unalia. Uzuri wa spea mtumba huwa ni Original ambayo inakuwa imetoka kwenyw gari kama yakwako kwamaana imetengenezwa kiwandani so its pure og ni vile tu inakuwa imetumika kwa muda fulani nisingependa kuelezea sana nisije badilisha mada kuwa bango la biashara lakini naamini wakuu wangu mmepata darasa fulani na madini kadhaa kama kuna kasoro unaweza ongezea kwani namimi naendelea kujifunza na hakuna kitu napenda kama kujifunza. Kwa leo naomba tuishie hapo mpaka wakati mwingine.